Sunday, March 31, 2013

TANZANIA HAINA HISTORIA YA UMWAGAJI WA DAMU KWA RAIA WAKE HATA WAKATI WA KUDAI UHURU WAKE , ILA SASA TUNAONA DALILI ZA UMWAGAJI WA DAMU KWA BAADHI YA RAIA WAKE.



Waumini wakiwa katika Ibada ya PASAKA
 Waumini

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJERUHI WALIOUMIA KATIKA GHOROFA LILILOPOROMOKA DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakimpa pole kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni mwa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.PICHA NA IKULU.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bw. Yusuf Abdallah ambaye ni mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25, katika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa Ghasia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole kijana Baqir Dhamji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25. Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya MOI.


Saturday, March 30, 2013

UP DATE: KATIKA BONANZA LA PASAKA LINALOENDELAA KATIKA UWANJA WA MAJIMAJI TIMU YA MANDELA YAICHAPA TTC MATOGOLO 2 - 0

Golikipa wa timu ya Mandela Kalugwana God akimpasia mpira mchezejaji wake Shabani Mlope

Katika Bonanza la Pasaka linaloendelea katika viwanja vya majimaji kwa kushilikisha timu mbili  toka Mbeya, ambalo linafanyika ndani ya uwanja wa majimaji leo hii timu ya Mandela baada ya kuchapwa mchezo wa kwanza na timu ya Mbeya Veteran Club bao moja kavu nayo katika mchezo wake wa kwanza. Awamu hii yaichapa timu ya TTC Matogolo  mabao mawili kavu  bila uluma .

Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa Apokea hilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora kutoka kwa Mwakilishi wa JICA nchini Yasunori Onishi

Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na Mwakilishi wa JICA nchini Yasunori Onishi  (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa Japan kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.

Rais Jakaya Kikwete Aelezea Kuhuzunishwa Kwake na Maafa ya Kuporomoka na kusababisha vifo vya watu na majeruhi Kwa Jengo la Ghorofa ya 16 Jijini Dar es Salaam,Atoa Maelekezo Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mheshimiwa Saidi Mecky Sadik pamoja na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova

Rais Jakaya Kikwete
---
Na Ikulu-Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa jana, Ijumaa, Machi 29, 2013, ametembelea jengo lililoporomoka na kusababisha vifo vya watu na majeruhi kwenye Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro mjini Dar es Salaam na amesikitishwa na kuhuzunishwa na maafa yaliyotokana na kuporomoka kwa jengo hilo.

BONANZA LA PASAKA NDANI YA MAJIMAJI - SONGEA

Katika Bonanza la Pasaka linalopofanyika katika uwanja wa majimaji  mjini songea mkoani Ruvuma likiwa linaendelea kwa shamlashamla na bashasha timu ya Mandela ya mjini songea yapigwa moja bila na Timu ya Mbeya Veterani,
Hii ni picha ya Pamoja ya Timu ya Tukuyu mbeya na timu ya Kambarage, wenye jezio nyekundu ni timu ya Kambarage na wenye njano ni Tukuyu ya mbeya katika mchezo huo timu ya kambarage imeichapa tukuyumbeya moja kavu.Tutaendelea kukupa matokeo ambapo sasa timu ya Mandelea imeingia uwanjani kwa mala ingine na timu ya TTC Matogolo

Friday, March 29, 2013

Nikiwa Vekesheni Zhengzhou China

 Nimemaliza safari ya farasi salama

KARIBU SONGEA

WAZEE WA YANGA WAKIPIGA DUA NDANI YA UWANJA WA JAMHURI.

WAKATI yanga wakikabiliwa na kibarua kigumu kesho kwa kupambana wenyeji wao Polisi Moro ambayo imeonekana kuzinduka kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu,wazee wa yanga wamenaswa jioni hii wakipiga duandani ya uwanja wa Jamhuri wakati vijana wao wakiendelea na mazoezi.
Walipohojiwa na Mtandao huu wazee hao walidai kwamba wanamuomba mungu awafanyiwe wepesi kwenye mchezo  kesho walidai kwamba ni mgumu.

