Friday, August 30, 2013

Mwaka huu Mahindi ya Chakula bweleleeeee!!!!


Haya ni mahindi yanayonunuliwa na NFRA katika kituo chao cha Mbozi Mkoani Mbeya


Na; Msigwablog
Msimu huu wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA, wamefanikiwa kukusanya zaidi ya tani 160,000 za mahindi kati ya tani zote 200,000 wanazokusudia kununua kutoka kwa wakulima. Mkoani Ruvuma peke yake tayari wamenunua tani 36,000 kati ya tani zote 50,000 wanazotarajia kununua msimu huu

Hali hii imevunja rekodi kwa kuwa Mahindi yamenunuliwa kwa kasi kubwa. Matharani mwaka jana, mahindi kama haya ya safari hii yalinunuliwa kwa muda wa miezi sita lakini safari hii ni ndani ya mwezi mmoja.

Mkurugenzi Mkuu wa NFRA Charles Warwa anasema pamoja na wao kununua mahindi hayo, pia wanaendelea kuzijizatiti kwa kujenga maghala mengi zaidi ili waweze kuhifadhi mahindi yote ndani ya maghala badala ya kuyahifadhi nje.

Mwaka huu NFRA imefanikiwa kupata mahindi mengi kutokana na kununua mahindi kwa bei nzuri ya shilingi 500 kwa kilo moja inayomfikia mkulima moja kwa moja, hali ambayo kwa Mkoani Ruvuma wanunuzi wengine binafsi wameshindwa kuifikia bei hiyo na hata mahindi yao nao wanayapeleka kwa NFRA

SWALI NI JE???? 
Baada ya NFRA kumaliza kununua tani zao 200,000 kwa msimu huu, wanunuzi binafsi wataendelea kununua mahindi ya wakulima kwa shilingi 500 kwa kilo moja? au ndio mwanzo wa Majanga?