Thursday, March 6, 2014

Siku nzuri niliyokutana na watu muhimu

 Nilipiga boksi na Kaka Zakaria Ngalimanayo, yeye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Klabu ya Wanalizombe Majimaji ya Songea ambayo ipo mawindoni kusaka kurejea Ligi kuu
 
Hapa nilikutana na Sheikh Jamal (Baba Mayasa) pili kulia, anayefuata ni Abdalah dege mmoja wa WanaCCM waliopata kuongoza Chama kwa heshima kubwa na baadaye akastaafu kistaarabu. Na kwanza Shoto ni Mpiganaji ninayemheshimu sana Juma Nyumayo Mwanataaluma mwenzangu.
 


Sunday, March 2, 2014

hufarijika kuwaona wapiganaji wakongwe



Mwandishi wa Habari Mkongwe hapa Nchini Mzee Mbunda wa kwanza kushoto, anafuatiwa na Andrew Kuchonjoma- Mwenyekiti Ruvuma Press Club, Andrew Chatwanga - Katibu Ruvuma Press Club, Nathan Mtega na Zakaria Nachoa - Mkurugenzi Manipsaa Songea
 
 Mpenda Mvula, Mmoja wa wapiganaji wakongwe katika mambo ya Uandishi wa Habari yeye akijikita katika upiga picha, waandishi wa habari wengi wakongwe hapa nchini wanamtambua huyu jamaa na mpaka leo angalia anatupiga jeki wadogo zake. Hongera sana Brother na Baba yetu katika fani, Big Respect



Samahani Wadau kwa kutoaga, sasa Nimerudi


Sunday, February 2, 2014

Mimi na Chama Cha Nani hii tumetimiza umri wa miaka 37.


 Naibu Katibu Mkuu wa CCM na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akishangilia pamoja na wana CCM wa Manispaa ya Songea kwa Chama hicho kutimiza miaka 37 tangu kizaliwe mwaka 1977 (tulipozaliwa pamoja na mimi). Mkutano huu ulifanyika katika uwanja wa Kibulang'oma kata ya Lizaboni, Songea Mjini katika Mkoa wa Ruvuma

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akipongezana na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dr Emmanuel Nchimbi kwa Chama hicho kutimiza miaka 37 tangu kizaliwe mwaka 1977 (tulipozaliwa pamoja na mimi)

 Wana CCM wakishangilia kwa nguvu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM ambacho sasa kimetimiza miaka 37 tangu kililetwa duniani mwaka 1977

 Mzee Mustafa Songambele mmoja wa waasisi wa Chama Cha Mapinduzi CCM na mwanachama namba 15 wa Chama cha TANU akiwahusia wana CCM na wananchi wengine wa Songea

 Tunakushukuru Mzee Songambele kwa kutuanzishia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisikika akisema Mwigulu Nchemba. Anayewatazama nyuma ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho.

Dr Emmanuel Nchimbi, Kiongozi wa "Maneno kidogo, Kazi zaidi" akimwaga maelezo juu ya miradi lukuki ya maendeleo aliyowafanyia wananchi wa jimbo lake katika sekta ya Afya, Barabara, Usafi wa Mazingira, Michezo na Elimu. Jamaa alishangiliwa kuwa Jembe tena Jembe la Mpunga

 Mwigulu Nchemba akiwaaga wananchi wa Songea baada ya kuhunguruma katika Jukwaa la Miaka 37 ya tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM, Mkutano uliohunguruma katika viwanja vya Kibulang'oma, Lizaboni Mjini Songea. Jamaa ajenda yake kuu ni Uzalendo na Utaifa kwa kila jambo na ndio maana muda wote ni skafu ya Bendera ya Taifa, I like this, Big respect Brother.


Friday, January 24, 2014

Hii imenikumbusha mbali sanaaaaaa

 Kijijini Ilembula, wilaya ya Wanging'ombe bado akina dogo wanalelewa kama ilivyokua mimi..


 Baada ya kumaliza kazi shambani safari ya nyumbani kuwahi ugali

Baba na mwana wakitoka kwenye majukumu.

Tuesday, January 21, 2014

Hongeraaaaa Mpiganaji Juma Nkamia


Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Selemani Nkamia akipokewa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Clement Mshana, katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Olegabriel

Hongera saaaaana Juma Nkamia.

