Sunday, April 28, 2013

Taswira Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete,Rais Wa Burundu Pierre Nkurunzinza,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta Wahudhuria Ufunguzi wa kikao cha kumi na moja cha Jumuiya ya Afrika Mashariki

 Marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka laiyekuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda Marehemu Eriya Kategaya wakati wa ufunguzi wa kikao cha kumi na moja cha Jumuiya hiyo jijini Arusha leo mchana. Katika Hoteli ya Ngurdoto.Kutoka kushoto Rais Wa Burundu Pierre Nkurunzinza,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati wa ufunguzi wa kikao cha juu cha kumi na moja cha Wakuu wa nchi wa jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofaniyka jijini Arusha.
 Marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye kikao cha kumi na moja cha Jumuiya hiyo jijini Arusha leo.
 Baadhi wa ajumbe walioshiriki ufunguzi wa kikao cha Juu cha kumi na moja cha Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(11th Extraordinary EAC Summit) kilichofanyika jijini Arusha.Picha na Freddy Maro-IKULU

Tuesday, April 23, 2013

MAJADILIANO KATI YA UJUMBE WA TANZANIA NA BENKI YA DUNIA KUHUSU VIPAUMBELE VYA MAENDELEO YA NCHI YETU YA TANZANIA

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akitoa ufafanuzi wa vipaumbele kwa ujumbe wa Benki ya Dunia.IMG_3736 
Kutoka kushoto ni Mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Dickson Lema, Mchumi wa BOT Bi. Haika Mbaga, Kaimu Balozi Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor na Mchumi wa BOT Bi. Sauda Msemo wakifuatilia majadiliano hayo.IMG_3737 
Kutoka kushoto ni Mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof.  Longinus Rutasitara, Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya uchumi, biashara na uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul Mwafongo wakiandika majadiliano hayo.IMG_3750 
Ujumbe wa Tanzania pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia wakijadili namna ya kuendeleza na kuboresha sekta mbalimbali zilizopewa vipaumbele kwa Tanzania ambavyo ni pamoja na Nishati, Usafirishaji na masuala mazima ya MKUKUTA.IMG_3747 
Wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano.IMG_3758 
Kutoka kushoto ni Meneja wa Ubinafsishaji Sekta ya Maendeleo kanda ya Afrika Bi. Irina Astra Khan, Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser akijibu hoja katika majadiliano hayo. Kulia ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akisikiliza kwa makini.

Chanzo:http://www.fullshangweblog.com

Monday, April 22, 2013

Wawili wafariki dunia katika ajali ya gari

Na Nathan Mtega,Songea
 WATU wawili wamefariki dunia na mmoja akijeruhiwa  katika ajali ya gari iliyotokea Aprili 21 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo la Wino wilayani Songea mkoani Ruvuma katika bara bara ya Songea-Njombe.
 Ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Scania yenye namba za usajili T 974 ANN iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Festo Elia  Kimata(29) ilipata ajali hiyo katika eneo la Wino mtelemkoni kwa kile kilichoelezwa kuwa dereva wa gari hilo alishindwa kuimudu kona hiyo hali iliyosababisha gari kupinduka na yeye  kufariki dunia papo hapo.
 Mtu mwingine aliyefariki dunia katika ajali hiyo ni Fausta Mlelwa(35) mkazi wa kijiji cha Kifagulo kilichopo katika eneo la Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma huku utingo wa gari hilo Lufinus Mayemba(32) akijeruhiwa vibaya na kulazimika kukimbizwa katika hospitali ya Misheni ya Peramiho kwa ajili ya matibabu.
 Ajali hiyo imetokea saa chache baada ya ajali nyingine iliyotokea katika eneo hilo iliyohusisha gari aina ya NOAH iliyokuwa ikitokea mjini Songea kuelekea jijini Mbeya ambayo ilisababisha watu kunusurika kifo kwa kujeruhiwa nba kulazwa katika hospitasli ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.
 Kufuatia kuwepo kwa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo baadhi ya wananchi wameiomba  wakala wa bara bara(TANROAD) mkoa wa Ruvuma kuboresha alama za bara barani katika eneoi hilo na pia serikali kuona uwezekano wa kukiboresha zaidi kituo cha afya cha afya cha Madaba eneo ambalo limekuwa na ajali nyingi.
 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki akitihibitisha kutokea  kwa ajali hiyo kwa njia ya simu alisema anawasiliana na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ili kuona uwezekano wa kufanyia lazi maombi ya wananchi hao.
Mwisho.

