Friday, August 30, 2013

Breaking news!!!! Marekani yatangaza kuwa Serikali ya Bashar al-Assad imeua watu 1429 kwa silaha za sumu nchini Syria


 John Kerry - Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, 
Alipokua akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika Ikulu ya Marekani (White House)

Na Msigwablog 
Muda mfupi uliopita Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amezungumza na vyombo vya habari na kutangaza rasmi kuwa serikali ya Marekani inajua na ina uhakika wa ushahidi kuwa serikali ya Syria ya Rais Bashar al-Assad imehusika kuwaua watu 1429 wiki iliyopita kwa kutumia silaha za sumu. Kerry amebainisha pia kuwa Kati ya watu Hao wamo watoto 426 waliouawa kwa silaha hizo za sumu.

Aidha Kerry anasema serikali ya Syria imekua ikitumia silaha za sumu na hiyo ni sehemu ya mkakati wake wa kukabiliana na maadui wake huko mashariki ya Kati.

Aidha Waziri Huyu wa mambo ya nje wa Marekani anasema Rais Obama Anajua kuwa kukabiliana na tatizo la Syria kutakua na madhara makubwa lakini potelea mbali.

Haya sasa wadau, shughuli nyingine pevu inanukia Syria.

 Rais wa Syria Bashar al-Assad 
Mtuhumiwa wa kutumia silaha za sumu wiki iliyopita kulikosababisha vifo vya watu 1429