Wednesday, July 17, 2013

MATUKIO KATIKA PICHA YA ZIARA YA WAZIRI MKUU WIALAYANI NAMTUMBO

Waziri mkuu mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Brigedi ya Kusini  Brigedia Jenerali John Chacha wakati alipokuwa akiwasili wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma
Waziri mkuu mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa wilaya ya Namtumbo Alhaji Mohamed Maje wakati alipokuwa akiwasili wilayani hapo akitokea Tunduru

Waziri mkuu mizengo Pinda akisalimiana na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Namtumbo 
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mhe. Abdul Lutavi akisoma taarifa kwa Waziri mkuu Mizengo pinda wakati alipotembea Wilayani hapo
 Nivizuri kupanua wigo wa barabara ili kufungua zaidi Songea namtupo kipande cha kwanza, namtumbo Tunduru
Mkurugenzi wa wilaya ya Namtumbo Alhaji Mohamed Majeakisoma Taarifa ya mradi wa ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Namtumbo kwa  kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Mizengo Kayanza Pinda (MB). Mradi huo unatokana na ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa mara ya kwanza alipofanya ziara wilayani Namtumbo mwaka 2009 na kusisitiza tena Oktoba 2010 wakati wa kampeni ya Uchaguzi mkuu wa Octoba 2010.Baada ya wananchi kumweleza Mhe. Rais kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya Hospital.   Mradi huo umeghalimu kiasi cha Tshs 600.000,000.00
 Mkurugenzi wa wilaya ya Namtumbo Alhaji Mohamed akimpa taarifa ya jengo la hospital Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Mizengo Kayanza Pinda (MB)
 Waziri mkuu Mizengo Kayanza Pinda akifungua hospital
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Mizengo Kayanza Pinda (MB) wa katikati akipewa maelezo mafupi toka kwa mganga wa mkuu wa wilaya ya Namtumbo
Jengo la Hospital

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Mizengo Kayanza Pinda (MB) akimuuliza swali bwana mifungo wa Wilaya ya Namtumbo alipofika katika ufunguzi wa Machinjio ya Ng'ombe.
Mradi huu wa machinjio ulibuniwa na wananchi wa kijiji cha Minazini kupitia Mpango shirikishi wa fursa na vikwazo.Mradi huu ulianza kujengwa mwaka wa fedha 2008/2009 chini ya ya mpango wa maendeleo ya kilimo wa Wilaya (DADPS). Mradi upo katika kijiji cha Minazini kilometa tatu kutoka makao makuu ya Wilaya .Umejengwa kwa awamu tatu na umekamilika mwezi April 2013,Ujenzi wa jengo hili umeghalimu jumla ya shilingi 148,259,120 ikiwa ni jumla ya fedha zote zilizotolewa kwa awamu hizo .
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Mizengo Kayanza Pinda (MB) akikata utepe katika ufunguzi wa Machinjio ya Minazini wilayani Namtumbo
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Mizengo Kayanza Pinda (MB) akivaa koti maalum wakati wa kukagua Machinjo 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Mizengo Kayanza Pinda (MB) akikata utepe
katika ufunguzi wa Mitambo ya umeme wa Jeneleta wilayani Namtumbo
Waziri mkuu akimalizia kukata utepe katika ufunguzi wa Mitambo ya umeme wa Jeneleta wilayani Namtumbo
Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akipewa maelezo na Mhandisi Stevine Manda baada ya kuzindua  mitambo ya umeme
Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akiwa katika picha ya pamoja
Bango
Hawa ni baadhi ya viongozi mbalimbali wachama na Serikali wakiwa na Waziri Mkuu katika ziara yake Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma
 Toka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Abdallah Lutavi akiteta jambo na  Mkurugenzi wa wilaya ya Namtumbo Alhaji Mohamed na wa mwisho kushoto ni Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwasalimia wananchi wa namtumbo wakati akiingia uwanjani kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa Namtumbo
 Waziri Mkuu Mizengo  Pinda akivishwa vazi la jadi na Wazee wa kimila wa Namtumbo   na Kumuomba aspire marungu wala rushwa. Waziri Mkuu Pinda ametegua kitendawili cha kuhitaji mkoa wilaya za Tunduru na Namtumbo na kuwataka waanzishe mchakato wa kuomba mkoa huo kusukuma maendeeleo yaliyodumaa kwa miundombinu duni na kuwa na eneo la utawala linalokadiriwa kufikia km za mraba 40 elfu.
Waziri mkuu akikabidhiwa Chidonga(Lungu) na mzee wa kimila alipo
Waziri mkuu Mizengo Kayanza Pinda akipokea zawadi ya Kichenje
VIA/demashonews