Friday, March 29, 2013

WAZEE WA YANGA WAKIPIGA DUA NDANI YA UWANJA WA JAMHURI.

WAKATI yanga wakikabiliwa na kibarua kigumu kesho kwa kupambana wenyeji wao Polisi Moro ambayo imeonekana kuzinduka kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu,wazee wa yanga wamenaswa jioni hii wakipiga duandani ya uwanja wa Jamhuri wakati vijana wao wakiendelea na mazoezi.
Walipohojiwa na Mtandao huu wazee hao walidai kwamba wanamuomba mungu awafanyiwe wepesi kwenye mchezo  kesho walidai kwamba ni mgumu.

Ugumu wa mchezo huo unatokana  timu zote mbili kuwa kwenye mazingila tofauti ambapo yanga wanaoongoza ligi hiyo wanapigania kutwaa ubingwa huku polisi inayoshika nafasi ya tatu kutoka chini ikibabana kujinasua katika janga la kushuka daraja,nani ataibuka kidede tusubiri kesho