Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akialimiana na Leah Kayombo, Mke wa Mbunge wa Mbinga Mashariki, Gaudence
Kayombo baada ya kuwasili mjini Mbinga akitoka Nyasa kwa ziara ya mkoa
wa Ruvuma, July 18, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akisalimiana na Madaktari wa kujitolea Kutoka Korea ya Kusini na Laos
wanaofanya kazi katika hospitali ya wilaya Mbinga , Julai 18, 2013.
Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata
utepe kuzindua utelemshaji wa mabomba ya gesi kutoka kwenye meli kwenye
bandari ya Mtwara Julai 18, 2013. Mabomba hayo yatatandikwa chini ya
ardhi kusafisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Kulia kwake ni
Balozi wa China nchini, Dr. Lu na Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na
Madini , Stephen Masela. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph
Simbakalia.
Wairi Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia (wapili kushoto) wakati
alipozindua utelemshaji wa mabomba ya gesi kutoka kwenye meli kwenye
bandari ya Mtwara, Julai 18, 2013. Mabomba hayo yatatandikwa ardhini ili
kuwezesha usafirishaji wa gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akisalimiana na Hassan Kasuguru,nahodha alieingiza bandarini Mtwara
meli yenye mabomba ya gesi kutoka China wakati alipozindua upakuaji wa
mabomba hayo Julai 18, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta
na Balozi wa China nchini, Dr. Lu kabla ya kushuhudia upakuaji wa
mabomba ya gesi kwenye bandari ya Mtwara , Julai 18, 2013. Mabomba hayo
yatatandikwa ardhini ili kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es
salaam.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu