Thursday, March 6, 2014

Wadau wajibu wetu uko wapi kwenye hili?

Jamaa jina kampuni akihaha kupiga simu muhimu wakati Mtandao ukiwa unasumbua.
 
 
Hili Tena;
 
Habri wapiganaji wenzangu;
Awali ya yote kwanza poleni kwa kazi na Hongera kwa kulijenga Taifa kwa gharama kubwa.
 
Leo nimeona tukumbushane jambo moja ambalo kwa maoni yangu naona hatuwatendei haki watanzania. Nasema hivi kwa sababu vyombo vya habari ama niseme waandishi wa habari ndio muhimili wa nne wa dola. Kwa lugha nyingine hapa ndio mahali pengine muhimu na pa kipekee ambapo wananchi wanapaswa wapate matumaini na kupaza sauti zao na kukataa kuonewa pale mihimili yote mitatu inayotambuliwa kuwa rasmi inaposhindwa kutimiza matakwa ya wananchi wake.
 
Kuanzia Mwaka jana watanzania wanapata matatizo makubwa ya usumbufu wa kimawasiliano ya simu. Sio kwamba mawasiliano hakuna la hasha, yapo saaana tena hadi vijijini ambako hakukudhaniwa kama ipo siku watu wake watawasiliana na dunia kwa urahisi.
 
Tatizo lililoibuka ni upatikanaji mgumu, ubora wa chini na wakati mwingine kukosekana kabisa kwa mawasiliano ya simu za Mkononi. wapo wanaosema pengine ni kwa sababu makampuni haya sasa yamejikita kwenye huduma za kifedha ndio maana kwenye upigaji wa simu hakutiliwi maanani ya ubora wake.
 
Hebu tufikiria mtu aliyeyapanga maisha yake kwa kutegemea simu ni moja ya nyenzo za kuwezesha mipango yake mawasilaiano yanapokosekana madhara yake nini? aliye na Mgonjwa akashindwa kuita gari kwa ajili ya kumpelaka mgonjwa wake kwa dharula hospitali inakuwaje? vivyo hivyo kwa wakulima, wafanyabiashara, wafanyakazi ma wengineo?
 
Hii leo ukitaka kupiga simu, huna hakika unayempigia kama utampata, na kama ukimpata huna hakika kama ubora wa mawasiliano utakua mzuri. Kila mahali watu wanapopiga simu wanalazimika kupayuka sauti ili kusikika, mara ukipiga simu unayempigia hapatikani hata kama mpo pamoja hapohapo (kama unajaribu), mara ukipiga simu unakutana na kelele za kuudhi.
 
Hii leo watanzania wanapotezewa muda, unapiga simu ili uongee na mtu fulani kwa haraka badala yake unapigiwa matangazo ya biashara kwanza kwa muda mrefu ndipo unajibiwa hapatikani ama unaunganishwa na muhusika.
 
Hii leo, watanzania wangapi wanaingiza vocha kwenye simu zinapotea, na ukifuatilia kwenye madawati ya wateja ya kampuni za simu hakuna msaada.
 
Hii leo makampuni ya simu yote madawati yake ya huduma kwa wateja ukipiga simu ya bure basi unapaswa utenge nusu saa kwa ajili ya kuuliza huduma Fulani ambayo kimsingi ni haki ya mteja na ya bure, tena makampuni mengine yameamua kuwabagua watanzania kuna huduma ya bure ya kusubiri hata saa nzima na kuna huduma ya kulipia.
 
Hii leo Serikali imetangaza kupungua kwa gharama za upigaji wa simu, nani kapunguza gharama hizo? badala yake watanzania wameanzishiwa utamaduni mpya wa kushiriki bahati nasibu ya kampuni za simu, mara tuma ujumbe ushinde milioni 50, nyumba nakadharika. Uhalali wa bahati nasibu hizi anaufuatilia nani, watanzania wanajua kinachofanyika kinaga ubaga?
 
Hii leo mawasiliano ya simu ya Kampuni Fulani yanaweza kukosekana hata siku nzima na watanzania hawaombwi radhi na hakuna fidia. 
 
Hii leo makampuni ya simu yanakusanya marundo ya faida na zote zinaishia kufanya matumizi ambayo hayana uangalizi kama huo uwajibikaji wa kijamii (Social Responsibility) una manufaa kwa watanzania? Hivi Kampuni ya simu kumleta msanii mkubwawa kimarekani na kumlipa mamilioni ya fedha ndio kipaumbele cha watanzania?
 
Yapo mengi yanayoudhi.
 
Mimi sina tatizo na maudhi ya makampuni haya ya simu kwa sababu najua kuwa makampuni haya yanatafuta faida.
 
Hoja yangu ni kwamba wanaofanywa vichwa vya wendawazimu ni watanzania. Kama ndivyo sie vyombo vya habari tumeshiriki vipi kulinyoosha hili?
 
Inawezekana nina majibu kuwa vyombo vyetu vya habari kwa sababu vinanufaika na matangazo ya biashara kutoka makampuni haya ndio maana haviwezi kuyakosea.
 
Sasa ninachojiuliza kwenye hili vipi wadau, tumeshindwa? tumetekwa na maadui? Bloggers msio na matangazo ya kampuni za simu, magazeti yasiyo na matangazo ya makampuni ya simu, Radio na Televisheni hapo vipi?
 
Watanzania wanaumia jamani, vibaya hivyo twende tuseme, hawa jamaa katika maeneo ambayo wapo makini nayo ni kulalamikiwa, wananchi wanalalamika lakini pa kulalamikia wanakosa kwa sababu sisi hatujawawezesha kulalamika. Vyombo vyetu vya habari ndio hivyo vinaogopa kunyea kambi.
 
Je tukae tu kimyaaaaa
 
Ahaaaaaa Jamani sio vizuri, tunakiuka weledi wetu, mbona  taasisi nyingine zikikosea tunaripoti lets do this please.
 
Kwa heriiiiiii