Wednesday, July 10, 2013

HAYA NDIYO YALIYOJITOKEZA KATIKA UKAGUZI WA MADUKA YA DAWA MUHIMU MKOANI RUVUMA

Naibu Msajili baraza la famasi nchini Leah Chenya  akifanya ukaguzi katika duka la dawa
Naibu msajili baraza la famasi nchini Leah Chenya akiwa ameshika moja ya kidhibiti alichokuta katika duka la dawa
Mfamasia  akiangalia dawa zilizokamatwa katika duka la mfanya kazi wa serikali huku akiwa amefuta nembo ya MSD
Mtuhumiwa akohojiwa baada ya kukutwa akiuza dawa za serikali huku akitoa huduma za kuchoma sindano kwa wale wanaofika katika duka lake  hali hii imepelekea kufunga duka hilo na hatua kali zimechukuliwa dhidi yake pia ni mfanyakazi wa serikali
Hizo hapo juu ni dawa zilizokutwa katika duka hilo zikiuzwa kinyume na sheria
Huyu ni mtuhumiwa aliyekutwa akiuza dawa ambazo hazipo katika orodha ya dawa ambazo anatakiwa kuuza katika duka lake pia akiwa na dawa za serikali
Paul Sonda toka mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kanda ya Nyanda za juu kusini akiangalia mfuko wa dawa za serikali zilizokutwa zikiuzwa katika duka la mfanya kazi wa Hospital ya Serikali mkoani Ruvuma
Toka kulia ni Emmenuel Yohana toka wizara ya afya na ustawi wa jamii kitengo cha  dawa akionyesha moja kati ya kadi za clinik zilizokutwa kadika dula la dawa zikiuzwa na duka hilo ni lamfanyakazi wa serikali na wakushoto ni Paul Sonda toka mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kanda ya Nyanda za juu kusini
Toka kushoto ni Paul Sonda toka mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kanda ya Nyanda za juu kusini akijaza fomu za maelekezo na anayefuata ni  kaimu mfamansia wa wilaya ya Tunduru Ng'walida 
------------------------------------------------
WIZARA ya afya kwa kushirikiana na mamlaka ya chakula na dawa nchini(TFDA) imefanya ukaguzi wa kushitukiza katika maduka ya dawa muhimu  na zahanati mkoani Ruvuma kwa ajili utekelezaji wa kanuni na taratibu za uendeshaji wa maduka hayo na zahanati.
 
 Ukaguzi huo ulioshirikisha maafisa kutoka wizara ya afya,mamlaka ya chakula na dawa na ukaguzi kanda ya nyanda za juu kusini umefanywa katika wilaya zote za mkoa wa Ruvuma kwa kuanza na halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo baadhi  ya maduka ya dawa muhimu yaliyokaguliwa yalikutwa na dosari kutoka kwa watoa dawa na wamiliki wa maduka hayo.
 
Akizungumzia mafanikio na changamoto zilizobainishwa kwenye ukaguzi huo kwa baadhi ya maduka ya dawa muhimu na zahanati katika halmashauri ya wilaya ya Songea vijijini Naib Msajili wa baraza la famasi nchini Leah Chenya amesema baadhi ya maduka yamekutwa yakiuza dawa ambazo haziruhusiwi kuuzwa kwenye maduka ya dawa muhimu huku baadhi yakitoa huduma ya tiba pamoja na kuchoma sindano mambo ambayo ni hatari kwa walaji.

Amesema baadhi ya maduka hayo na zahanati kumekutwa dawa za serikali zikiuzwa baada ya kufutwa nembo za utambulisho wa alama za serikali kwenye maboksi ya dawa hizo hukubaadhi ya dawa zikiendelea kuuzwa wakatimuda wake wa matumizi umekwishapita na nyingine hazijasajiliwa na baraza la famasi nchini kwa ajili ya kutumika na wananchi na kuendelea kuhatarisha afya za walaji.
 
 Aidha amesema uamuzi wa kufanya ukaguzi huo wa kushitukiza mkoani Ruvuma ni kwa sababu mkoa wa Ruvuma ndiyo ulikuwa wa mfano wa kuanzishwa kwa mradi wa uboreshaji na kuanzishwa kwa maduka ya dawa muhimu badala ya maduka ya dawa baridi mpango ambao ulianzishwa kwa kanuni na taratibu zilizowekwa kwa pamoja na wizara ya afya na ustawi wa jamii na mamlaka ya chakula na dawa nchini.
 
Amesema pia lengo ni kuona mpango huo unafanikiwa kwa kiasi gani na kufahamu changamoto wamazokabiliana nazo watoa dawa na wamiliki wa maduka hayo ya dawa muhimu katika eneo ambalo mradi ulianzia na ukaguzi umebaini kuwepo kwa mafanikio na changamoto ambazo zinapaswa kufanyiwa kazi kwa ajili ya kulinda affya ya walaji wa dawa kwa sababu kila dawa ni sumu ikitumika bila kufuata maelekezo ya kitaalamu.
 
Akizungumzia changamoto zilizopo kwenye ukaguzi huo ni pamoja kidogo uliopangwa kwa ajili ya ukaguzi ikilinganishwa na ukubwa wa mkoa wa Ruvuma hivyo mafanikio yamefikia asilimia sitini na eneo kubwa halikuweza kufikiwa na ukaguzi huo ambao ni muhimu kufanywa mara kwa mara na wakaguzi wa ngazi ya kata na wilaya.
 
Naye Afisa kutoka wizara ya Afya na ustawi na jamii Emmanuel Yohana amesema dawa zote za serikali zilizokutwa kwenye maduka ya dawa muhimu na zahanati yamechukuliwa na kukabidhiwa kwa wafanga wakuu wa wilaya ili ziweze kutimika na wananchi kama mpango wa serikali unavyoelekeza na hatua zitachukuliwqa dhidi ya wahusika wa dawa hizo.