Sunday, December 29, 2013

Niko sawa, ila kwa sasa nje ya uwanja miezi mitatu

Ball control 100% Super, chezea mimi!??

Hongera Majjid Mjengwa, Wadau sisi vipi?




Hongera Majjid Mjengwa,

Wiki hii inayomalizika mdau mwenzetu katika tasnia ya habari, mchambuzi mkongwe, mwandishi kindakindaki, mfuatiliaji na mdadavuaji wa habari na matukio na mengine mengi Majjid Mjengwa ameweka sokoni kitabu chake kinachomuelezea gwiji wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na mpigania ukombozi wa Taifa la Afrika ya Kusini, Hayati Mzee Nelson Rolihlahla Mandela.

Mjengwa ameandika kitabu hiki wakati muafaka na amewatendea haki wanajamii hasa wale ambao ama kwa sababu za umri, zama, ama kwa sababu ya kukosa fursa ama kwa sababu nyingine hawakupata kujua kuhusu mwanasiasa huyo Mkongwe alivyojitolea maisha yake kuipigania Afrika ya Kusini iliyokua imetumbukia katika janga la ubaguzi wa rangi ulioendeshwa na makaburu.

Ni sawa Mjengwa ameandika mengi yenye manufaa kwa jamii na ndivyo alivyo kwa tunayefuatilia maisha yake ya uandishi.

Lakini mimi nimeona katika Blog hii Nimpongeze Ndugu Mjengwa kwa sababu alichokifanya ni wajibu wa kila mtu aliyehifadhi historia, taaluma na fursa ya kukiunganisha kizazi cha sasa  na yale yaliyojiri kabla yake.

Katikati ya mwaka 2013 nilihudhuria kongamonano moja lililomwalika Askofu Mstaafu Norbert Mtega katika Jubilei ya kumpongeza Padre Christian Mhagama mmoja wa waandishi wazuri wa vitabu, Askofu Mtega katika Siku hii alisema “Msomi asiyeandika vitabu ni sawa na Mama mjamzito asiyezaa”

Kwa maana hii Mjengwa na waandishi wengine wa vitabu wanatimiza wajibu wao, na wale wasiofanya hivyo wakati wana taaluma ya kufanya hivyo hawatimizi wajibu wao.

Japo kuwa sijapata nakala ya kitabu cha simulizi za Mzee Mandela cha Mjengwa, mimi ni mmoja wa wasomaji wa Blog ya Mjengwa kila uchao na nimefuatilia maandalizi yake kwa kuwa alikua akiweka kwenye Blog yake kila anapofanya tafsiri ya kile kitabu cha Mzee Madiba cha safari ya Ukombozi yaani “Long work to Freedom” Kwa kweli nikiri kuwa hata mimi sijakisoma kitabu hicho cha Madiba na hivyo nilivutiwa mno na simulizi iliyokua ikitafsiriwa na Mjengwa kwenye Blog yake.

Kuna mengi ya kuyasema lakini katika pongezi nimalizie kwa kusema Hongera sana Mjengwa na hongera kwa kuona umuhimu wa kuchapisha kitabu ili iwe kumbukumbu sahihi kwa kila anayetaka kusoma Simulizi za Mzee Mandela na endelea kufanya hivyo kwa mambo mengine mengi yaliyo hazina kwenye kichwa chako kama ilivyo kwaida yako.

Wadau sisi vipi?

Nauliza swali hili kwa sababu naamini kuwa wengi wanaweza kufanya kama alivyofanya Majjid Mjengwa katika simulizi za Mzee Madiba. Hasa kwa sisi waandishi wa habari na katika hili nawagusa zaidi waandishi wa habari wakongwe ambao mimi naamini wana mambo mengi mazuri ya kukisimulia kizazi hiki cha leo hapa Tanzania kuliko watu wengine.

Ndio, wanahabari tunayo fursa hii kwa sababu tunaona mengi. Najiuliza hapa Tanzania Mwalimu Nyerere amefanya mengi katika kupigania uhuru, kuijenga Tanganyika, kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar na mengine mengi. Yapo yaliyokua kama vitimbwi, yapo yaliyoonesha uthubutu wa hali ya juu, yapo yaliyoonesha kujitolea hata kufa, yapo yaliyoonesha ujasiri ambao unaonekana leo kama vitu visivyowezekana na mengine kibao.

