Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na Mwakilishi wa
JICA nchini Yasunori Onishi (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa
Japan kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji
safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.
Waziri
wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki
Okada (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa Japan kusaidia shilingi
bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama katika
baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.
---
Serikali ya Japan kupitia Shirika
la JICA imesaini mkataba wa kuisaidia Tanzania shilingi Bilioni 1.28
za kusaidia usambazaji maji katika mkoa wa Tabora .
Fedha hizo zimetolewa leo(jana)
na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mh. MASAKI OKADA katika sherehe
iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya
Tanzania Waziri wa Fedha Mh. Dkt. William Mgimwa alisema msaada huo
utasaidia kupunguza kero ya upatikanaji wa maji katika baadhi ya vijiji
mkoani Tabora na pia kukabiliana na vita dhidi ya umaskini.
‘’Ninafurahi ya kuona kwamba
makubaliano ya msaada huu tulio saini hivi punde utaiwezesha serikali
yako ya Japan kupitia kampuni ya JICA kutupatia fedha za Kijapan Yeni 76
milioni sawa na shilingi bilioni 1.28 za kitanzania, kwaajili ya
kusaidia utekelezaji wa usamabazaji maji vijijini katika mkoa wa
Tabora”. Mh. Dkt, Mgimwa alisema.
Aidha Dkt Mgimwa kwa niaba ya
Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania aliishukuru Serikali ya Japan kwa
msaada wake huo muhimu ambao umekuja muda muafaka wakati Tanzania iko
katika mapambano dhidi ya umaskini ikiwemo kuhakikisha wanapata maji
safi na salama.
Kwa
upande wake Balozi wa Japan
nchini Tanzania Mh, MASAKI OKADA alisema kuwa Japan tangu mwaka
1996,inatekeleza miradi sita ya maji katika mikoa ya Kagera ,Singida,
Manyara , Shinyanga ,Mwanza , Mara, Mtwara , Lindi, Pwani , Dar es
Salaam pamoja na Zanzibar.Alisema kuwa hadi hivi sasa jumla ya watu laki
nane na sitini elfu wamenufaika na miradi hiyo hapa nchini Tanzania.
Japan na Tanzania zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu ambapo hadi hivi sasa uhusiano wa Nchi hizo umedumu kwa muda wa miaka 50
Na
Benedict Liwenga
Idaya ya Habari Maelezo-Dar es Salaam