WAZIRI WA FEDHA WA TANZANIA DKT WILIAM MGIMWA NA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROF BENNO NDULU WASHIRIKI MAJADILIANO KATI YA UJUMBE WA TANZANIA NA BENKI YA DUNIA JUU YA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO NCHINI TANZANIA

 Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akitoa ufafanuzi wa vipaumbele kwa ujumbe wa Benki ya Dunia.
 Kutoka kushoto ni Mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Dickson Lema, Mchumi wa BOT Bi. Haika Mbaga, Kaimu Balozi Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor na Mchumi wa BOT Bi. Sauda Msemo wakifuatilia majadiliano hayo.
 Kutoka kushoto ni Mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof.  Longinus Rutasitara, Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya uchumi, biashara na uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul Mwafongo wakiandika majadiliano hayo.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser, Meneja wa Social Protection kanda ya Afrika Bi. Lynne D-Sherburne – Benz na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano hayo.
 Wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano.
 Ujumbe wa Tanzania pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia wakijadili namna ya kuendeleza na kuboresha sekta mbalimbali zilizopewa vipaumbele kwa Tanzania ambavyo ni pamoja na Nishati, Usafirishaji na masuala mazima ya MKUKUTA.
 Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop aliyekaa katikati, akitoa ufafanuzi wa mikakati wa vipaumbele hivyo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier na kulia ni Mkurugenzi wa Sekta ya kupunguza umasikini na masuala ya Uchumi kanda ya Afrika Bw. Marcelo Giugale. 
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu akijibu hoja kwa ujumbe wa Benki ya Dunia huku Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akimsikiliza kwa makini. Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC
 

Watu sita wanusurika kifo ajali ya gari Songea

Na Nathan Mtega,Songea
 
 WATU sita wamenusurika kifo baada ya gari waliokuwa wakisafiria kutoka Songea kuelekea jijini Mbeya kupinduka katika eneo la Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma na kusababisha watu hao kujeruhiwa na kukimbizwa katika kituo cha afya cha Madaba kilichopo wilayani Songea.
 
 Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walimuambia mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu kuwa ajali hiyo ilitokea Aprili 21 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi ambapo gari aina ya NOAH yenye namba za usajili T 627 BUX iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Joel Mwakopisya(57)  mkazi wa Mbeya lilipinduka katika eneo hilo na kusababisha majeraha kwa watu sita .
 
Aidha taarifa kutoka katika kituo cha  afya cha Madaba wilayani Songea imewataja majeruhi waliofikishwa katika kituo hicho kuwa ni Erika Kihwanja(79) ambaye alikuwa anatolewa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kupelekwa jijini Mbeya ambae alizimia baada ya tukio hilo na wengine ni Obadia Mwaikosya(55),Grace Daud(29), Luth Joseph(19) na Joshua Said(10) mwanafunzi wa darasa la tatu latika shule ya msingi De Paul ya mjini Songea.
 
 Aidha majeruhi watano wameletwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma ambapo kwa mujibu wa Kaimu mganga mkuu mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt Mahtew Chanangula aliwataja Grace Daud na Erika Kihwanja kuwa ndiyo wenye halimbaya na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deisdedit Nsimeki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuhahidi kutoa taarifa zaidi baada ya uchunguzi kufanyika.
 

Joseph Joseph Mkirikiti “ Kuwa na fikra pana ni kujijengea hazina ya leo na kesho”

Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph Mkirikiti akizungumza katika kongamano lilofanyika katika ukumbi wa St Augustine tawi la songea
Ni baadhi ya wanachuo waliohudhuria wakifatilia kwa makini jambo.
Wadau waliohudhuria katika kongamano kutoka kulia ni William  Mrocky mwanachuo wa St Joseph College of information Technology, wakatikati ni Deus Ndileki pia ni tutorial ass at
St. Joseph Institute of Technology na wakushoto ni Janethy Mollel mwanachuo wa St Joseph College of information Technology.
Wadau mbalimbali wakifatilia kwa makini
Wafanyakazi wa Restless development wakifatilia kwa makini mjadala uliokuwa unaendela ukumbini hapo
Mratibu wa  Restless development Bw. Nicas Ngumba akisima hutuba kwa mgeni rasim
Wanafunzi wa shule ya Songea Girls Secondary School wakiwa katika picha ya pamoja
......................................................................................

 Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Wilaya ya Songea Bw, Joseph Joseph Mkirikiti katika  kongamano la vijana  lililofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha  St. Augustine tawi la songea,

Kongamano hilo liliandaliwa na Restless development shirika lisilo la kiserikali ambalo linalofanya kazi na vijana katika nchi 11 ulimwenguni, ufundisha vijana na jamii kwa ujumla kuhusu afya ya uzazi na makuzi, jinsia, stadi za maisha, elimu ya uraia, ujasiliamali na kuwajengea uwezo vijana waliopo ndani na nje ya shule. Lengo kubwa ni kuwaweka vijana katika mstari wa mbele katika kujiletea maendeleo.

Joseph Mkirikiti amesema kuwa vijana ni kundi muhimu na ndio chachu ya maendeleo katika nchi yoyote ile na hakuna nchi iliyoendelea bila ya kuwatumia vijana kwani ni kundi lenye nguvu na tajiri wa maarifa.
Hivyo  kuachana na tabia ya kujivunia ujana kanakwamba ujana ni wamilele badala yake waone kule wanakokwenda na  wajielekeze katika fikra pana sio fikra finyu,

" Lazima utambue ujana ni ndoto kwa sababu kila dakika unayoyafikiria ni machache sana utayaota,  ndoto zenu zisiwe kutafuta ukubwa bali ziwe za kuwatumikia wanyonge,Nchi yetu inatumia rasilimali nyingi kuwasomesha vijana ambao mwisho wa siku wanaishia mitaani bila kuwa na ajira zinazoeleweka wala kujiajiri wao wenyewe walio wengi wanaosoma kwa malengo yakuwa viongozi na wengine hubagua kazi na hata sehemu za kufanyia kazi ,tutumie vyanzo tulivyo navyo kuleta maendeleo”

Kongamano hili limewakuwakutanisha vijana kutoka katika vyuo mbalimbali na shule za sekondari zilizopo manispaa ya Songea ili kuongeza jitihada katika kutengeneza sekta ya vijana iliyoimara.

 Kwa upande wake Bw. Lucian Sengesela ambaye ni mkufunzi wa chuo cha ualimu songea amesema ujana unakabiliwa na majukumu ya kuwa mzazi wa sasa na wa baadaye ikiwemo changamoto mbalimbali za maisha,maambukizi ya magonjwa hasa hatarishi kama vile ukimwi, changamoto za kimaadili, ukosefu wa ajira na kumiliki rasilimali.

“ ukosefu wa ajira kwa vijana unachangiwa na maadili ya tabia kwani vijana wengi kwa sasa hawana maadili hata maofosini wengi wao wako kisasa  zaidi  kwa kujiona wao ni wasomi, kubagua kazi  kwa kujiona wao ni wasomi hawezi kufanya kazi ambazo haziendani na hadhi yao,  pia wengi wao pale wanapopangiwa kazi vijijini hukataa kuripoti sehemu ya kazi  

Nae Bw. Nicas Ngumba ambaye ni mratibu wa  Restless development amesma  wameona haja ya kuandaa kongamano la vijana ili kuweza kujadili utambuzi wa fursa za uzalishaji mali, ajira na kujiajiri kama msingi wa kutengeneza sekta ya vijana iliyo imara, pia tuweze kutizama mfumo wa elimu na hasa ule wa vyuo ili kuweza kuona uwaandae vipi vijana ili waweze kunufaika na fursa za uzalishaji mali ili waweze kujiajiri wao wenyewe.

Soma Kwa Makini Baadhi ya Dondoo Za Bajeti Ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika iliyosomwa Bunge Mjini Dodoma Leo Ambayo Serikali itatumia Shilingi 328,134,608,000/-Mwaka Ujao Wa Fedha.

