Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke
wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakimpa pole
kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni mwa majeruhi
walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa
iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.PICHA NA IKULU.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke
wake Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bw. Yusuf Abdallah ambaye ni mmoja
wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji
Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25, katika wodi ya Sewa
Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
jijini Dar es salaam. kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa Ghasia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke
wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya
Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani
Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka
katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25
Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond
Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke
wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya
Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole kijana Baqir
Dhamji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka
katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25. Kulia
ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya MOI.