Ugumu wa mchezo huo unatokana  timu zote mbili kuwa kwenye mazingila tofauti ambapo yanga wanaoongoza ligi hiyo wanapigania kutwaa ubingwa huku polisi inayoshika nafasi ya tatu kutoka chini ikibabana kujinasua katika janga la kushuka daraja,nani ataibuka kidede tusubiri kesho

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AFIKA KUJIONEA JENGO LA GHOROFA 16 LILILOPOROMOKA JIJINI DAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.

PART OF THE BUILDING THAT COLLAPSED IN DAR ES SALAAM MARCH 29, 2013

RAMBI RAMBI KUTOKA UJERUMANI KUFUATIA KUANGUKA KWA JENGO DAR!

UTU (1)
Umoja wa Watanzania Ujerumani umepokea  kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuanguka kwa jengo mjini Dar es Salaam.tunawapa pole nyingi ndugu na jamaa wa waliopoteza maisha, Umoja Wa Watanzania Ujerumani unaungana na watanzania wote pamoja wafiwa katika maombolezi ya msiba huu mkubwa.
Tunawaombea marehemu wote mungu awaweke mahala pema peponi AMIN

BREAKING NYUZZZZZ.......: MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI EVALIST MUSHI AKAMATWA ZANZIBAR

MTU ANAESADIKIWA KUWA NDIE MUUAJI WA PADRI EVALIST MUSHI WA KANISA KATOLIKI,VISIWANI ZANZIBAR,AMEKAMATWA ALASILI HII MAENEO YA KARIAKOO,ZANZIBAR.

JESHI LA POLISI LIMETHIBITISHA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA HUYO,NA KWENYE NAE KITUONI KWA AJILI YA MAHOJIANO ZAIDI.

PADRI MUSHI ALIUWAWA KWA KUPIGWA RISASI MWEZI ULIOPITWA WAKATI AKIWA KWENYE GARI LAKE KUELEKEA KANISANI KWENYE IBADA YA JUMAPILI.

GLOBU YA JAMII ITALETA TAARIFA KAMILI YA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA HUYO HAPO BAADAE KIDOGO.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lapitisha kuanzishwa kwa kikosi cha uingiliaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana lilikubali kutumwa kwa kikosi cha uingiliaji ili kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya makundi ya waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Nchi 15 wajumbe wa baraza hilo lilipitisha azimio la kuanzishwa kwa kikosi hicho chini ya utaratibu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO.

YANGA KUZINDUA TAWI JIPYA MAREKANI

TUNAPENDA KUWATANGAZIA RASMI MASHABIKI, WADAU NA WAPENZI WOTE WA TIMU YETU YA SOCCER YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB MLIOPO MAREKANI KUWA TUNAZINDUA RASMI TAWI LETU HAPA MAREKANI LITAKALO JULIKANA KAMA YOUNG AFRICANS FAMILY USA. TUNAOMBA UKIPATA TANGAZO HILI MWARIFU NA MWENZIO.

TAREHE: JUMAMOSI 03/30/2013 

MAHALI: KILIMANJARO PASSION RESTAURANT

ADDRESS: 2310 PRICE AVENUE, WHEATON,MD 20902

MUDA:  4:00 PM

KWA MAWASILIANO: 
ALEX KASSUWI : TEL :301 305 9685

YOUNG AFRICANS "DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

KESHO KIBARUA KIKALI CHA NDUGU WAWILI DIMBA LA KAITABA!

SONY DSC
By Baraka Mpenja
Ni vita ya kufa na kupona kati ya watengeneza sukari nchini Tanzania klabu ya Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar watakaokuwa na kazi ngumu ya kuwania pointi tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu  soka Tanzania bara.
Pambano hilo la watengeneza sukari sukari limevuta hisia za mashabiki lukuki wa soka kwa mikoa ya kanda ya ziwa Victoria  huku likitarajiwa sehemu ya kufurahia katika mapumziko ya pasaka.

RAIS KIKWETE, ATEMBELEA ENEO LILIPOTOKEA AJALI YA KUANGUKA GHOROFA JIJINI DAR

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.

Taswira Maalum Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Aongoza Mamia Kuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis Jijini Dar es Salaam Leo

 Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowassa na Mbunge wa Mafia Mhe Abdulkarim Shah alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.