Saturday, August 3, 2013

Wadau mnamkumbuka Mwandishi wa Habari Mkongwe Agustino Mbunda?


Huyu ndiye Agustino Mbunda.

Leo nje ya mkutano wa kawaida waandishi wa habari katika Mkoa wa Ruvuma, nimekutana na Mwandishi wa habari wa Siku nyingi Mzee Agustino Mbunda.

Nimefurahi kukutana nae kwa sababu ni miongoni wapiganaji waliofanya kazi kubwa ya kuwaelewesha watanzania juu ya umuhimu wa fani hii.

Kwa wenye kumbukumbu Agustino Mbunda ndiye aliyefichua kashfa ya meno ya tembo mwaka 1988 iliyomhusisha aliyekua mbunge wa Songea Mjini Abdulabi Ally Yusuf, ambaye alitiwa hatiani na mahakama kuu na kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 12 Jela.

Mbunda pia ndiye aliyeandika habari kuhusu ugonjwa wa mihogo uitwao Cassava Mealbug ambao uliathiri mashamba mengi na kutishia Hali ya chakula. Maeneo yaliyoathirika ni pamoja ukanda wa mwambao wa ziwa Nyasa. Habari hii ndio ililazimu serikali kuagiza manyigu kutoka nchini Nigeria kwa ajili ya kukabiliana na wadudu wa cassava Mealbug. Inasemekana tatizo lilikomeshwa kutokana na kupandikizwa kwa manyigu hayo ambayo yapo hadi Leo.

Mkongwe huyu wa Habari pia aliandika historia miaka ya mwanzoni mwa 1980, (Tarehe kamili nasearch) aliporipoti juu ya mchezo mchafu unaofanywa na menejimenti ya ghala la mbolea la Makambako Mkoani Iringa, ambapo wakulima walikua wakinyanyaswa kupewa mbolea kwa kuwekewa ukiritimba huku mbolea hiyo ikipelekwa kwa wafanyabiashara na kuuzwa kwa bei juu. Aliyekua waziri Mkuu wakati huo Edward Moringe Sokoine alisafiri usiku kucha hadi Makambako na akafika na kukuta meneja wa ghala hilo kalala, akatuma mtu akamwamshe na alipofika na kuulizwa akakosa majibu na hapohapo kikaota nyasi

Pia aliandika habari kuhusu simba wala watu Tunduru, kukatokea upinzani kutoka kwa baadhi ya maafisa wanyamapori. Mmojawao akaamua kwenda Tunduru na yaliyomkuta nae akaliwa na Simba.

Big Up Mzee Mbunda, tupo pamoja and we are proud of you Sir