Saturday, August 3, 2013

Ruvuma Press wafanya mkutano wao wa kawaida, Mwambungu atoa neno.



Chama cha waandishi wa habari Mkoani Ruvuma Leo kinaendesha mkutano wake wa kawaida. Mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ambaye pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuwa makini katika kazi zao kwa kuhakikisha wanaanza kazi yenye kuwasaidia watanzania kukabiliana na changamoto za maisha ikiwemo kupambana na umasikini.

Aidha Mwambungu ameonya kuwa waandishi wa habari waepuke kuwa mawakala wa kuzalisha milipuko inayovuruga amani na kuleta mifarakano katika jamii.

Mkuu Huyu wa Mkoa ambaye amekua kipenzi wa karibu wa vyombo vya habari pia ametaka waandishi wa habari wajenge tabia ya kupendana, waache kuchimbanachimbana na Daima wajadili mambo yenye manufaa kwao na wananchi wanaowahudumia.

Katika Mkutano huo Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoani Ruvuma Andrew Chatwanga amemuomba Mkuu wa Mkoa na Meya wa Manispaa hiyo Charles Mhagama wasivunje jengo la kitega uchumi la chama hicho lililopo katikati ya mji ambalo Manispaa iliidhinisha livunjwe kutokana na taratibu za mipango miji.

Mwambungu amekubali ombi Hilo na ameisihi Manispaa ya Songea iongeze mwaka mmoja kwa Jengo Hilo kuendelea kuwepo.

Chatwanga pia amemuomba Mkuu wa Mkoa Mwambungu akisaidie chama hicho kutunisha mfuko kwa ajili ya mradi wa uanzishaji wa kituo cha Radio ambacho ununuzi wa vifaa na studio unaendelea kwa kutegemea michango ya wadau.