  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza
--
 KILIMO KUTUMIA SHS. 328,134,608,000 KATIKA MWAKA WA FEDHA UJAO

Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika inatarajia kutumia jumla ya shilingi 328,134,608,000/- katika mwaka ujao wa fedha.

Takwimu hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza wakati akiwasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2013/14.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi 247,094,320,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na Shilingi 81,040,288,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya maendeleo.

Chiza aliongeza kuwa  Shilingi 210,175,943,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengine (OC) kwa ajili ya Wizara hiyo .

Aidha ,shilingi 25,602,969,000 ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Wizara na Shilingi11,315,408,000 ni Mishahara (PE) ya Bodi na Taasisi zote zilizoko chini ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Kwa upande shughuli za maendeleo, Chiza alisema kuwa Wizara hiyo imetenga kiasi cha shilingi 23,927,000,000 ikiwa ni fedha za ndani na shilingi 57,113, 288,000 ni fedha za Nje.

Wabunge wanatarajia kujadili bajeti ya Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika kwa kipindi cha siku mbili ambapo itahitimishwa kesho.

Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhe. Chiza amesema Serikali inatarajia kufufua Kituo cha Kilimo Anga ili kukiwezesha kuwa na ndege na Wataalam watakaosaidia kudhibiti milipuko ya visumbufu vya mazao hasa Nzige.

Mhe. Chiza amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imekuwa ikitegemea huduma ya ndege kukodi kutoka kwenye mashirika ya kikanda ya kudhibiti nzige wekundu na nzige wa jangwani ambazo wakati mwingine hazipatikani wakati zinazohitajika.

Kufuatia hali hiyo amesema Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imekamilisha viwango vya kiufundi (Technical Specifications) kwa ajili ya kutangaza zabuni ya ununuzi wa ndege moja ya kunyunyuzia viuatilifu.
---

SERIKALI ITAENDELEA KUWAENDELEZA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO NCHINI

SERIKALI inatekeleza mkakati wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini kwa kuwatambua wao na mahitaji  ya mitaji na vifaa ili kutekeleza kazi yao kwa ufanisi.

Kauli hiyo imetolew na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Julius Masele wakati akijibu swali na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani leo mjini Dadoma aliyetaka kujua ni lini wachimbaji wadogo wadogo wa Ng’ombeni, Kalalami, Kigwase watatambuliwa na Serikali na kupewa kipaumbele kwenye uchimbaji, na kupewa mikopo ya kujikimu wakati wakitafuta Madini.

Amesema kuwa katika kutambua umuhimu wa wachimbaji wadogo wadogo Wizara hiyo imeshakwishatoa imetoa jumla ya viwanja 612 vya uchimbaji mdogo wa madini katika maeneo ya Ng’ombeni, Kalalani na Kigwase ikiwa ni hekta 3,864. 

Aidha, Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa na Wakala wa Jiolojia inaendelea kubainisha maeneo yanayofaa kwa uchimbaji mdogo ili yaweze kutengwa kisheria na kugawiwa kwa wachimbaji hao.

Masele alisema kuwa katika utekelezaji wa mkakati huo unashirikisha wachimbaji wenyewe kwa kuimarisha vyama vyao vya kimkoa na chama cha kitaifa (FEMATA) na kujadili masuala yao katika vikao vya pamoja vya kila baada ya miezi sita baina ya wawakilishi wao na Wizara.

Ameongeza kuwa Wizara ya Nishati na Madini inakamilisha taratibu za Mfuko rasmi wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kupata mikopo ya vifaa vya uchimbaji wenye tija.

Aidha , Naibu Waziri huyo amewasisitiza wachimbaji wadogo wadogo kuwa mikopo hiyo wanayopata inapaswa itumike vizuri katika malengo waliyoombea ili wajihakikishie kuzalisha madini mengi na kujiongezea kipato.
--

UDHIBITI WA VISUMBUFU VYA MAZAO

SERIKALI itafufua kituo cha Kilimo Anga kwa kukiwezesha kuwa na ndege na Wataalam ili kujenga uwezo wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Masoko kudhibiti milipuko ya visumbufu vya mazao hasa Nzige.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza wakati akiwasilisha Bungeni Makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo leo.

