Saturday, August 31, 2013

Friday, August 30, 2013

Breaking news!!!! Marekani yatangaza kuwa Serikali ya Bashar al-Assad imeua watu 1429 kwa silaha za sumu nchini Syria


 John Kerry - Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, 
Alipokua akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika Ikulu ya Marekani (White House)

Na Msigwablog 
Muda mfupi uliopita Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amezungumza na vyombo vya habari na kutangaza rasmi kuwa serikali ya Marekani inajua na ina uhakika wa ushahidi kuwa serikali ya Syria ya Rais Bashar al-Assad imehusika kuwaua watu 1429 wiki iliyopita kwa kutumia silaha za sumu. Kerry amebainisha pia kuwa Kati ya watu Hao wamo watoto 426 waliouawa kwa silaha hizo za sumu.

Aidha Kerry anasema serikali ya Syria imekua ikitumia silaha za sumu na hiyo ni sehemu ya mkakati wake wa kukabiliana na maadui wake huko mashariki ya Kati.

Aidha Waziri Huyu wa mambo ya nje wa Marekani anasema Rais Obama Anajua kuwa kukabiliana na tatizo la Syria kutakua na madhara makubwa lakini potelea mbali.

Haya sasa wadau, shughuli nyingine pevu inanukia Syria.

 Rais wa Syria Bashar al-Assad 
Mtuhumiwa wa kutumia silaha za sumu wiki iliyopita kulikosababisha vifo vya watu 1429



Siku niliyokutana na Sheikh Mkuu wa Tanzania


Ustaadhi Gerson Msigwa na Sheikh Mkuu Issa Bin Simba

Mwaka huu Mahindi ya Chakula bweleleeeee!!!!


Haya ni mahindi yanayonunuliwa na NFRA katika kituo chao cha Mbozi Mkoani Mbeya


Na; Msigwablog
Msimu huu wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA, wamefanikiwa kukusanya zaidi ya tani 160,000 za mahindi kati ya tani zote 200,000 wanazokusudia kununua kutoka kwa wakulima. Mkoani Ruvuma peke yake tayari wamenunua tani 36,000 kati ya tani zote 50,000 wanazotarajia kununua msimu huu

Hali hii imevunja rekodi kwa kuwa Mahindi yamenunuliwa kwa kasi kubwa. Matharani mwaka jana, mahindi kama haya ya safari hii yalinunuliwa kwa muda wa miezi sita lakini safari hii ni ndani ya mwezi mmoja.

Mkurugenzi Mkuu wa NFRA Charles Warwa anasema pamoja na wao kununua mahindi hayo, pia wanaendelea kuzijizatiti kwa kujenga maghala mengi zaidi ili waweze kuhifadhi mahindi yote ndani ya maghala badala ya kuyahifadhi nje.

Mwaka huu NFRA imefanikiwa kupata mahindi mengi kutokana na kununua mahindi kwa bei nzuri ya shilingi 500 kwa kilo moja inayomfikia mkulima moja kwa moja, hali ambayo kwa Mkoani Ruvuma wanunuzi wengine binafsi wameshindwa kuifikia bei hiyo na hata mahindi yao nao wanayapeleka kwa NFRA

SWALI NI JE???? 
Baada ya NFRA kumaliza kununua tani zao 200,000 kwa msimu huu, wanunuzi binafsi wataendelea kununua mahindi ya wakulima kwa shilingi 500 kwa kilo moja? au ndio mwanzo wa Majanga?

Tuesday, August 27, 2013

Hili linaudhi wadauuuuuu!!!



Ndugu zangu???????

Hakuna jambo linanikera wakati wa kazi unakuta mpiganaji anakuja kwenye interview na simu ya Mkononi tena mchina kwa ajili ya kurekodi sauti, halafu anaisogeza mdomoni mwa anayehojiwa.

Kwa wapiga picha this is very unfair. Jamani nunue voice recorder na bei zake sio ghali kivile. tuweke microphone tuonekane serious people.

Na ujumbe huu uwafikie Wamiliki wa vyombo vya habari, wanunulieni waandishi wenu wa habari Voice Recorder, msitake vipindi vya chee kama ni live transmission basi nunue teleporters

Lets change guys!!!! 

Monday, August 19, 2013

Nakumbuka Kama vile kulikua na Kampeni ya kuondoa utitiri wa Minara ya simu, radio, TV nk?

Haya kila anayetaka kurusha matangazo ajenge Mnara wake na vijumba vya walinzi na mafundi.
 Aweke uzio na majenerator yake ya kufua umeme.
Na pia aweke solar power system yake.

Minara hiyo yoooote ingeweza kuwa mnara mmoja na kila mmoja akakobeka virusha matangazo yake hapo. Tafakari..........Chukua hatua.

Wangapi wanamuunga Mkono Dr Harrison Mwakyembe????????

 Nimebahatika kutazama live kipindi cha Jenerali On Monday Chanel Ten. Dr Mwakyembe akizungumza na David Ramadhan kuhusu Shughuli aliyoianza ya kukomesha upitishaji wa dawa za Kulevya viwanja vya ndege na bandari
 Akisisitiza "Hakatizi mtu na dawa za kulevya bila kubambwa"
Uwanja wa Ndege wa Dar es salaam, wenye kashfa ya kutumiwa kupitisha dawa za kulevya

Sunday, August 18, 2013

Monday, August 12, 2013

Majimaji Sports Club sasa kuwa Kampuni

Wadau walioshiriki Mkutano ulipokea taarifa ya Majimaji Sports Clu kuwa Kampuni

Na; Msigwablog 
Hatimaye wadau wa timu ya Majimaji ya Songea almaarufu Wanalizombe wameamua kuwa timu hiyo iwe kampuni na itakayokua ikiuza hisa zake katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

Haijafahamika hisa moja itauzwa shilingi ngapi na kutakua na hisa ngapi lakini kulingana na maelezo ya wadau walioandaa mkutano huu yaani Kampuni ya Tanzania Mwandi hatua hiyo inalenga kukabiliana na changamoto kuu ya timu hiyo ambayo ni ukata.

Silas Mwakibinga ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF anasema sasa wawekezaji mbalimbali wanaweza kununua hisa, kama  inavyofanyika kwa timu za ligi kuu nchini Ulaya hali ambayo itaiwezesha timu hiyo kujiimarisha kiuchumi ikiwemo kuwa na uwanja wake, kusajili wachezaji wazuri na kuwaandaa vizuri kwa mashindano na pia itakua na uwezo wa kufanya biashara.

Mwakibinga anasema tayari baadhi ya wawekezaji wameshaonesha nia ya kununua hisa nyingi na kuwekeza katika timu ya Majimaji wakiamini kuwa mfumo huo unalipa na Majimaji itakua katika nafasi nzuri ya kuwa timu bora zaidi katika timu za soka za Tanzania Bara.

Akiwasilisha Mada kwa niaba ya Mwanasheria Dr Damas Ndumbaro, mwanasheria Abel Ngilangwa anasema kwa kuwa Kampuni sasa Majimaji Sports Club itakua imeachana na mfumo wa kuwa mali ya wanachama na sasa itakua ni mali ya wanahisa na kwamba mwenye hisa nyingi zaidi ndiye atakayekua na sauti zaidi kwenye Kampuni.

Mdau mwingine wa Soka ambaye pia ni mwanasheria Sebastian Walyuba amewashauri wapenzi wa timu ya Majimaji na wanaruvuma kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kununua hisa kwa kuwa hiyo ndio njia pekee itakayowawezesha kushiriki katika timu hiyo vingine watatupwa nje.

Mapema akifungua Mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alisema mfumo huo ni mzuri na akatoa changamoto kwa uongozi wa Kampuni ya Majimaji kuhakikisha timu inashinda katika mechi zake na kwamba kwa kufanya hivyo ndio njia pekee itakayowavutia wawekezaji wengi kuweka pesa zao katika Kampuni hiyo
.........................

Chezea mimi weyeee!!!!!!!

Nakikanyaga

Friday, August 9, 2013

Big Respect!!!!!!

Shoto Mama Mzazi wa Mimi, Kati ni Mimi na kulia Shangazi wa Mimi. Hapa tulikua tunaandaa kinywaji.

Hii kitu imewalipia watu ada hiii, ohooo!!!!!!!

Billionare Oprah Winfrey aonja joto ya ubaguzi wa rangi Uswisi

Oprah Winfrey 

Habari kutoka nchini Uswisi zinasema tajiri mwanamke dunia Oprah Winfrey Raia wa Marekani mwenye asili ya Africa ameonja joto ya jiwe alipoingi katika duka moja nchini Uswisi, pale muuza duka alipokataa kumpa mkoba wa kike (Kipima joto) wenye thamani ya Pauni 24,477 sawa na shilingi milioni 61 kwa madai kuwa hana uwezo wa kumudu gharama za kuununua mkoba huo.

