Monday, August 12, 2013

Majimaji Sports Club sasa kuwa Kampuni

Wadau walioshiriki Mkutano ulipokea taarifa ya Majimaji Sports Clu kuwa Kampuni

Na; Msigwablog 
Hatimaye wadau wa timu ya Majimaji ya Songea almaarufu Wanalizombe wameamua kuwa timu hiyo iwe kampuni na itakayokua ikiuza hisa zake katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

Haijafahamika hisa moja itauzwa shilingi ngapi na kutakua na hisa ngapi lakini kulingana na maelezo ya wadau walioandaa mkutano huu yaani Kampuni ya Tanzania Mwandi hatua hiyo inalenga kukabiliana na changamoto kuu ya timu hiyo ambayo ni ukata.

Silas Mwakibinga ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF anasema sasa wawekezaji mbalimbali wanaweza kununua hisa, kama  inavyofanyika kwa timu za ligi kuu nchini Ulaya hali ambayo itaiwezesha timu hiyo kujiimarisha kiuchumi ikiwemo kuwa na uwanja wake, kusajili wachezaji wazuri na kuwaandaa vizuri kwa mashindano na pia itakua na uwezo wa kufanya biashara.

Mwakibinga anasema tayari baadhi ya wawekezaji wameshaonesha nia ya kununua hisa nyingi na kuwekeza katika timu ya Majimaji wakiamini kuwa mfumo huo unalipa na Majimaji itakua katika nafasi nzuri ya kuwa timu bora zaidi katika timu za soka za Tanzania Bara.

Akiwasilisha Mada kwa niaba ya Mwanasheria Dr Damas Ndumbaro, mwanasheria Abel Ngilangwa anasema kwa kuwa Kampuni sasa Majimaji Sports Club itakua imeachana na mfumo wa kuwa mali ya wanachama na sasa itakua ni mali ya wanahisa na kwamba mwenye hisa nyingi zaidi ndiye atakayekua na sauti zaidi kwenye Kampuni.

Mdau mwingine wa Soka ambaye pia ni mwanasheria Sebastian Walyuba amewashauri wapenzi wa timu ya Majimaji na wanaruvuma kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kununua hisa kwa kuwa hiyo ndio njia pekee itakayowawezesha kushiriki katika timu hiyo vingine watatupwa nje.

Mapema akifungua Mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alisema mfumo huo ni mzuri na akatoa changamoto kwa uongozi wa Kampuni ya Majimaji kuhakikisha timu inashinda katika mechi zake na kwamba kwa kufanya hivyo ndio njia pekee itakayowavutia wawekezaji wengi kuweka pesa zao katika Kampuni hiyo
.........................

Chezea mimi weyeee!!!!!!!

Nakikanyaga

Friday, August 9, 2013

Big Respect!!!!!!

Shoto Mama Mzazi wa Mimi, Kati ni Mimi na kulia Shangazi wa Mimi. Hapa tulikua tunaandaa kinywaji.

Hii kitu imewalipia watu ada hiii, ohooo!!!!!!!

Billionare Oprah Winfrey aonja joto ya ubaguzi wa rangi Uswisi

Oprah Winfrey 

Habari kutoka nchini Uswisi zinasema tajiri mwanamke dunia Oprah Winfrey Raia wa Marekani mwenye asili ya Africa ameonja joto ya jiwe alipoingi katika duka moja nchini Uswisi, pale muuza duka alipokataa kumpa mkoba wa kike (Kipima joto) wenye thamani ya Pauni 24,477 sawa na shilingi milioni 61 kwa madai kuwa hana uwezo wa kumudu gharama za kuununua mkoba huo.

Oprah amekitafsiri kitendo hicho kuwa ni ubaguzi wa rangi, akiamini kuwa muuza duka huyo alimuona kuwa kwake mtu mweusi hawezi kuwa na uwezo wa kununua mkoba huo.

Oprah Winfrey anayetajwa kuwa moja ya matajiri wakubwa wanawake dunia mwenye asili ya Africa anadai alikwenda dukani hapo akiwa simple, na hakukua na viashiria vya mtu maarufu ambaye kwa kawaida hutembea na watu wengi kwa ajili usalama na huduma nyingine anasema alipoingia dukani hapo alipendezwa na mkoba huo uliokua umewekwa ukutani na ndipo alipotaka kuuona ili afanye uamuzi  wakuununua ama la.

Alikwenda nchini Uswisi kuhudhuria harusi ya Tina Turner.

Anasema aliomba mara ya kwanza, muuzaji akamwambia mkoba huo ni ghrama mno hawezi kuimudu bei yake, akauliza mara ya pili bado akapewa jibu hilo hilo na akauliza mara ya tatu bado akapewa jibu hilo hilo hadi alipoamua kuondoka dukani hapo.

mmliki wa duka hilo Trudie Goetz ameomba radhi kwa lililotokea.

Hata hivyo Oprah amekiri kuwa pengine alijibiwa hivyo kwa kuwa muuzaji hamfahamu na kwa sababu Vipindi vyake "Oprah shows" si maarufu nchini Uswisi.

Tayari Oprah Winfrey ametunukiwa tuzo ya ya Rais ya heshima ya juu ya Uraia nchini Marekani ambayo atakabidhiwa na Rais Barack Obama katika Ikulu ya Marekani (White House) Baadaye Mwaka huu.

Haya wadau habari ndio hiyo, Dada ana mihela ya kumwaga hadi anashangazwa na muuza duka anayeona so kumuuzia mwafrika mkoba wa milioni 61.

Thursday, August 8, 2013

Wadau Hii Vipi?

wakati nachanja mbuga mahali nimekutana na Mjadala "Watoto wanaposhiriki kazi kama hii ya kubeba matofari na kupanga matanuru, ni kujifunza kazi ama Ajira mbaya kwa watoto?"

Nilipokutana na Mh Moses Machali Singapore

Shoto Moses Machali (Mb) na Mimi

Nilipokutana na Mheshimiwa Moses Machali nilijifunza kuwa daima binadamu tnapaswa kuwajibika kwa kila wajibu tulionao na ukiwa kiongozi ni muhimu ujifunze kutoka ndani ya Jamii.

Big Up!!!! Mh. Moses Machali.

Wednesday, August 7, 2013

Hongera sana Kaka Julius Mlawa "Mtazamo"

Julius Mlawa - Mtazamo

  • Huyu Jamaa ni mfanyabiashara wa mazao na msindikaji wa unga wa sembe
  • Pia ni msafirishaji wa mizigo
  • Anamiliki Kampuni ya Mtazamo Enterprises
  • anafanya shughuli zake katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Leo nimejisikia kumwambia Hongera sana kwa sababu zifuatazo;
  1. Jinsi anavyoishi kwa ushirikiano na upendo na watu mbalimbali.
  2. Jinsi anavyoendesha shughuli zake na wafanyakazi wake kibinadamu
  3. Jinsi anavyoipenda nchi yake Tanzania
  4. Jinsi anavyopenda maendeleo ya kila mtu
  5. Jinsi anavyowajali watu wanaopigania maisha
  6. Kakaa mbali na ukatili na unyama
  7. Na mengine mengi mazuri mnoooooo
Naamini huu ni mfano wa kuigwa, so lets be smart as he do.