Sunday, March 31, 2013
RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJERUHI WALIOUMIA KATIKA GHOROFA LILILOPOROMOKA DAR ES SALAAM
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke
wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakimpa pole
kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni mwa majeruhi
walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa
iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.PICHA NA IKULU.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke
wake Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bw. Yusuf Abdallah ambaye ni mmoja
wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji
Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25, katika wodi ya Sewa
Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
jijini Dar es salaam. kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa Ghasia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke
wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya
Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani
Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka
katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25
Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond
Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke
wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya
Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole kijana Baqir
Dhamji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka
katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25. Kulia
ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya MOI.
Saturday, March 30, 2013
UP DATE: KATIKA BONANZA LA PASAKA LINALOENDELAA KATIKA UWANJA WA MAJIMAJI TIMU YA MANDELA YAICHAPA TTC MATOGOLO 2 - 0
Katika Bonanza la Pasaka linaloendelea katika viwanja vya majimaji kwa kushilikisha timu mbili toka Mbeya, ambalo linafanyika ndani ya uwanja wa majimaji leo hii timu ya Mandela baada ya kuchapwa mchezo wa kwanza na timu ya Mbeya Veteran Club bao moja kavu nayo katika mchezo wake wa kwanza. Awamu hii yaichapa timu ya TTC Matogolo mabao mawili kavu bila uluma .
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa Apokea hilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora kutoka kwa Mwakilishi wa JICA nchini Yasunori Onishi
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na Mwakilishi wa
JICA nchini Yasunori Onishi (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa
Japan kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji
safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.
Rais Jakaya Kikwete Aelezea Kuhuzunishwa Kwake na Maafa ya Kuporomoka na kusababisha vifo vya watu na majeruhi Kwa Jengo la Ghorofa ya 16 Jijini Dar es Salaam,Atoa Maelekezo Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mheshimiwa Saidi Mecky Sadik pamoja na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova
Rais Jakaya Kikwete
---
Na Ikulu-Dar es Salaam
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana
wa jana, Ijumaa, Machi 29, 2013, ametembelea jengo lililoporomoka na
kusababisha vifo vya watu na majeruhi kwenye Mtaaa wa Indira
Gandhi/Morogoro mjini Dar es Salaam na amesikitishwa na kuhuzunishwa na
maafa yaliyotokana na kuporomoka kwa jengo hilo.
BONANZA LA PASAKA NDANI YA MAJIMAJI - SONGEA
Hii ni picha ya Pamoja ya Timu ya Tukuyu mbeya na timu ya Kambarage, wenye jezio nyekundu ni timu ya Kambarage na wenye njano ni Tukuyu ya mbeya katika mchezo huo timu ya kambarage imeichapa tukuyumbeya moja kavu.Tutaendelea kukupa matokeo ambapo sasa timu ya Mandelea imeingia uwanjani kwa mala ingine na timu ya TTC Matogolo
Friday, March 29, 2013
WAZEE WA YANGA WAKIPIGA DUA NDANI YA UWANJA WA JAMHURI.
WAKATI
yanga wakikabiliwa na kibarua kigumu kesho kwa kupambana wenyeji wao
Polisi Moro ambayo imeonekana kuzinduka kwenye mzunguko wa pili wa ligi
kuu,wazee wa yanga wamenaswa jioni hii wakipiga duandani ya uwanja wa
Jamhuri wakati vijana wao wakiendelea na mazoezi.
Walipohojiwa
na Mtandao huu wazee hao walidai kwamba wanamuomba mungu awafanyiwe
wepesi kwenye mchezo kesho walidai kwamba ni mgumu.
Ugumu wa mchezo huo unatokana
timu zote mbili kuwa kwenye mazingila tofauti ambapo yanga wanaoongoza
ligi hiyo wanapigania kutwaa ubingwa huku polisi inayoshika nafasi ya
tatu kutoka chini ikibabana kujinasua katika janga la kushuka
daraja,nani ataibuka kidede tusubiri kesho
MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AFIKA KUJIONEA JENGO LA GHOROFA 16 LILILOPOROMOKA JIJINI DAR LEO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi
katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli
za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu
waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni
17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
RAMBI RAMBI KUTOKA UJERUMANI KUFUATIA KUANGUKA KWA JENGO DAR!
