Saturday, July 6, 2013

Breaking News!!!!!!!! Ndege Boeing 777 yaanguka huko San Fransisco

TAHARUKI!!!!!


Taarifa tulizozipata hivi punde zinasema Ndege aina ya Boeing 777 inayoendeshwa na Asiana Airline imeanguka wakati ikikaribia kutua katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa San Francisco nchini Marekani.

Imefahamika kuwa ndege hiyo ilikua na abiria 290 na wafanyakazi 12 na iliruka kutoka uwanja wa ndege wa Seoul huku ikionekana kutoka moshi katika injini zake,  uwanja wa Ndege wa San Francisco umethibitisha kuwa ndege hiyo ni namba 214 na ilikua ikitokea Korea Kusini.

Watu walishuhudia tukio hilo wanasema walianza kuona bawa mojawapo la ndege likiwa na hitilafu na baadaye moto ukawa unafuka kabla ya kusikia kishindo kikubwa.

wanasema wakati ndege hiyo ikianguka kulikua na ndege nyingine iliyokua ikitua katika uwanja huo. Mara baada ya kuanguka milango ya dharula ilikua imefunguka kwa ajili ya watu kujinusuru.

Ndege hiyo ni miongoni mwa ndege kubwa za Korea Kusini

Habari zaidi zitawajia
 
 
Vikosi vya zimamoto vikiwa katika harakati za kuzima moto
 
kazi ikiendelea