Wednesday, July 10, 2013

WANANCHI WAUA SIMBA KWA SUMU YA PANYA TUNDURU



Na Steven Augustino, Tunduru
WAKAZI wa Kijiji cha Wenje katika Kata ya Nalasi Mashariki Wilayani
Tunduru Mkoani Ruvuma wamefanikiwa kuwaua Simba wa wili Kati ya Simba
Watatu waliokuwa wanatishia maisha ya wananchi Kijijini hapo.

Diwani wa kata hiyo Bw. Kalengo Kuwale  alisema kuwa tukio hilo
limefanikiwa baada ya wananchi hao kutia Sumu ya Panya katika Mzoga wa
Nyama ya Mbuzi aliyekuwa ameuawa na Simba hao.

Alisema hadi Wanafanikiwa kuwaua Simba hao walikwisha fanikiwa kuua
zaidi ya mifugo 30 toka kundi la simba hao livamie katika kijiji hicho
Julai 6 mwaka huu pamoja na kutishia usalama wao .

Alisema katika tukio la Julai 6 mwaka huu Simba hao waliua Mbuzi 9 na
mbwa mmoja, Julai 7 wakaua Mbuzi 5, Julai 8 mbuzi 7 na Julai 9 ambapo
simba hao pia walifanikiwa kuua mbuzi 8 wote  wakiwa ni mali ya
wananchi wa Kijiji hicho.

Kwamujibu wa Diwani Kuwale aliitaja mifugo hiyo kuwa ni zaidi ya mbuzi
30 na mbwa mmoja na kwamba maamuzi ya kuwategea Sumu hiyo kulifuatia tukio la Viongozi wa idara ya maliasili Wilayani humo kuchelewa
kupeleka Askari wao wakati huo wananchi wakikosa amani kutokana na
kuzagaa kwa simba hao Kijijini kwao.

Akizungumzia tukio hilo kaimu afisa wanyama pori wa Wilaya hiyo Bw.
Peter Mtani mbali na kudhibitisha ofisi yake kuwa na taarifa hizo
alisema kuwa tayari amekwisha peleka askari kwa ajili ya kumshwaga
Simba aliyebaki na kumuwezesha kurudi Porili ili asisababishe madhara
mengine.

Mtani aliendelea kufafanua kuwa chanzo cha simba hao kuvamia katika
makazi ya wananchi ni pamoja na kushamiri kwa matukio ya wafugaji
kuvamia na kuweka makazi katika maeneo ya hifadhi za Wanyama pori
likiwemo Pori la hifadhi ya Taifa la Selous kwa upande wa Tanzania na
Mpakani mwa hifadhi ya Pori la Niasa kwa Upande wa Nchi ya msumbiji.

Akizungumzia Tukio la wafugaji hao Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw.
Chande Nalicho alisema kuwa tayali ofisi yake kwa kushirikiana na
Ofisi ya Mkurugenzi Mtengaji wa Halimashauri ya Wilaya hiyo wameandaa
mikakati ya kufanya msako kwa wafugaji wote waliovamia katika mapori
tengefu na hifadhi za taifa kwa ajili ya kuanza kuwaondoa katika
maeneo hayo.
Mwisho