Haya yote yalifanyika mbele ya waandishi wa habari. Jamani tupeni utamu, tupeni historia, achieni kalamu zenu zitembee, msiache uhondo huo uteketee, msisubiri waje wazungu watafiti ndio waandike.

Akina Mzee Abdul Ngalawa, Ahamed Kipozi, Jenerali Ulimwengu, Phili Karashani, Ernest Mrutu, Agustino Mbunda, Ben Kiko, Hamza Kasongo, Mhidin Michuzi na wengine wengi tupeni uhondo.

Si lazima kutafsiri vitabu lakini zipo simulizi kuhusu yale mliyoyaona wakati huo, jinsi nchi ilivyoendeshwa, jinsi mabadiliko yalivyokuja na mengine mengi.

Sisemi kwamba hamjafanya kabisa hapana, najua baadhi huandaa vipindi, huandika makala na kufanya mahojiano lakini isiishie hapo, tuandikieni vitabu, vitangazeni ili watanzania wavinunue na waijue nchi yao ilikotoka. Jenerali Ulimwengu nakupongeza pia kwa kuwa umetekeleza hili.

Nasema hivi kwa sababu naamini kuwa, baadhi ya matatizo yanayotukumba sasa Tanzania yanaweza kutatuliwa kwa nguvu ndogo tu ya sisi wanahabari kutumia kalamu zetu kuwapata taarifa watanzania, kuwakumbusha watanzania na kuwaonesha njia ya kupita.

Leo hii inashangaza kumuona mtanzania akitoa kipaumbele kwa mambo ambayo yanaibomoa nchi, yanavuruga moyo wa kuijenga nchi kwa kujitolea, yanajenga chuki, yanaruhusu wabaya kuivuruga nchi. Tulikotoka haikua hivyo, na nchi za wenzetu kama vile China bado wanafanya yale ambayo sie tulikua tunayafanya kabla ya miaka ya 90.

Najua aya hiyo hapo juu itakua imewachefua baadhi ya watu, lakini niseme sababu hizo zinazotumiwa na baadhi yetu kuhalalisha mambo yanayoigharimu nchi utatuzi wake unapaswa kutenganishwa na jukumu la msingi la kujenga Taifa letu.

Kama kuna wezi, mafisadi ama walafi tuwaache washughulikiwe na vyombo husika. Wasiohusika tukazane kujenga nchi, haiwezekani sote tukawa walalamikaji, sote tunatafuta wala rushwa na wezi na mwisho wa siku sote tukawa wanasiasa. Nchi atajenga nani?

Jamani eheee wakongwe wa Habari andikeni vitabu watanzania wasome enzi za mwalimu watanzania waliishi vipi?

Na je wala rushwa hawakuwepo?

Mafisadi hawakuwepo?

Viongozi legelege hawakuwepo?

Siasa hazikuwepo?

Waaminisheni watanzania kuwa kila mtu anaweza kuwa mpigania nchi yake na akawa shujaa, kama ambavyo Mjengwa amemuandika Mzee Madiba na simulizi nyingi nyingi alizowahi kuandika.


Mwisho nawapenda sana na niliyoandika sio msahafu. 


Tuesday, December 24, 2013

Kwa muda nyumbani Ilembula

 Brigedi Kamanda wangu, Mwite Chester katika pozi pande za Njombe Town
 Babu, wajukuu na Mkamwana. Kutoka Shoto Chester, Wayne, Mzee Partinus Msigwa na My wife wangu nani hiii ahaaa nani huyuuuu, nani hii ntawambia baadaye.
 Mimi na Ka’Fulo
 Wayne na Bibi Mlangadu
 Mimi na Bibi Mlangadu na Cathy Mgunda
 Bibi Agnes Mlangadu akiwa mwenye furaha
 Mama Semahuvi
Mama yangu Mzazi Paskalina Mahuve a.k.a “Semahuvi” akikamilisha mawasiliano ya mambo Fulani ya kula bata kwa wajukuu zake

MERRY CHRISTMAS



Wadau tusherehekee kwa amani upendo na Mshikamano. 
Nawapenda Nyote Mle, Mnywe na nani hiiiiii pia 

Wednesday, December 18, 2013

Tukumbushane Wadau




Kwanza nawapongeza wapiganaji wote tunaoendelea kufanya kazi ya uandishi wa habari ambayo kimsingi ni kazi ya kiutumishi kwa umma.

