Thursday, July 4, 2013

Jinsi mzozo unavyoendelea kwenye familia ya Mzee Mandela

Kijijini Qunu
Kijijini Qunu
Mjukuu wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela, Mandla Mandela ameshutumia vikali kwa kitendo chake cha kuhamisha mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mzee Nelson kutoka kwenye makaburi waliyokua wamezikiwa.
Al Jazeera wameripoti kwamba tayari familia ya mzee Nelson Mandela inatajwa kufikiria kuchukua hatua za kisheria zaidi kwa mjukuu huyo mkubwa kuliko wote wa Mandela ambae alifanya hicho kitu bila idhini ya familia 2011 na kuzika mabaki karibu na nyumbani kwake miaka miwili iliyopita.
.
Familia imekua ikipelekeshana nae na kulumbana kuhusu ni wapi atazikwa Mzee Mandela atakapofariki kwa sababu mwenyewe alishawahi kutamka karibu miaka 20 iliyopita kwamba akifa azikwe kwenye kijiji cha Qunu lakini Mandla amekua akifanya mipango Mzee akazikwe MVEZO.
Nyumba ya mzee Mandela kijijini Qunu
Nyumba ya mzee Mandela kijijini Qunu.
Nelson Mandela na wajukuu
Nelson Mandela na wajukuu
Pamoja na hiyo ripoti ya Al Jazeera, BBC wameripoti kwamba Mandla ameshindwa katika hiyo kesi ambapo Mahakama kuu iliamua maiti hizo lazima zirejeshwe katika makaburi yao Jumatano.
Mandela anaendelea kuugua hospitalini na haijulikani ikiwa mawakili wa Mandla wataka rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.
 
Jamaa za familia ya Mandela waliwasilisha kesi ya uhalifu dhidi ya Mandla kwa kosa la uhalifu.
Msemaji wa polisi, Mzukisi Fatyela aliambia BBC kuwa maafisa wa usalama watachunguza tuhuma dhidi ya Mandla za kufukua makaburi kinyume na sheria.