Umoja wa Watanzania Ujerumani
umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuanguka kwa jengo mjini Dar
es Salaam.tunawapa pole nyingi ndugu na jamaa wa waliopoteza maisha,
Umoja Wa Watanzania Ujerumani unaungana na watanzania wote pamoja wafiwa
katika maombolezi ya msiba huu mkubwa.
Tunawaombea marehemu wote mungu awaweke mahala pema peponi AMIN
BREAKING NYUZZZZZ.......: MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI EVALIST MUSHI AKAMATWA ZANZIBAR
MTU ANAESADIKIWA KUWA NDIE MUUAJI
WA PADRI EVALIST MUSHI WA KANISA KATOLIKI,VISIWANI ZANZIBAR,AMEKAMATWA
ALASILI HII MAENEO YA KARIAKOO,ZANZIBAR.
JESHI LA POLISI LIMETHIBITISHA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA HUYO,NA KWENYE NAE KITUONI KWA AJILI YA MAHOJIANO ZAIDI.
PADRI MUSHI ALIUWAWA KWA KUPIGWA
RISASI MWEZI ULIOPITWA WAKATI AKIWA KWENYE GARI LAKE KUELEKEA KANISANI
KWENYE IBADA YA JUMAPILI.
GLOBU YA JAMII ITALETA TAARIFA KAMILI YA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA HUYO HAPO BAADAE KIDOGO.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lapitisha kuanzishwa kwa kikosi cha uingiliaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa jana lilikubali kutumwa kwa kikosi cha uingiliaji ili kuchukua hatua za
kijeshi dhidi ya makundi ya waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Nchi 15 wajumbe wa baraza hilo lilipitisha
azimio la kuanzishwa kwa kikosi hicho chini ya utaratibu wa tume ya Umoja wa
Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO.
YANGA KUZINDUA TAWI JIPYA MAREKANI
TUNAPENDA KUWATANGAZIA RASMI MASHABIKI, WADAU NA WAPENZI WOTE WA TIMU YETU YA SOCCER YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB MLIOPO MAREKANI KUWA TUNAZINDUA RASMI TAWI LETU HAPA MAREKANI LITAKALO JULIKANA KAMA YOUNG AFRICANS FAMILY USA. TUNAOMBA UKIPATA TANGAZO HILI MWARIFU NA MWENZIO.
TAREHE: JUMAMOSI 03/30/2013
MAHALI: KILIMANJARO PASSION RESTAURANT
ADDRESS: 2310 PRICE AVENUE, WHEATON,MD 20902
MUDA: 4:00 PM
KWA MAWASILIANO:
ALEX KASSUWI : TEL :301 305 9685
YOUNG AFRICANS "DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"
KESHO KIBARUA KIKALI CHA NDUGU WAWILI DIMBA LA KAITABA!
By Baraka Mpenja
Ni vita ya kufa
na kupona kati ya watengeneza sukari nchini Tanzania klabu ya Mtibwa
Sugar dhidi ya Kagera Sugar watakaokuwa na kazi ngumu ya kuwania pointi
tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Pambano hilo la watengeneza sukari
sukari limevuta hisia za mashabiki lukuki wa soka kwa mikoa ya kanda ya
ziwa Victoria huku likitarajiwa sehemu ya kufurahia katika mapumziko
ya pasaka.
RAIS KIKWETE, ATEMBELEA ENEO LILIPOTOKEA AJALI YA KUANGUKA GHOROFA JIJINI DAR
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Taswira Maalum Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Aongoza Mamia Kuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis Jijini Dar es Salaam Leo
Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowassa na Mbunge wa Mafia Mhe Abdulkarim Shah alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
Subscribe to:
Posts (Atom)