Naomba tuendelee kutumikia umma wa watanzania na tuendelee kuandika habari zenye maslai kwa umma. Kwangu mimi utumishi wetu utakua na maana na manufaa kwa watanzania kama tutaandika, kutangaza, kuonesha na kuchapisha habari, taarifa na matangazo yenye kuitetea Tanzania na watu wake.

Kwenye kazi ya kuitetea Tanzania na watu wake tusisahau kwamba zipo taarifa nyingine ama habari nyingine licha ya ukweli wake na ubora wake zina madhara kwa Tanzania na watu wake, kwa aidha kuichafua nchi usoni kwa mataifa mengine ama zinawaathiri watanzania.

Naamini tunayajua haya na wengi tunayatekeleza, hebu tuendelee kufanya hivyo na wale wasiofanya oneni umuhimu wa kufanya hivyo ili Tanzania iwe mahali salama pa kuishi na watanzania wafurahie maisha yao licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi ikiwemo umasikini.

Tukiwa tunakumbushana hili hebu pia tukumbushane umuhimu wa kuzingatia weledi, maadili, haiba na staha ya mwandishi wa habari. Tusione haya kujifunza, tusione makosa kukosoana na isiwe hatari kukubali pale unaposhindwa.

Nasema hivyo kwa sababu wapo baadhi yetu ambao kimsingi hata wao wanajua kwamba kazi hii haiendani nao lakini wanalazimisha, matharani kuwa watangazaji bila kujali ubora wa sauti, rafudhi na uwezo wao kiutangaza, wapo wanaofanya uchambuzi magazetini kwenye redio na Televisheni bila kujali kama uchambuzi wao hauna utafiti wa kutosha wala mpangilio, wapo wanaokwenda kukusanya habari bila kujali muonekana wao mbele ya jamii na tabia zao kama zinafanana na kioo cha jamii na wapo wanaochapisha magazeti na vijarida bila kujali yale wanayochapisha kama yana tija ama la.

Nasema bahati nzuri, haya ninayosema sie wenyewe wahusika tunayajua, nashauri tupime wenyewe na kuchukua hatua kabla ya kuhukumiwa na jamii ama kusubiri tupigiwe kelele.

Na sasa tunakwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na baadaye Uchaguzi Mkuu na tayari hekaheka zimeanza leo, nashauri tutumie kalamu zetu kukataza hekaheka hizi kwa sababu zina madhara kwa taifa, muda wake bado japo wapo watakaonikosoa. Tunaliacha taifa liwe linatumia muda mrefu kujadili uchaguzi badala ya maendeleo, tunaliacha taifa ligubikwe na ajenda ya siasa badala ya kupambana na umasikini unaowatafuna watanzania wengi, tunaacha watu wachache wanaotetea maslai yao kuliyumbisha taifa na mwishowe tunawaacha watanzania washindwe kutengeneza ajenda za nchi yao. Ndio, ni sisi waandishi wa habari tunaopaswa kuwajibika kwa hili anayekataa atupishe.

Napiga la Mgambo nikiomba waandishi wenzangu tuwe chanzo cha matumaini kwa watanzania, tusiache nchi ikitupiwa mawe ndani na nje, tusiache matatizo ya watanzania yakawa donda ndugu, na tuwaongoze watanzania kukataa jambo lolote linaloigharimu nchi na watu wake kwa njia ya amani.

Mwisho nawapenda sana na Aluta Continua………..

