Saturday, June 15, 2013

SHEREHE YA UWT KWA PLO ZAFANA DAR

 Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akiwalaki Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead na Makamu Mwenyekiti wa POL Tayseer Khalid (mwanaume mwenye miwani) Khalid na ujumbe wake walipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, waliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wanne Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.

 Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba (wapili kulia), akiwa na  Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer Khalid, wakati ujumbe wa chama hicho ulipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, iliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi 
 Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO) Jihad Abu Zead akitazama bidhaa za kina mama wa UWT, ujumabe wa Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khali (kulia kwa Jihad), ulipowalisi. Wengine ni Mwenyeji wao, Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migoro na Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
 UNAONA WANAVYOWASHANGILIA! Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimwambia Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, wakati ujumbe wa chama hicho ulipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, iliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni, Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid na Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
 Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Jehad Abu Zead, akimpa kadi mwanachama mpya wa CCM, Mohamed Ali, katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba na Wanne ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wasita niBalozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujaisa
 Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akimzadia nguo, Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, wakati  cha Palestina (PLO) Jehad Abu Zead, akimpa kadi mwanachama mpya wa CCM, Mohamed Ali, katika sherehe maalum iliyoandaliwa na UWT leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Mamia ya wanachama wapya wa CCM ambao wengi wao ni vijana, wakiwa katika picha ya p0amoja na viongozi baada ya kupewa kadi zao katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Kinamama wakimwayamwaya wakati wa sherehe hiyo
 Wengine wakigaragara chini kwa furaha wakati wa sherehe hiyo
 Kikundi cha Vijana wa CCM cha Ilala wakionyesha umahiri wao wa kuchgeza sarakasi wakati wa sherehe hiyo
 Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi akimwekeza jambo, Mwenyekiti wake, Sophia Simba wakati wa sherehe hiyo
 Viongozi wote wa meza kuu wakiwaaga wananchi baada ya sherehe hiyo kufana
 Wana-UWT nao wakiwaaga viongozi kwa furaha
 Mjumbe wa Kamati Tandaji wa PLO, Jihad akionyesha zawadi aliyopewa na wanachama wa UWT katika sherehe hiyo. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba na Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer Khalid

 Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba akizungumza wakati wa sherehe hiyo
 Jihad akizungumza wakati wa sherehe hiyo
 Vijana wanaoshiriki Miss Kanga Party ya Kibaha, wakisalimiana na wageni wa heshima kwenye sherehe hiyo.
 Wana-UWT wakiwa wamemzonga Jihad na hivyo Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi kulazimika kutumia msuli kuwazuia, walipokuwa wakimshangilia kiongozi wakati akiondoka Uwanjani
Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba akiagana na Makamu Mwenyekiti wa PLO baada ya sherehe. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

WAZEE WA ELERAI WAIOMBEA CCM USHINDI

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na wanachama wa CCM kata ya Elerai mara tu baada ya kuwasili kwenye kata hiyo..
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibadilishana jambo na mmoja wa wanachama wakongwe wa kata ya Elerai kabla ya kuanza kwa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa Udiwani ya kata hiyo.
Mbunge wa Vijana mkoani Arusha , Ndugu Catherine Magige akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwataka wakazi wa kata hiyo kutambua thamani ya kura kwa kuichagua CCM.
Naibu Waziri wa Ardhi, Mhe. Goodluck Olemadeye akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwaambia CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa wakati na kila kilichoahidiwa Arusha kitafanyika.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Elerai, Mwl.Emmanuel Laizer,na kuwaambia wana Arusha muda wa kufanya maendeleo ni huu na CCM haina kazi nyingine zaidi ya kuleta maendeleo Arusha.
Mgombea wa kiti cha Udiwani kwa tiketi ya CCM, Mwalimu Emmanuel Laizer akihutubia wakazi wa kata ya Elerai  kwenye mkutano wa kufunga kampeni.
Bibi na mjukuu wake wakifuatilia kwa makini yale yanayosemwa na viongozi wa CCM wakati wa kufunga kampeni za udiwani kata ya Elerai.
Mbunge wa Vijana Arusha ,Ndugu Catherine Magige akisikiliza kwa makini sera za mgombea wa udiwani wa kata ya Elerai ,Mwl. Emmanuel Laizer.
Mboya akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwaelezea kuwa alipotea sana kuishabikia Chadema na amewasihi wakazi wa kata hiyo kutofanya makosa kama kweli wanataka maendeleo.
Wakazi wa kata ya Elerai ,Arusha mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Itikdi na Uenezi Nape Nnauye mara baada ya kufungwa kwa kampeni za uchaguzi wa Diwani, juni 14.2013.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UJUMBE WA CHAMA CHA UKOMBOZI CHA PALESTINA (PLO)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Ukombozi cha nchini Palestina (PLO) uliofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam jana Juni 14, 2013 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR 2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Tayseer Khalid, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Juni 14, 2013. Picha na OMR 4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Tayseer Khalid, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam jana Juni 14, 2013. Kushoto ni Asha-Rose Migiro wa CCM na (kulia) ni Jihad Abu Zneid wa PLO. Picha na OMR
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Asha-Rose Migiro wa CCM, baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam jana Juni 14, 2013. Katikati ni Jihad Abu Zneid wa PLO. Picha na OMR 3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Tayseer Khalid, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam jana Juni 14, 2013. Kushoto ni Asha-Rose Migiro wa CCM na (kulia) ni Jihad Abu Zneid wa PLO. Picha na OMR

