Ball control 100% Super, chezea mimi!??
Sunday, December 29, 2013
Hongera Majjid Mjengwa, Wadau sisi vipi?
Hongera
Majjid Mjengwa,
Wiki
hii inayomalizika mdau mwenzetu katika tasnia ya habari, mchambuzi mkongwe,
mwandishi kindakindaki, mfuatiliaji na mdadavuaji wa habari na matukio na
mengine mengi Majjid Mjengwa ameweka sokoni kitabu chake kinachomuelezea gwiji
wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na mpigania ukombozi wa Taifa la Afrika
ya Kusini, Hayati Mzee Nelson Rolihlahla Mandela.
Mjengwa
ameandika kitabu hiki wakati muafaka na amewatendea haki wanajamii hasa wale
ambao ama kwa sababu za umri, zama, ama kwa sababu ya kukosa fursa ama kwa
sababu nyingine hawakupata kujua kuhusu mwanasiasa huyo Mkongwe alivyojitolea
maisha yake kuipigania Afrika ya Kusini iliyokua imetumbukia katika janga la
ubaguzi wa rangi ulioendeshwa na makaburu.
Ni
sawa Mjengwa ameandika mengi yenye manufaa kwa jamii na ndivyo alivyo kwa
tunayefuatilia maisha yake ya uandishi.
Lakini
mimi nimeona katika Blog hii Nimpongeze Ndugu Mjengwa kwa sababu alichokifanya
ni wajibu wa kila mtu aliyehifadhi historia, taaluma na fursa ya kukiunganisha
kizazi cha sasa na yale yaliyojiri kabla
yake.
Katikati
ya mwaka 2013 nilihudhuria kongamonano moja lililomwalika Askofu Mstaafu
Norbert Mtega katika Jubilei ya kumpongeza Padre Christian Mhagama mmoja wa
waandishi wazuri wa vitabu, Askofu Mtega katika Siku hii alisema “Msomi
asiyeandika vitabu ni sawa na Mama mjamzito asiyezaa”
Kwa
maana hii Mjengwa na waandishi wengine wa vitabu wanatimiza wajibu wao, na wale
wasiofanya hivyo wakati wana taaluma ya kufanya hivyo hawatimizi wajibu wao.
Japo
kuwa sijapata nakala ya kitabu cha simulizi za Mzee Mandela cha Mjengwa, mimi
ni mmoja wa wasomaji wa Blog ya Mjengwa kila uchao na nimefuatilia maandalizi
yake kwa kuwa alikua akiweka kwenye Blog yake kila anapofanya tafsiri ya kile
kitabu cha Mzee Madiba cha safari ya Ukombozi yaani “Long work to Freedom” Kwa
kweli nikiri kuwa hata mimi sijakisoma kitabu hicho cha Madiba na hivyo
nilivutiwa mno na simulizi iliyokua ikitafsiriwa na Mjengwa kwenye Blog yake.
Kuna
mengi ya kuyasema lakini katika pongezi nimalizie kwa kusema Hongera sana
Mjengwa na hongera kwa kuona umuhimu wa kuchapisha kitabu ili iwe kumbukumbu
sahihi kwa kila anayetaka kusoma Simulizi za Mzee Mandela na endelea kufanya
hivyo kwa mambo mengine mengi yaliyo hazina kwenye kichwa chako kama ilivyo
kwaida yako.
Wadau
sisi vipi?
Nauliza
swali hili kwa sababu naamini kuwa wengi wanaweza kufanya kama alivyofanya
Majjid Mjengwa katika simulizi za Mzee Madiba. Hasa kwa sisi waandishi wa
habari na katika hili nawagusa zaidi waandishi wa habari wakongwe ambao mimi
naamini wana mambo mengi mazuri ya kukisimulia kizazi hiki cha leo hapa
Tanzania kuliko watu wengine.
Ndio,
wanahabari tunayo fursa hii kwa sababu tunaona mengi. Najiuliza hapa Tanzania
Mwalimu Nyerere amefanya mengi katika kupigania uhuru, kuijenga Tanganyika,
kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar na mengine mengi. Yapo yaliyokua kama
vitimbwi, yapo yaliyoonesha uthubutu wa hali ya juu, yapo yaliyoonesha
kujitolea hata kufa, yapo yaliyoonesha ujasiri ambao unaonekana leo kama vitu
visivyowezekana na mengine kibao.
Haya
yote yalifanyika mbele ya waandishi wa habari. Jamani tupeni utamu, tupeni
historia, achieni kalamu zenu zitembee, msiache uhondo huo uteketee, msisubiri
waje wazungu watafiti ndio waandike.
Akina
Mzee Abdul Ngalawa, Ahamed Kipozi, Jenerali Ulimwengu, Phili Karashani, Ernest
Mrutu, Agustino Mbunda, Ben Kiko, Hamza Kasongo, Mhidin Michuzi na wengine wengi tupeni uhondo.