Taswira mbalimbali za Dar, Nairobi na Kampala

 Bandari Salama (Dar es salaam) kutoka angani
 Unapoachana na jiji la Dar Ukiwa angani

Angani unapokatiza Mlima Kilimanjaro

Angani ukikaribia kutua Uwanja wa Ndega Nairobi (Jomo Kenyatta Airport)

Uwanja wa Ndege Entebe, Kampala Uganda
 Kuelekea Mjini Kampala
 Unaingi Jijini Kampala

ASANTE WADAU KWA SALA ZENU NIMEKWENDA NIMERUDI SALAMA






Thursday, December 5, 2013

Wapiga boksi tulipomaliza kazi maalumu

 Pande za Tukuyu wapiga boksi wakitalii ndani baada ya kazi maalumu. toka Shoto Silvanus Kigomba, Mimi, Jongo, Mwishee na Mary
Nipo na Mzee Mpakatwe (Mngoni Orijino) Kaji Moja leo, ahahahahaaaaa

Tuesday, December 3, 2013

Nimepita Makongolosi Chunya na Nimekutana na Baba Mzazi eeee babaaaa!!!

Nimefurahi sana kukutana na mtu muhimu kwa tasnia ya wanahabari hususani kwa Redio na Luninga. Huyu jamaa anaitwa Lawena Nsonda Maarufu kwa jina la Baba Mzazi, Mzee wa Makongolosi, kama humjui fuatilia vipindi vya mijadala kwa njia ya simu katika Redio na Luninga zote za Bongo. Ametukaribisha vizuri mimi na Mpiganaji mwenzangu Said Makala wa Channel Ten, nyumbani kwake Makongolosi Chunya.
 Shoto mimi na kulia Baba Mzazi babaa eeeeee!!!!
 Pamoja kuanzia shoto mimim Baba Mzaziii na Said Makala
 Makongolosi kuna embe nzuri, tamu lakini cha kusikitisha huishia  kuoza kipindi kama hiki, wenye dhamana ya viwanda na biashara mnajua hiliiiiii!!!
 Mti wa mwembe ukiwa umenona matunda pande za Makongolosi Chunya
Tamu eheeeee!!!!

Na wadau tulipokutana Nyasaland

 Kwanza Shoto John Bukuku wa Full Shangwe, Said Makala wa Channel Ten na Mimi.
Kuanzia Shoto Said Makala, Said Mwishee, Mary, Nasoro Hassan, Mimi, Sheila Simba, Dadi Mnamba, John Bukuku, Suleiman Jongo, Geofrey Lunyungu

Thursday, October 24, 2013

JAMBO BOMBAY(MAMBO YA INDIA)

Hoooo zimepitwa na wakati, hooooo chesesi ya Lori, hapa India ni kujimwaga tu. tena ndinga zinamilikiwa na serikali
 Mjini kumekucha

 Ng'ombe hadi mjini




Wednesday, October 23, 2013

TANGAZO



HYTES the organization I'm representing in Tanzania, has opened its application for Secondary School scholarships. We pay average of Shs. 300,000 per student covering tuition fee, exam fees, books and supplies.


Most of Government school students can benefit alot as the tuition fee ranges to Shs. 20,000. So Shs. 300,000 will cover at least every thing.

Kindly ask as many as students from Songea Boys, Mletele, Ruhuwiko, and other students from secondary schools in Songea  to see attached application, complete the forms and submitt them to me via my e-mail before the deadline of 1st November 2013. 

Friday, October 11, 2013

Kumradhi!!!!

Ndugu za wadau,
Mniwie radhi sana kwa kutokua hewani kwa kipindi kirefu.
Hii ilisababishwa na sababu za msingi zilizoninyima Muda wa kuwapa chakula Kama kawaida.
Sasa nimerejea, twende pamoja.

Monday, September 23, 2013

KUMRADHI!!!

Mniwie radhi wadau, 
Sijawatendea haki kwa siku kadhaa ni kwa sababu zilizo nje ya uwezo.
Nitarejea kuanzia Septemba 28, 2013
Samahani kwa uchovu huu

Thursday, September 5, 2013

Super Feo Express Basi pekee yenye luninga kila kiti cha Abiria Tanzania

 
Basi la Kampuni ya Super Feo Express ambalo Mpaka sasa ndio kampuni pekee ya mabasi Tanzania iliyoweza kufikia viwango vya juu vya ubora wa Mabasi hasa kwa kuweka Luninga kwa kila kiti ili kila abiria aweze kuangalia luninga yake na kuamua nini cha kuangalia kama vile yupo kwenye ndege kubwa za abiria.
 