Najua kwa pongezi hizi wapo ninaowaudhi lakini naomba wadau tujenge utamaduni wa kukubali mafanikio ya binadamu. 

Nampongeza Juma Seleman Nkamia, mwanahabari wa siku nyingi na mbaye pengine amekua kichocheo cha wana habari wengi wanaofanya vizuri hii leo kutokana na umahiri wake wa utangazaji.

Juma umetutoa kimasomaso, umetupa heshima unatuwakilisha. Sina mengi zaidi na sitaki kuzua mjadala naomba niikamilishe furaha yangu kwa kusema Cheza karata yako vizuri utusafishie njia sote tuliofurahi na wasiofurahi. Ukweli ni kwamba wewe ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Kwani kitu gani eheee, Kaji moja bana. Ahahahahaaaaa!!!!!

Wadau tumetimiza wajibu wetu katika hili?


 Soko la wauzaji vyakula la Namtumbo

 Soko la Namtumbo kwa ndani 

 Vitunguu bwelele

 Nyanya, Tangawizi bwelele

 Maharage na njugu bwelele

 Karanga a.k.a Mtesa

 Viazi

Jambo,

Ni matumaini yangu kuwa wapiganaji wenzangu tunaendelea na jukumu letu la kuwatumikia watanzania.
Tuendelee kufanya hivyo licha ya changamoto tunazokutana nazo.

Ndugu zangu nimepita katika Soko la mazao na bidhaa ndogondogo la Namtumbo Mjini Mkoani Ruvuma na nikiwa hapo kengele ikagonga

Imegonga baada ya kushuhudia vilio vya wauzaji wa Matunda, mbogamboga na vyakula vingine wakilia ugumu wa biashara. wanadai  soko huporomoka sana kipindi hiki cha Mvua kwa kuwa wanunuzi wengi huhamia mashambani wakishughulika na kilimo. Bidhaa nilizoziona sokoni ni pamoja na Nyanya, Vitunguu, viazi, mbogamboga na matunda. Staili inayotumia kuuza bidhaa hizi ni ile ile ya hata kabla Tanzania haijapata uhuru, bidhaa zote zingali zinauzwa zikiwa na thamani ya shambani, hazijaongezwa thamani

Kwa hilo nikakumbuka wajibu wetu waandishi wa habari, kwamba katika safari ya kuongeza thamani bidhaa za wakulima wadau mbalimbali wanapaswa kuhusika, kwanza wadau wa maendeleo matharani taasisi za mitaji, wataalamu wa mashine za kusindikia mazao, wataalamu wa kilimo na usindikaji na wengineo ikiwemo serikali. Sio lengo langu kuwajadili hao

Kengele yangu iligonga kwa swali moja kwamba je sisi waandishi wa habari tumetimiza wajibu wetu wa kuwasaidia wakulima wa Tanzania kuanza na kuchochea safari ya kuongeza thamani ya mazao yao? tumewaonesha fursa zilizopo? tumewaonesha pa kuanzia? Kama tumefanya inatosha? Na kama inatosha tumepima utekelezaji wake na matokeo yake? Na je tunawakumbusha wadau wengine juu ya wajibu huu? kama tumefanya inatosha? Na pia je tumepambana kidete kama tunavyopambana katika masuala ya wanasiasa?

Sio lengo langu kutaka tujilaumu bali kukumbushana kuwa huu ni wajibu mwingine tunaoweza kuwasaidia wakulima. Nafahamu yapo maeneo mengi ya nchi hii yenye shida hii. Naomba tulione hili na tuamue kulivalia njuga. tusipofanya hivi watanzania hasa walala hoi wanaendelea kuumia. Tupige kelele watanzania wale Nyanya za Tanzania popote walipo badala ya baadhi ya watanzania ama watu wanaokuja nchini kwetu kununua nyanya kutoka nje ya nchi. Na sio kwa nyanya tu hata bidha nyingine. Huu ni wakati wa Mvua embe kiasi gani za wakulima zimeoza vijijini kwa kukosa kusindikwa? mbogamboga kiasi gani zinatupwa ama kuachwa ziharibika mashambani?

Tuamue tunaweza kwani sisi ni mhimili wa nne wa Dola japo sio rasmi

Natoa hoja