Sunday, July 7, 2013

Tahariri Hongera Raia namba Moja



Tahariri!

Hongera JK.

Leo nilikua napitia baadhi ya mambo ya kimsingi yaliyofanywa na Raia namba Moja wa Tanzania (Mnamfahamu). inawezekana upo mjadala lakini bila kujali munkali za watu nimechagua kusema Hongera JK.

Nina ndoto kuwa, safari ya mabadiliko ya watanzania na maisha yao na uchumi wao inaweza ikaanzia kwenye program mumihu ya “Big Result”

Nionavyo Mimi hii ikichanganywa na Katiba tutakayoamua watanzania kwa kuzingatia changamoto za dunia na mustakabali wa maisha ya binadamu wa sasa, utakua ni muarobaini wa kutosha kwa matatizo yetu.

Haya ni mawazo huru, na nayamalizia kwa kusema tunapojadili mustakabali wa Taifa tuwe na mawazo huru tusiongozwe na mihemuko ya itikadi za kisiasa, kidini, kikabila, kimajimbo wala ubinafsi. Dawa ya matatizo ya watanzania itatatuliwa na sisi wenyewe watanzania tukiamua kwa pamoja kuyakabili.

Na ndio maana nimechagua kusema Hongera JK, kwa sababu huyu jamaa ameruhusu haya yote kufanyika.

Mnyonge mnyongeeni, haki yake Mpeni.

By Mimi.