Mkurugenzi
wa Shirika la kimatifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni Vibeke Jense
katikati akimfahamisha kitu Mkurugenzi wa Tume ya Utangazaji Omar Chande
mara baada ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vya Idara ya Habari
Maelezo, kulia Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali
Mbarouk.Hafla hiyo ilifanyika Wizara ya Habari Kikwajuni mjini
Zanzibar.Waziri
wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk, akimkabidhi
zawadi ya mlango Mkurugenzi Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni Vibeke Jense, huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo-Zanzibar).
Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar
Shirika
la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limeikabidhi vifaa
Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar vyenye thamani ya
Shilingi Milioni 46 ili kuijengea uwezo Wizara hio.
Vifaa
hivyo ni pamoja na Kamera mbili, Lenzi mbili, Digital Recorder 7,
Vipaza sauti viwili, TV moja, pamoja na Mashine 2 za kutayarishia
vipindi.
Akikabidhi
vifaa hivyo Mkurugenzi wa UNESCO Tanzania Bi Vebeke Jense amesema lengo
la kuletwa vifaa hivyo ni kuijengea uwezo Wizara hiyo ili kuleta
mabadiliko hasa katika upande wa tasnia ya habari.
Baada
ya Makabidhiano hayo Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said
Ali Mbarouk amelishukuru Shirika hilo kwa kuwa karibu na Wizara yake na
kuahidi Vifaa hivyo vitatumika ipasavyo ili kutimiza lengo
lililokusudiwa.
Waziri
Mbarouk amesema iwapo Wafanyakazi watavituza Vifaa hivyo na kuvifanyia
kazi ipasavyo hapana shaka mabadikliko katika wizara hiyo yataonekana
hasa ikizingatiwa kuwa ni vifaa vya kisasa.
Amesema
kwa muda Mrefu Idara ya Habari Maelezo imekuwa na upungufu wa Vifaa
katika kukabiliana na majuku yake ya kila siku na kwamba upatikanaji wa
Vifaa hivyo itakuwa ni suluhu ya tatizo hilo.
Kwa
upende wake Mkurugenzi wa Tume ya Utangazaji Omar Chande amesema
itakuwa ni jambo jema iwapo Vifaa hivyo pia vitatumika katika kuandaa
habari za vijijini badala ya mijini pekee.
Aidha
amefahamisha kuwa baadhi ya vifaa vinatarajiwa kufika siku za karibuni
ili kuiwezesha Idara ya Habari Maelezo kuwa ya kisasa na kutimiza
maelengo yake.
Msaada
huo wa Vifaa vyenye thamani ya Milioni 46 umekuja kufuatia ahadi
iliyotolewa na Shirika la UNESCO kwa Idara ya Habari kuiwezesha kupata
Vifaa ambavyo vitasaidia katika kuendeleza majukumu yake ya kila siku.