Mhe. Chiza amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imekuwa ikitegemea huduma ya ndege kutoka kwenye mashirika ya kikanda ya kudhibiti nzige wekundu na nzige wa jangwani ambazo wakati mwingine hazipatikani wakati zinazohitajika hali ambayo husababisha Wizara kutegemea kukodisha ndege kutoka sehemu nyingine.

Amesema Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imekamilisha viwango vya kiufundi (Technical Specifications) kwa ajili ya kutangaza zabuni ya ununuzi wa ndege moja ya kunyunyuzia viuatilifu.

Aidha, Wizara itaweka utaratibu wa kuingia ubia na makampuni binafsi na taasisi zinazotoa huduma kama hizo ili kukijengea uwezo kituo cha Kilimo Anga.

Wakati huo huo, Wizara ya Kilimo, Ushirika na Chakula ilisambaza lita ,6000 za kiuatilifu cha kudhibiti milipuko ya viwavijeshi katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Mbeya, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Geita. Dodoma, Morogoro na Tanga kunusuru hekta 16,418 za mazao ya nafaka.
---

SERIKALI IMEFANIKIWA KUONGEZA WATAALAM WA KILIMO NCHINI HADI KUFIKIA 7,974

Wataalam wa ugani wameongezeka kutoka 3,379 waliokuwepo mwaka 2007 hadi kufikia 7,974 mwezi Juni jana(2012) baada ya Serikali kuajiri wahitimu kutoka vyuo mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Adam Kighoma Malima wakati akijibu swali Mhe. Mch. Dk. Getrude Rwakatare (Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi).

Amesema kuwa mwaka 2007 Serikali ilifanya tathmini ya upatikanaji wa huduma za ugani nchini na kubaini kwamba mojawapo ya vikwazo vikubwa vya upatikanaji wa huduma za ugani kwa ufanisi nchini ni upungufu mkubwa wa wataalam.

Malima ameongeza kuwa matokeo ya tathmini hiyo yalionyesha kuwa kulikuwepo na wataalam 3,379 nchini ikilinganishwa na mahitaji halisi ya wataalam 15,082.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo , Serikali ilianza kutekeleza Mpango wa kuimarisha huduma za Ugani nchini ambapo kuanzia mwaka 2007 Serikali imevifufua vyuo 13 vya kilimo nchini (MATIs) vilivyo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

 “Ukarabati mkubwa wa vyuo vitatu MATI Ukiriguru, Maruku na Naliendele-Mtwara na ukarabati mdogo kwa baadhi ya vyuo kumi vingine umefanyika”. Mhe. Malima alisema.

Aidha, Mhe. Malima amesema kuwa vyuo viwili vya mashirika yasiyo ya kiserikali vilishirikishwa katika kutoa mafunzo yaliyolenga kuongeza idadi ya wataalam wa Ugani na vyuo hivo kwa sasa vina uwezo wa kudahili wanafunzi 3,500 kwa wakati mmoja ikilinganishwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 600 uliokuwepo kabla ya mwaka 2007.
 
* Habari zote za Bunge na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma.

Sunday, April 21, 2013

VIKWAZO VINAVYOCHANGIA KUSHUKA KWA ELIMU WILAYA YA TUNDURU MKONI RUVUMA HIVI NI MOJA WAPO

  picha sio ya tukio halisi
Na Steven Augustino, Tunduru
 Imebainishwa kuwa Mahusiano mabaya kati ya Walimu na Wanafunzi na
 Wanafunzi wadaiwa kukataa kukaa katika mabweni na Hosteli ni miongoni
 mwa vikwazo vya maendeleo ya elimu Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na
 kupelekea Wilaya hiyo kupata matokeo mabaya kwa wanafunzi waliofanya
 mitihani ya Kidato cha pili na cha nne katika kipindi cha mwaka 2011/2012 .

