Saturday, July 20, 2013

UFUNGUZI WA GOAL INITIATIVE PROGRAMME

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akitoa vyeti kwa Wahitimu wa mpira wa Goal wakati wa ufunguzi wa mpango wa Goal Initiative uliofanyika katika shule ya Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi kutoka Benki ya Standard Chartered Bi. Liz Lloyd na kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Zanaki Bi. Rehema Tunzu na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo. 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akijiandaa kupiga mpira aliopasiwa toka kwa  kocha wa mpira wa Goal (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mpango wa Goal Initiative uliofanyika shule ya Sekondari ya Zanaki jana jijini Dar es Salaam. 
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Zanaki Bi. Rehema Tunzu akituliza mpira aliopasiwa toka kwa kocha wa mpira wa Goal Initiative (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mpango wa Goal Initiative. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Bi. Liz Lloyd ufunguzi huo ulifanyika jana shule ya Sekondari Zanaki jana jijini Dar es Salaam. 
 Mkufunzi wa mchezo wa Goal Bwana Brian Suskiewile akitoa maelekezo kwa Washiriki (hawapo pichani) jinsi ya kutumia mpira wa Goal wakati wa ufunguzi wa mchezo huo jana jijini Dar es Salaam katika shule ya Sekondari ya Zanaki, kushoto kwake ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa mafunzo ya mpango wa mchezo wa Goal Initiative. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Bi. Liz Lloyd. Ufunguzi huo ulifanyika jana katika shule ya Sekondari ya Zanaki iliyoko jijini Dar es salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.