Wednesday, September 4, 2013

Hivi vyombo vya habari Tanzania vipo Serious?

Mtazamo tu,
Leo ni siku nyingine ambayo nimejiuliza maswali mengi mno,
Tangua naanza kusoma Uandishi wa Habari, Kozi mbalimbali nilizopata nafasi ya kuhudhuria, Semina iwe za Baraza la Habari Tanzania MCT, Umoja wa vyama vya waandishi wa Habari Tanzania UTPC na nyinginezo walimu na watoa mada wamekua wakizungumzia umuhimu wa vyombo vya habari kuwatumikia wananchi. Na hapa ndipo palipo na hoja kuwa vyombo vya habari vyote vinaitumikia jamii.

Baadhi ya walimu na watoa mada niliopata fursa ya kupokea masomo yao ni wahariri wa vyombo vya habari.

Kitaaluma habari yoyote inapaswa kuwa na sifa zifuatazo;
1. Iwe na ukweli usio na mashaka (Accuracy)
2. Iripotiwe kwa wakati unaofaa (Timely)
3. Iwe na uzito unaostahili (Magnitude)
4. Iwahusu watu ambako inatangazwa au kuchapishwa (Proximity)
Na mengine mengi ambayo yanaweza kujadiliwa

Zipo hoja nyingi juu ya maswali ninayojiuliza lakini kimsingi napata tabu sana na kipengee cha nne hapo juu kuhusu sifa za habari. Nacho ni habari kuwahusu wale wanaotangaziwa (Proximity)

Kila ninapoangalia vyombo vya habari vya Tanzania na inawezekana hata nje ya Tanzania, mahali hapa hapana mafanikio. Habari zilizojaa na kupewauzito wa juu kwenye vyombo vya habari iwe Magazeti, Radio ama Televisheni ni zile zinazogusa zaidi wakazi waliopo Dar es salaam ama katika miji mikubwa kama vile Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na kidogo Morogoro. Sio tu habari lakini pia katika maeneo haya ndiko vyombo vya habari vimeweka wawakilishi wao na hata ofisi zao na kwa kufanya hivi hata uwiano wa habari umeathirika.

Hali hii imekwenda hata kwenye usikivu wa Redio na Telesheni na usambazaji wa magazeti. maeneo haya ndio yaliyo na uhakika wa kufikiwa na vyombo vya habari zaidi na kwa uhakika ikilinganishwa na maeneo mengine. 

Najiuliza;
Tunachokisema sicho tunachotekeleza?
Habari nazo zinafuata miji?
Walioko vijijini hawana haki ya habari?
Wamiliki wa vyombo vya habari hawalijui hili?
Mamlaka za Serikali zenye wajibu wa Kuchukua hatua juu ya hili vinafanya nini?

Nionavyo mimi, ipo changamoto katika hili.
1. Vyombo vya habari vinapaswa kuwagusa watanzania wote bila kuwabagua kimaeneo.
2. Wahariri kabla hawachapisha gazeti, kabla hawajarusha taarifa za habari za Radio na Magazeti     
    wajiulize ni kwa kiasi gani wameigusa Tanzania kwa sehemu kubwa (Uwiano)
3. Vinginevyo tukubaliane kuwa hata sisi tunachokisema sicho tunachokifanya

TUJIREKEBISHE