Taswira za ajali ya ndege na uchunguzi unaoendelea
Moto Mkubwa ulifuka kabla ya vikosi vya zimamoto havijaudhibiti
Hatimaye imefahamika kuwa idadi
ya waliosalimika katika ajali ya Ndege iliyotokea katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa San Francisco Nchini Marekani ni 305 na ni watu wawili ndio
waliopoteza maisha. Kati ya waliosalimika wati 182 walilazwa Hospitali na
wengine 123 walitibiwa na kurejea
kuondoka.
Uchunguzi zaidi kuhusiana na
ajali hii bado unaendelea kufanyika. Ndege hii inaendeshwa na kampuni kubwa
kuliko zote huko Korea Kusini iitwayo Asiana Airlines. Ndege yenyewe ni aina ya
Boeing 777 na ilikua ni ndege namba 214.
Imethibitika kuwa Ndege hii ya
injini mbili ilikua na abiria 291 na wafanyakazi 16 na iliruka kutoka uwanja wa
Ndege wa Seoul Korea Kusini na kusafiri
kwa takribani saa 10 kabla ya kukutwa na ajali wakati ikitua katika uwanja wa
ndege wa San Francisco
Waliofariki dunia ni Binti Ye
Mengyuan na Wang Linjia wote ni raia wa China na walikaa katika viti vya nyuma
ya nege ambapo ndiko mshindo mkubwa wa kuanguka ulikopiga.