Tuesday, May 6, 2014

Wadau tuongeze juhudi kuinadi Tanzania



Ujumbe
Kwa takribani siku tatu nimekua safarini kikazi Pemba na Unguja na kisha Dar es salaam. 
Nadhani wadau bado tuna kazi ya kufanya kuzinadi fursa zilizopo katika maeneo yetu kimkakati. Kwa mfano fukwe zetu bado zinatumia kwa Uchuuzi wa Samaki, Kampuni ya Azam Marine sasa imetatua moja ya kero kubwa zilizokua zikikabili mawasiliano kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar nina maana kero ya Usafiri lakini bado hakuna joto la ushirikiano wa kimanufaa linaloonekana kwa kiasi cha kutosha kwa kutumia fursa hii mfano Ukuzaji Utalii wa Ndani na nje kati ya maeneo haya mawili, Hotel na mengine.

Nimejifunza kuwa Zanzibar bado inahitaji kutangazwa zaidi ya ilivyo sasa, Utamaduni wake, rasilimali zake hasa mazao ya marashi, Utamaduni wake nakadharika. Nimejifunza kuwa wawekezaji katika sekta ya Hotel Zanzibar wanapaswa kufanya zaidi ya ilivyo sasa ili pawe mahali pakukimbiliwa na hata watu wakipato cha Chini badala ya kuwategemea wageni pekee.

Nimejifunza kuwa sisi waandishi wa habari kwa kutumia rungu letu la Utangazaji na uchapishaji tuna kazi kubwa ya kuamsha, kujenga na kuimarisha Utalii wa ndani. tuwajenge watanzania kuwa Mtalii si lazima awe mgeni kutoka nje ya nchi. tunaweza kufanya hili.

Na kwa kuwa wakati huu Tanzania imefunikwa na joto la kuandika Katiba Mpya huku ajenda ya Muungano wa namna gani ikiwa imefunika kazi nzima ya Kuandika Katiba tuna kazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania juu ya safari hii ili imalizike kwa usalama. Safari hii iepuka mambo yatakayovuruga maziwa na asali waliyonayo watanzania wa bara na visiwani hata kama wengi wanaona haijawanufaisha wananchi. tuwawezeshe watanzania kupima hoja zinzotolewa ni kwa namna gani fursa hizi zitaathirika ama kupiga hatua.

Muhimu zaidi tufanye kazi hii tukiwa na mawazo huru na kutanguliza maslai ya Taifa Mbele. Najua hapa kuna chngamoto kubwa lakini Mungu aongoze

Gerson