Oprah amekitafsiri kitendo hicho kuwa ni ubaguzi wa rangi, akiamini kuwa muuza duka huyo alimuona kuwa kwake mtu mweusi hawezi kuwa na uwezo wa kununua mkoba huo.

Oprah Winfrey anayetajwa kuwa moja ya matajiri wakubwa wanawake dunia mwenye asili ya Africa anadai alikwenda dukani hapo akiwa simple, na hakukua na viashiria vya mtu maarufu ambaye kwa kawaida hutembea na watu wengi kwa ajili usalama na huduma nyingine anasema alipoingia dukani hapo alipendezwa na mkoba huo uliokua umewekwa ukutani na ndipo alipotaka kuuona ili afanye uamuzi  wakuununua ama la.

Alikwenda nchini Uswisi kuhudhuria harusi ya Tina Turner.

Anasema aliomba mara ya kwanza, muuzaji akamwambia mkoba huo ni ghrama mno hawezi kuimudu bei yake, akauliza mara ya pili bado akapewa jibu hilo hilo na akauliza mara ya tatu bado akapewa jibu hilo hilo hadi alipoamua kuondoka dukani hapo.

mmliki wa duka hilo Trudie Goetz ameomba radhi kwa lililotokea.

Hata hivyo Oprah amekiri kuwa pengine alijibiwa hivyo kwa kuwa muuzaji hamfahamu na kwa sababu Vipindi vyake "Oprah shows" si maarufu nchini Uswisi.

Tayari Oprah Winfrey ametunukiwa tuzo ya ya Rais ya heshima ya juu ya Uraia nchini Marekani ambayo atakabidhiwa na Rais Barack Obama katika Ikulu ya Marekani (White House) Baadaye Mwaka huu.

Haya wadau habari ndio hiyo, Dada ana mihela ya kumwaga hadi anashangazwa na muuza duka anayeona so kumuuzia mwafrika mkoba wa milioni 61.

Thursday, August 8, 2013

Wadau Hii Vipi?

wakati nachanja mbuga mahali nimekutana na Mjadala "Watoto wanaposhiriki kazi kama hii ya kubeba matofari na kupanga matanuru, ni kujifunza kazi ama Ajira mbaya kwa watoto?"

Nilipokutana na Mh Moses Machali Singapore

Shoto Moses Machali (Mb) na Mimi

Nilipokutana na Mheshimiwa Moses Machali nilijifunza kuwa daima binadamu tnapaswa kuwajibika kwa kila wajibu tulionao na ukiwa kiongozi ni muhimu ujifunze kutoka ndani ya Jamii.

Big Up!!!! Mh. Moses Machali.

Wednesday, August 7, 2013

Hongera sana Kaka Julius Mlawa "Mtazamo"

Julius Mlawa - Mtazamo

  • Huyu Jamaa ni mfanyabiashara wa mazao na msindikaji wa unga wa sembe
  • Pia ni msafirishaji wa mizigo
  • Anamiliki Kampuni ya Mtazamo Enterprises
  • anafanya shughuli zake katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Leo nimejisikia kumwambia Hongera sana kwa sababu zifuatazo;
  1. Jinsi anavyoishi kwa ushirikiano na upendo na watu mbalimbali.
  2. Jinsi anavyoendesha shughuli zake na wafanyakazi wake kibinadamu
  3. Jinsi anavyoipenda nchi yake Tanzania
  4. Jinsi anavyopenda maendeleo ya kila mtu
  5. Jinsi anavyowajali watu wanaopigania maisha
  6. Kakaa mbali na ukatili na unyama
  7. Na mengine mengi mazuri mnoooooo
Naamini huu ni mfano wa kuigwa, so lets be smart as he do.

Mnamkumbuka Patrick Betwel Masai?

Wanamichezo Mnamkumbuka Kiungo Patrick Betwel a.k.a Masai

Sunday, August 4, 2013

Taja Mmoja mmoja

Kutoka shoto............... 
 Wapiganajiiiiiiiiiiii
Da' Kele akipiga boksi, utaumiaaaa!!!! Ohooooo!!!!! 
Ka' Mtega na nanii hii wangu.

Wapiganaji wakipiga boksi

Mwenye nani hii twende, mwenye kanani hii twende. Hata Mchina ruksa ahahahaaaaa

Chindiye na Mrs nani hiii


wako?????