Si
lazima kutafsiri vitabu lakini zipo simulizi kuhusu yale mliyoyaona wakati huo,
jinsi nchi ilivyoendeshwa, jinsi mabadiliko yalivyokuja na mengine mengi.
Sisemi
kwamba hamjafanya kabisa hapana, najua baadhi huandaa vipindi, huandika makala
na kufanya mahojiano lakini isiishie hapo, tuandikieni vitabu, vitangazeni ili
watanzania wavinunue na waijue nchi yao ilikotoka. Jenerali Ulimwengu
nakupongeza pia kwa kuwa umetekeleza hili.
Nasema
hivi kwa sababu naamini kuwa, baadhi ya matatizo yanayotukumba sasa Tanzania
yanaweza kutatuliwa kwa nguvu ndogo tu ya sisi wanahabari kutumia kalamu zetu
kuwapata taarifa watanzania, kuwakumbusha watanzania na kuwaonesha njia ya
kupita.
Leo
hii inashangaza kumuona mtanzania akitoa kipaumbele kwa mambo ambayo yanaibomoa
nchi, yanavuruga moyo wa kuijenga nchi kwa kujitolea, yanajenga chuki,
yanaruhusu wabaya kuivuruga nchi. Tulikotoka haikua hivyo, na nchi za wenzetu
kama vile China bado wanafanya yale ambayo sie tulikua tunayafanya kabla ya
miaka ya 90.
Najua
aya hiyo hapo juu itakua imewachefua baadhi ya watu, lakini niseme sababu hizo
zinazotumiwa na baadhi yetu kuhalalisha mambo yanayoigharimu nchi utatuzi wake
unapaswa kutenganishwa na jukumu la msingi la kujenga Taifa letu.
Kama
kuna wezi, mafisadi ama walafi tuwaache washughulikiwe na vyombo husika. Wasiohusika
tukazane kujenga nchi, haiwezekani sote tukawa walalamikaji, sote tunatafuta
wala rushwa na wezi na mwisho wa siku sote tukawa wanasiasa. Nchi atajenga nani?
Jamani
eheee wakongwe wa Habari andikeni vitabu watanzania wasome enzi za mwalimu
watanzania waliishi vipi?
Na
je wala rushwa hawakuwepo?
Mafisadi
hawakuwepo?
Viongozi
legelege hawakuwepo?
Siasa
hazikuwepo?
Waaminisheni
watanzania kuwa kila mtu anaweza kuwa mpigania nchi yake na akawa shujaa, kama
ambavyo Mjengwa amemuandika Mzee Madiba na simulizi nyingi nyingi alizowahi
kuandika.
Mwisho
nawapenda sana na niliyoandika sio msahafu.
Tuesday, December 24, 2013
Kwa muda nyumbani Ilembula
Brigedi Kamanda wangu, Mwite Chester katika pozi pande za
Njombe Town
Babu, wajukuu na Mkamwana. Kutoka Shoto Chester, Wayne, Mzee
Partinus Msigwa na My wife wangu nani hiii ahaaa nani huyuuuu, nani hii
ntawambia baadaye.
Mimi na Ka’Fulo
Wayne na Bibi Mlangadu
Mimi na Bibi Mlangadu na Cathy Mgunda
Bibi Agnes Mlangadu akiwa mwenye furaha
Mama Semahuvi
Mama yangu Mzazi Paskalina Mahuve a.k.a “Semahuvi” akikamilisha
mawasiliano ya mambo Fulani ya kula bata kwa wajukuu zake
Friday, December 20, 2013
Wednesday, December 18, 2013
Tukumbushane Wadau
Kwanza nawapongeza
wapiganaji wote tunaoendelea kufanya kazi ya uandishi wa habari ambayo kimsingi
ni kazi ya kiutumishi kwa umma.
Naomba tuendelee
kutumikia umma wa watanzania na tuendelee kuandika habari zenye maslai kwa
umma. Kwangu mimi utumishi wetu utakua na maana na manufaa kwa watanzania kama
tutaandika, kutangaza, kuonesha na kuchapisha habari, taarifa na matangazo
yenye kuitetea Tanzania na watu wake.
Kwenye kazi ya
kuitetea Tanzania na watu wake tusisahau kwamba zipo taarifa nyingine ama
habari nyingine licha ya ukweli wake na ubora wake zina madhara kwa Tanzania na
watu wake, kwa aidha kuichafua nchi usoni kwa mataifa mengine ama zinawaathiri
watanzania.
Naamini tunayajua haya
na wengi tunayatekeleza, hebu tuendelee kufanya hivyo na wale wasiofanya oneni
umuhimu wa kufanya hivyo ili Tanzania iwe mahali salama pa kuishi na watanzania
wafurahie maisha yao licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi ikiwemo umasikini.
Tukiwa tunakumbushana
hili hebu pia tukumbushane umuhimu wa kuzingatia weledi, maadili, haiba na
staha ya mwandishi wa habari. Tusione haya kujifunza, tusione makosa kukosoana
na isiwe hatari kukubali pale unaposhindwa.