 Hii ni sehemu ya ndani kwenye viti vya abiria ambapo kila abiria anatumia luninga yake
Mabasi ya kampuni ya Super Feo hupatiwa matengenezo kwa uangalifu wa hali ya juu katika gereji yao Mjini Songea na mafundi wanaotumika ni Watengenezaji wenyewe wa Mabasi haya yaani Wachina kutoka Kampuni ya Yutong ya China


Matengenezo yanaendelea

Wednesday, September 4, 2013

Hivi vyombo vya habari Tanzania vipo Serious?

Mtazamo tu,
Leo ni siku nyingine ambayo nimejiuliza maswali mengi mno,
Tangua naanza kusoma Uandishi wa Habari, Kozi mbalimbali nilizopata nafasi ya kuhudhuria, Semina iwe za Baraza la Habari Tanzania MCT, Umoja wa vyama vya waandishi wa Habari Tanzania UTPC na nyinginezo walimu na watoa mada wamekua wakizungumzia umuhimu wa vyombo vya habari kuwatumikia wananchi. Na hapa ndipo palipo na hoja kuwa vyombo vya habari vyote vinaitumikia jamii.

Baadhi ya walimu na watoa mada niliopata fursa ya kupokea masomo yao ni wahariri wa vyombo vya habari.

Kitaaluma habari yoyote inapaswa kuwa na sifa zifuatazo;
1. Iwe na ukweli usio na mashaka (Accuracy)
2. Iripotiwe kwa wakati unaofaa (Timely)
3. Iwe na uzito unaostahili (Magnitude)
4. Iwahusu watu ambako inatangazwa au kuchapishwa (Proximity)
Na mengine mengi ambayo yanaweza kujadiliwa

Zipo hoja nyingi juu ya maswali ninayojiuliza lakini kimsingi napata tabu sana na kipengee cha nne hapo juu kuhusu sifa za habari. Nacho ni habari kuwahusu wale wanaotangaziwa (Proximity)

Kila ninapoangalia vyombo vya habari vya Tanzania na inawezekana hata nje ya Tanzania, mahali hapa hapana mafanikio. Habari zilizojaa na kupewauzito wa juu kwenye vyombo vya habari iwe Magazeti, Radio ama Televisheni ni zile zinazogusa zaidi wakazi waliopo Dar es salaam ama katika miji mikubwa kama vile Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na kidogo Morogoro. Sio tu habari lakini pia katika maeneo haya ndiko vyombo vya habari vimeweka wawakilishi wao na hata ofisi zao na kwa kufanya hivi hata uwiano wa habari umeathirika.

Hali hii imekwenda hata kwenye usikivu wa Redio na Telesheni na usambazaji wa magazeti. maeneo haya ndio yaliyo na uhakika wa kufikiwa na vyombo vya habari zaidi na kwa uhakika ikilinganishwa na maeneo mengine. 

Najiuliza;
Tunachokisema sicho tunachotekeleza?
Habari nazo zinafuata miji?
Walioko vijijini hawana haki ya habari?
Wamiliki wa vyombo vya habari hawalijui hili?
Mamlaka za Serikali zenye wajibu wa Kuchukua hatua juu ya hili vinafanya nini?

Nionavyo mimi, ipo changamoto katika hili.
1. Vyombo vya habari vinapaswa kuwagusa watanzania wote bila kuwabagua kimaeneo.
2. Wahariri kabla hawachapisha gazeti, kabla hawajarusha taarifa za habari za Radio na Magazeti     
    wajiulize ni kwa kiasi gani wameigusa Tanzania kwa sehemu kubwa (Uwiano)
3. Vinginevyo tukubaliane kuwa hata sisi tunachokisema sicho tunachokifanya

TUJIREKEBISHE

Nimekutana na Da'Marietha Msembele

Kwanza Mimi, pili Da Marietha Msembele na nanilyuuuu!!!

Saturday, August 31, 2013

Tukumbushane, Ufugaji wa kuku unalipa.


 Kazizi kangu ka kuku nyumbani kanaendelea kukua. Mwakani watakua zaidi ya Mia inshallah.
Baba mwenye nyumba