Mkuu wa mkoa wa RUVUMA SAID MWAMBUNGU amezindua maadhimisho ya 17 ya wiki ya maziwa nchini na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kunywa maziwa kwa wingi kwa lengo la kuboresha afya zao
Akizungumza na wananchi na wadau wa maziwa katika viwanja
vya manispaa ya SONGEA MWAMBUNGU alisema
kati ya lita bilioni 1.6 za maziwa zinazozalishwa hapa nchi kwa mwaka ni
wastani wa lita 11.6 tu zinazonywewa na mtu mmoja wa mkoa wa Ruvuma kiasi
ambacho ni kidogo ukilinganisha na viwango vya kimataifa vya lita 200 kwa mtu
kwa mwaka.
Maadimisho
hayo ya wiki ya maziwa ambayo yanafanyika kwa mara
ya kwanza mkoaniMkoani Ruvuma ambapo MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID
MWAMBUNGU aliwaamasisha wananchi wa mkoa wake kuongeza kasi ya unywaji
wa maziwa
sambamba na kufuga ng’ombe wa kisasa wanaotoa maziwa mengi badala ya
ng’ombe wa
asili ambao uzalishaji wao ni mdogo.
Maadhimisho haya yameambatana na maonyesho ya bidhaa
mbalimbali za maziwa pamoja utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa
unywaji maziwa, usindikaji na uzalishaji wake hata hivyo baadhi ya wadau wa maziwa kutoka vyama
vya usindikaji maziwa wamesema maziwa mengi yanayozalishwa hapa nchini
yanashindwa kuwafikia wanywaji kutokana na asilimia chache zinazosindikwa.
Wiki ya maziwa iliyozinduliwa leo mkoani hapa
itaendelea kwa siku nne zijazo ambapo hapo kesho madereva wa pikipiki maarufu
kama YEBOYEBO, wafungwa na wagonjwa hospitalini watagawiwa maziwa ya bure kama
sehemu ya uhamasishaji