Nasema hivyo kwa
sababu wapo baadhi yetu ambao kimsingi hata wao wanajua kwamba kazi hii
haiendani nao lakini wanalazimisha, matharani kuwa watangazaji bila kujali
ubora wa sauti, rafudhi na uwezo wao kiutangaza, wapo wanaofanya uchambuzi
magazetini kwenye redio na Televisheni bila kujali kama uchambuzi wao hauna
utafiti wa kutosha wala mpangilio, wapo wanaokwenda kukusanya habari bila
kujali muonekana wao mbele ya jamii na tabia zao kama zinafanana na kioo cha
jamii na wapo wanaochapisha magazeti na vijarida bila kujali yale
wanayochapisha kama yana tija ama la.
Nasema bahati nzuri,
haya ninayosema sie wenyewe wahusika tunayajua, nashauri tupime wenyewe na
kuchukua hatua kabla ya kuhukumiwa na jamii ama kusubiri tupigiwe kelele.
Na sasa tunakwenda
kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na baadaye Uchaguzi Mkuu na tayari
hekaheka zimeanza leo, nashauri tutumie kalamu zetu kukataza hekaheka hizi kwa
sababu zina madhara kwa taifa, muda wake bado japo wapo watakaonikosoa. Tunaliacha
taifa liwe linatumia muda mrefu kujadili uchaguzi badala ya maendeleo,
tunaliacha taifa ligubikwe na ajenda ya siasa badala ya kupambana na umasikini
unaowatafuna watanzania wengi, tunaacha watu wachache wanaotetea maslai yao
kuliyumbisha taifa na mwishowe tunawaacha watanzania washindwe kutengeneza
ajenda za nchi yao. Ndio, ni sisi waandishi wa habari tunaopaswa kuwajibika kwa
hili anayekataa atupishe.
Napiga la Mgambo
nikiomba waandishi wenzangu tuwe chanzo cha matumaini kwa watanzania, tusiache
nchi ikitupiwa mawe ndani na nje, tusiache matatizo ya watanzania yakawa donda
ndugu, na tuwaongoze watanzania kukataa jambo lolote linaloigharimu nchi na
watu wake kwa njia ya amani.
Mwisho nawapenda sana
na Aluta Continua………..
Taswira mbalimbali za Dar, Nairobi na Kampala
Bandari Salama (Dar es salaam) kutoka angani
Unapoachana na jiji la Dar Ukiwa angani
Angani unapokatiza Mlima Kilimanjaro
Angani ukikaribia kutua Uwanja wa Ndega Nairobi (Jomo Kenyatta Airport)
Uwanja wa Ndege Entebe, Kampala Uganda
Kuelekea Mjini Kampala
Unaingi Jijini Kampala
ASANTE WADAU KWA SALA ZENU NIMEKWENDA NIMERUDI SALAMA
Thursday, December 5, 2013
Wapiga boksi tulipomaliza kazi maalumu
Pande za Tukuyu wapiga boksi wakitalii ndani baada ya kazi maalumu. toka Shoto Silvanus Kigomba, Mimi, Jongo, Mwishee na Mary
Nipo na Mzee Mpakatwe (Mngoni Orijino) Kaji Moja leo, ahahahahaaaaa
Tuesday, December 3, 2013
Nimepita Makongolosi Chunya na Nimekutana na Baba Mzazi eeee babaaaa!!!
Nimefurahi sana kukutana na mtu muhimu kwa tasnia ya wanahabari hususani kwa Redio na Luninga. Huyu jamaa anaitwa Lawena Nsonda Maarufu kwa jina la Baba Mzazi, Mzee wa Makongolosi, kama humjui fuatilia vipindi vya mijadala kwa njia ya simu katika Redio na Luninga zote za Bongo. Ametukaribisha vizuri mimi na Mpiganaji mwenzangu Said Makala wa Channel Ten, nyumbani kwake Makongolosi Chunya.
Shoto mimi na kulia Baba Mzazi babaa eeeeee!!!!
Pamoja kuanzia shoto mimim Baba Mzaziii na Said Makala
Makongolosi kuna embe nzuri, tamu lakini cha kusikitisha huishia kuoza kipindi kama hiki, wenye dhamana ya viwanda na biashara mnajua hiliiiiii!!!
Mti wa mwembe ukiwa umenona matunda pande za Makongolosi Chunya
Tamu eheeeee!!!!
Na wadau tulipokutana Nyasaland
Kwanza Shoto John Bukuku wa Full Shangwe, Said Makala wa Channel Ten na Mimi.
Kuanzia Shoto Said Makala, Said Mwishee, Mary, Nasoro Hassan, Mimi, Sheila Simba, Dadi Mnamba, John Bukuku, Suleiman Jongo, Geofrey Lunyungu
Subscribe to:
Posts (Atom)