CHAMA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA (TUMA) CHAOMBOLEZA KIFO CHA LANGA

165
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  
Chama cha muziki wa kizazi kipya Tanzania (TUMA) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa msanii mahiri wa Hip Hop nchini marehemu Langa Kileo.Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari,marehemu Langa Kileo alifariki siku ya jana jioni katikia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipopelekwa kwa ajili ya matibabu.
Tasnia ya muziki nchini imepata pigo lingine tena kwani ni takribani muda wa wiki 2 tokea msanii mwingine mahiri Albert Mangweha afariki Dunia akiwa nchini Afrika Kusini na kuzikwa  katika makaburi ya Kihonda yaliyopo Mkoani Morogoro.
Tunapenda kutoa wito kwa wasanii wote nchini kujitokeza kwa wingi na kuonyesha upendo pamoja na kutoa ushirikiano katika kipindi hiki kugumu cha msiba wa msanii mwenzetu Langa Kileo.
Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu,ndugu,jamaa,marafiki na mashabiki wote wa muziki nchini na kuahidi kutoa ushirikiano katika wakati huu mgumu kwetu sote.
Tunaamini tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi,Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Langa Kileo.
Amin.
Fredrick Gerson Mariki
Mwenyekiti wa TUMA (TANZANIA URBAN MUSIC ASSOCIATION)

BABA AMKANA MTOTO KISA ANA NYWELE ZA KIARABU.....MAMA AKASIRIKA NA KUMTUPA, POLISI WAMTIA MBARONI

Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Khadija Idd anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro  akidaiwa kumtupa barabarani mtoto wake mwenye umri wa miezi 6 baada ya mwanaume aliyezaa naye kumkataa.

Shuhuda wetu ambaye ni dereva wa bodaboda aliyefahamika kwa jina la Shabani, alisema tukio hilo lilitokea Juni 11, mwaka huu maeneo ya Mafiga karibu na Msikiti wa Mahita ambapo Khadija alichukua uamuzi huo baada ya mwanaume aliyezaa naye kumgomea mtoto kwa madai ana nywele za Kiarabu hivyo si wake.

“Huyu dada alifika kwenye kijiwe chetu akiwa amembeba mtoto mgongoni na kukodi pikipiki ili nimpeleke mjini.
 
“Tulipofika kwenye msitu uliopo karibu na mashamba ya SUA, aliniambia niendeshe spidi kuna mtu anamuwahi. 
Nilitii amri lakini tulipofika mbele kidogo nikashangaa anamtupa yule mtoto.

“Nilipoona vile nilisimama na kumhoji kwa nini anafanya vile, akawa hajibu. Nikamchukua na kumpeleka kituo kikuu cha polisi akiwa hana mtoto. Baadae wasamaria wema walimuokota mtoto akiwa ameumia na kumfikisha polisi,” alisema mtoa habari huyo.


 


Mwandishi wetu alifika katika kituo hicho cha polisi na kufanikiwa kumkuta Khadija akiwa chini ya ulinzi mkali huku mwanaye akitokwa na damu usoni na alipoulizwa kulikoni alisema:
 
“Jamani naomba msamaha, nimefanya hivyo kwa hasira baada ya baba wa mtoto kudai si wake, eti ni Mwarabu wakati yeye ni Mngoni wa Songea, nisameheni sitarudia tena.”

Akizungumza na mwandishi wetu, Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Morogoro, Tausi Mbalamwezi alisema mwanamke huyo amefanya kitendo kibaya na sasa wanamsaka baba wa mtoto ili amlee huku mtuhumiwa akisuburi taratibu nyingine.

 “Yupo hapa na tumemkuta na kadi ya kliniki ikionesha kuwa, baba wa mtoto anaitwa Costa Haule. Huyu hana nia njema na mtoto kwani alitaka kumuua kwa hiyo baada ya kumtibia tunawatafuta ndugu wa mwanaume au baba wa mtoto ili wamlee wakati tukiandaa utaratibu wa kumfikisha mahakamani,” alisema Afande Tausi.
GPL

Rais Kikwete akutana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mark Simmonds jijini London Uingereza leo(picha na Freddy Maro).

Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.

Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila
--- 
Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.

Katika hukumu iliyosomwa jana jioni, mahakama imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa, Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye uongozi.
Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri mahakama ya Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye mahakama za kitaifa.