Monday, September 23, 2013

KUMRADHI!!!

Mniwie radhi wadau, 
Sijawatendea haki kwa siku kadhaa ni kwa sababu zilizo nje ya uwezo.
Nitarejea kuanzia Septemba 28, 2013
Samahani kwa uchovu huu

Thursday, September 5, 2013

Super Feo Express Basi pekee yenye luninga kila kiti cha Abiria Tanzania

 
Basi la Kampuni ya Super Feo Express ambalo Mpaka sasa ndio kampuni pekee ya mabasi Tanzania iliyoweza kufikia viwango vya juu vya ubora wa Mabasi hasa kwa kuweka Luninga kwa kila kiti ili kila abiria aweze kuangalia luninga yake na kuamua nini cha kuangalia kama vile yupo kwenye ndege kubwa za abiria.
 
 Hii ni sehemu ya ndani kwenye viti vya abiria ambapo kila abiria anatumia luninga yake
Mabasi ya kampuni ya Super Feo hupatiwa matengenezo kwa uangalifu wa hali ya juu katika gereji yao Mjini Songea na mafundi wanaotumika ni Watengenezaji wenyewe wa Mabasi haya yaani Wachina kutoka Kampuni ya Yutong ya China


Matengenezo yanaendelea

Wednesday, September 4, 2013

Hivi vyombo vya habari Tanzania vipo Serious?

Mtazamo tu,
Leo ni siku nyingine ambayo nimejiuliza maswali mengi mno,
Tangua naanza kusoma Uandishi wa Habari, Kozi mbalimbali nilizopata nafasi ya kuhudhuria, Semina iwe za Baraza la Habari Tanzania MCT, Umoja wa vyama vya waandishi wa Habari Tanzania UTPC na nyinginezo walimu na watoa mada wamekua wakizungumzia umuhimu wa vyombo vya habari kuwatumikia wananchi. Na hapa ndipo palipo na hoja kuwa vyombo vya habari vyote vinaitumikia jamii.

Baadhi ya walimu na watoa mada niliopata fursa ya kupokea masomo yao ni wahariri wa vyombo vya habari.

Kitaaluma habari yoyote inapaswa kuwa na sifa zifuatazo;
1. Iwe na ukweli usio na mashaka (Accuracy)
2. Iripotiwe kwa wakati unaofaa (Timely)
3. Iwe na uzito unaostahili (Magnitude)
4. Iwahusu watu ambako inatangazwa au kuchapishwa (Proximity)
Na mengine mengi ambayo yanaweza kujadiliwa

Zipo hoja nyingi juu ya maswali ninayojiuliza lakini kimsingi napata tabu sana na kipengee cha nne hapo juu kuhusu sifa za habari. Nacho ni habari kuwahusu wale wanaotangaziwa (Proximity)

Kila ninapoangalia vyombo vya habari vya Tanzania na inawezekana hata nje ya Tanzania, mahali hapa hapana mafanikio. Habari zilizojaa na kupewauzito wa juu kwenye vyombo vya habari iwe Magazeti, Radio ama Televisheni ni zile zinazogusa zaidi wakazi waliopo Dar es salaam ama katika miji mikubwa kama vile Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na kidogo Morogoro. Sio tu habari lakini pia katika maeneo haya ndiko vyombo vya habari vimeweka wawakilishi wao na hata ofisi zao na kwa kufanya hivi hata uwiano wa habari umeathirika.

Hali hii imekwenda hata kwenye usikivu wa Redio na Telesheni na usambazaji wa magazeti. maeneo haya ndio yaliyo na uhakika wa kufikiwa na vyombo vya habari zaidi na kwa uhakika ikilinganishwa na maeneo mengine. 

Najiuliza;
Tunachokisema sicho tunachotekeleza?
Habari nazo zinafuata miji?
Walioko vijijini hawana haki ya habari?
Wamiliki wa vyombo vya habari hawalijui hili?
Mamlaka za Serikali zenye wajibu wa Kuchukua hatua juu ya hili vinafanya nini?

Nionavyo mimi, ipo changamoto katika hili.
1. Vyombo vya habari vinapaswa kuwagusa watanzania wote bila kuwabagua kimaeneo.
2. Wahariri kabla hawachapisha gazeti, kabla hawajarusha taarifa za habari za Radio na Magazeti     
    wajiulize ni kwa kiasi gani wameigusa Tanzania kwa sehemu kubwa (Uwiano)
3. Vinginevyo tukubaliane kuwa hata sisi tunachokisema sicho tunachokifanya

TUJIREKEBISHE

Nimekutana na Da'Marietha Msembele

Kwanza Mimi, pili Da Marietha Msembele na nanilyuuuu!!!