 Hayo yalibainishwa na afisa elimu Sekondari Mwl. Ally Mtamila wakati
 akiwasilisha taarifa ya matokeo ya kidato cha pili na cha Nne
 katikakipindi cha mwaka 2011/2012,

  Kwa mujibu wa tarifa hiyo mwaka 2011 matokeo ya Kidato cha pili Wilaya
 hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia 35%, huku takwimu hizo kwa
 upande wa matokeo ya Kidato cha Nne katika kipindi cha mwaka 2012
 zikionesha kuwa Wilaya hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia 59.46%
 kiwango kilichodaiwa kuwa ni kidogo na kiliifanya Wilaya yao kushika
 nafasi ya mwisho kimkoa.

 Awali aikifungua Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Chande Nalicho
 pamoja na kubainisha kuwa pamoja na serikali kuwa na vipaumbele
 vingine vya maendeleo lakini Elimu ni muhimu ilikujiletea mabadiliko
 ya kweli.

 Dc nalicho aliendelea kueleza kuwa Ili kuwaletea maendeleo wananchi wa
 Tunduru ni lazima wilaya ijikite katika kusimamia elimu na kuhalalisha
 uwepo wao na kwamba wasipo wakazania kusomaa shule maendeleo
 yanayopiganiwa na serikali hayatakuwa na maana yoyote kwao.

 Katika taarifa hiyo Mkuu Dc. Nalicho akatolea mfano wa Takwimu za
 ufaulu wa wanafunzi 2764 waliochaguliwa kujiunga na masomo ya
 sekondari  hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu ni asilimia 60% ya  watoto
 wote waliochaguliwa  kujiunga na masomo ya sekondari.

  Akizungumzia upande wa Shule za Msingi  Mwaka 2011Shule ya Msingi
 Nakapanya ilifaulisha Watoto 26 lakini takwimu zinaonesha kuwa  watoto
 wote hawakwenda shule na kuongeza kuwa hali hiyo inawakatisha tama
 hata walimu wa shule za msingi zinazofaulisha watoto hao .

 Wakichangia kwa nyakati tofauti Mwl. Issa Ngajime alisema kuwa chanzo
 cha kushamiri kwa utoro,uchangiaji hafifu wa chakula mashuleni na
 wanafunzi kukataa kukaa katika hostel zilizojengwa katika shule zao
 Viongozi wa serikali za Vijiji wanasitahili kubeba lawama huku
 wakiwataka viongozi kutochanganya elimu na Siasa kwa kuboresha mbinu
 za kufundishia na kuchukua hatua kwa Wanafunzi ambao wamekuwa
 wakibainika kuchaguliwa wakiwa hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu.

  Mkuu wa shule ya Mgomba Mwl. Elis Banda alisema kuwa tatizo wanafunzi
 kukataa kukaa katika Hosteli linatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya
 watoto wanaosoma katika shule hizo kuwa ni wakazi wa maeneo husika na
 akapendekekeza kuwepo kwa utaratibu wa kutenga Shule za kanda kwa
 ajili ya kupeleka wanafunzi kutoka maeeneo tofauti huku akiitaka
 serikali kutoa maelekezo ya vitabu vya kununuliwa tofauti na sasa
 ambapo kumekuwa na maelekezo ya kuwataka wakuu wa shule kutumia vitabu
 kutoka katika kampuni ya EMACK  ambapo alishauri kupunguzwa kwa idadi
 ya vitabu vya kufundishia.

 Wadau hao waliendelea kubainisha vikwazo vingine kuwa ni paomja
 Na wanafunzi kubeba mimba wakiwa shuleni.
Mkuu wa Shule ya sekondari Lukumbule Mwl. Mathias Katto akabainisha
 vikwazo vingine kuwa shule zao kutokuwa na walimu wa masomo ya
 Sayansi,Shule kutokuwa na maktaba,Watoto kutoka katika maeneo husika
 na miundombinu ya Nyumba wanazo ishi nimbovu ,mila na destuli potofu
 za kuwafundisha watoto wadogo hasa wakike mafunzo ya kuishi kiunyumba
 ambayo hutolewa kupitia mafunzo ambayo hutolewa katika jando, Unyago
 na Msondo na ngoma ya Sakamimba hali ambayo imekuwa ikipelekea baadhi
 ya wanafunzi kuishi kwa wanaume huku wakiwa wanaendelea na masomo.