Rais Mstaafu Clinton Amtembelea Dr Shein Ikulu zenji


RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BIN CLINTON.NA RAIS DK.SHEIN


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.

Saturday, August 3, 2013

Wadau mnamkumbuka Mwandishi wa Habari Mkongwe Agustino Mbunda?


Huyu ndiye Agustino Mbunda.

Leo nje ya mkutano wa kawaida waandishi wa habari katika Mkoa wa Ruvuma, nimekutana na Mwandishi wa habari wa Siku nyingi Mzee Agustino Mbunda.

Nimefurahi kukutana nae kwa sababu ni miongoni wapiganaji waliofanya kazi kubwa ya kuwaelewesha watanzania juu ya umuhimu wa fani hii.

Kwa wenye kumbukumbu Agustino Mbunda ndiye aliyefichua kashfa ya meno ya tembo mwaka 1988 iliyomhusisha aliyekua mbunge wa Songea Mjini Abdulabi Ally Yusuf, ambaye alitiwa hatiani na mahakama kuu na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 12 Jela.

Mbunda pia ndiye aliyeandika habari kuhusu ugonjwa wa mihogo uitwao Cassava Mealbug ambao uliathiri mashamba mengi na kutishia Hali ya chakula. Maeneo yaliyoathirika ni pamoja ukanda wa mwambao wa ziwa Nyasa. Habari hii ndio ililazimu serikali kuagiza manyigu kutoka nchini Nigeria kwa ajili ya kukabiliana na wadudu wa cassava Mealbug. Inasemekana tatizo lilikomeshwa kutokana na kupandikizwa kwa manyigu hayo ambayo yapo hadi Leo.

Mkongwe huyu wa Habari pia aliandika historia miaka ya mwanzoni mwa 1980, (Tarehe kamili nasearch) aliporipoti juu ya mchezo mchafu unaofanywa na menejimenti ya ghala la mbolea la Makambako Mkoani Iringa, ambapo wakulima walikua wakinyanyaswa kupewa mbolea kwa kuwekewa ukiritimba huku mbolea hiyo ikipelekwa kwa wafanyabiashara na kuuzwa kwa bei juu. Aliyekua waziri Mkuu wakati huo Edward Moringe Sokoine alisafiri usiku kucha hadi Makambako na akafika na kukuta meneja wa ghala hilo kalala, akatuma mtu akamwamshe na alipofika na kuulizwa akakosa majibu na hapohapo kikaota nyasi

Pia aliandika habari kuhusu simba wala watu Tunduru, kukatokea upinzani kutoka kwa baadhi ya maafisa wanyamapori. Mmojawao akaamua kwenda Tunduru na yaliyomkuta nae akaliwa na Simba.

Big Up Mzee Mbunda, tupo pamoja and we are proud of you Sir


























Ruvuma Press wafanya mkutano wao wa kawaida, Mwambungu atoa neno.



Chama cha waandishi wa habari Mkoani Ruvuma Leo kinaendesha mkutano wake wa kawaida. Mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ambaye pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuwa makini katika kazi zao kwa kuhakikisha wanaanza kazi yenye kuwasaidia watanzania kukabiliana na changamoto za maisha ikiwemo kupambana na umasikini.

Aidha Mwambungu ameonya kuwa waandishi wa habari waepuke kuwa mawakala wa kuzalisha milipuko inayovuruga amani na kuleta mifarakano katika jamii.

Mkuu Huyu wa Mkoa ambaye amekua kipenzi wa karibu wa vyombo vya habari pia ametaka waandishi wa habari wajenge tabia ya kupendana, waache kuchimbanachimbana na Daima wajadili mambo yenye manufaa kwao na wananchi wanaowahudumia.

Katika Mkutano huo Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoani Ruvuma Andrew Chatwanga amemuomba Mkuu wa Mkoa na Meya wa Manispaa hiyo Charles Mhagama wasivunje jengo la kitega uchumi la chama hicho lililopo katikati ya mji ambalo Manispaa iliidhinisha livunjwe kutokana na taratibu za mipango miji.

Mwambungu amekubali ombi Hilo na ameisihi Manispaa ya Songea iongeze mwaka mmoja kwa Jengo Hilo kuendelea kuwepo.

Chatwanga pia amemuomba Mkuu wa Mkoa Mwambungu akisaidie chama hicho kutunisha mfuko kwa ajili ya mradi wa uanzishaji wa kituo cha Radio ambacho ununuzi wa vifaa na studio unaendelea kwa kutegemea michango ya wadau.