Picha
juu na chini ni Foleni ya magari ya takataka zaidi ya 30 yaliyokwama
katika dampo la Pugu Kinyamwezi kwa takribani siku tatu kutokana na
ubovu wa miundo mbinu huku taka zikiendelea kuoza ndani ya magari hayo
na kusababisha harufu mbaya kwa wakazi wa maeneo hayo.(Picha na Dewji
Blog).
Katapila likiwa katika jitihada za kuchonga barabara ili angalau magari ya taka yaweze kufika eneo la dampo kuwamga taka.
Masela
wakifurahia baada ya gari la taka lililokuwa limekwama kufanikiwa
kupandisha kilima katika dampo hilo kuelekea kumwaga taka.
Wanafunzi
wa shule ya msingi walipokutwa na camera yetu katika dampo hilo
wakikatiza na kuzubaa zubaa eneo hilo wakati wa saa za shule.
Wakazi
wa maeneo hayo wakichambua takataka hizo kujiokotea chupa tupu za maji
na mifuko ya plastiki ikiwa ni ajira waliyojitengenezea katika kuendesha
maisha yao ya kila siku, shuhuda wa Mo Blog Zainul Mzige anatanabaisha
kwamba chupa wanazookota huuzwa kilo moja kwa shilingi 100 kitu
kinachowapelekea wafanyaji wa biashara hii kuwa watumwa wa pombe za
kienyeji haswa almaarufu kama Gongo au Chang'aa.
Mitaro ya maji machafu ikiwemo mikojo na vinyesi katika dampo hilo...Je kuna kupona kweli hapa????
Magari
ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni nayo yalikwama kwenye dampo
hilo, pichani yakielekea kuwamga taka hizo baada ya barabara kutengemaa
kwa kiasi.
Pichani
ni juu na chini Mama lishe wakitoa huduma ya chakula chini ya mti
katika eneo lilizongukwa na taka ikiwemo harufu kali na Nzi wanaozunguka
hapa na pale lakini vibarua wa dampo hilo hawana la kufanya.
Moja
ya Katapila lililokodiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam
likiwa limekufa na kushindwa kufanya kazi kutokana na kukwamisha na
miundo mbinu ya eneo hilo la dampo huku mafundi wakihangaika kulifufua.
Meneja wa Dampo la Pugu Kinyamwezi Bw. Richard Katiti akizungumzia
changamoto kubwa wanayokabiliana nayo katika kipindi hiki cha mvua kitu
ambacho kinawapelekea kutumia jitihada za ziada ikiwemo kukodisha magari
(Vijiko) ili kujitahidi kuhakikisha miundo mbinu ya kufika katika dampo
hili inapitika kwa urahisi ili kuondoa vikwazo kwa magari yanayotoa
huduma ya kuzoa taka mjini.
Devera wa gari la Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Bw.
Ramadhani Sufi akielezea adha wanayoipata ambapo amefafanua kuwa inafika
mahali inawabidi kulala siku mbili na gari zenye mzigo wa taka katika
mazingira ambayo ndio wanayoshinda na kula kitu ambacho kinaweza
kuwasabishia maradhi hivyo ameliomba jiji kurekebisha hali hiyo ili
kuwaepusha na mazingira hatarishi kiafya kutokana na uchafu
unaolundikana mahali pamoja kuanzia dampo hadi kwenye magari.
Aidha
amefafanua kuwa hali hiyo inasababisha kutuchafulia jina la kampuni
yetu na kuonekana kama hatufanyi kazi kumbe tatizo lipo kwenye utaratibu
mzima wa Manispaa na suala la miundo mbinu.Pia ameshauri jiji
liongezewe uwezo kutokana na kuwa na vyombo vichache na chakavu kitu
kinachopelekea kuzidiwa katika kutoa huduma katika dampo hilo.
Mmoja
wa madereva wa magari ya taka yaliyokwama kutokana na miundo mbinu
mibovu Bw. Frank John akielezea kero ya kwenye dampo la taka lililopo
maeneo ya Pugu Kinyamwezi ambapo amesema taka zimelundikana barabara
hazipitiki hata magreda ya kuzoa hayana pakupita na kuwaomba watu
wanaohusika na dampo kujaribu kutengeneza njia mbadala na kushauri
itafutwe njia kipindi cha Masika taka ziwe zinamwaga sehemu nyingine na
kipindi cha Kiangazi kiwe na sehemu yake na kushauri mamlaka
zinazohusika na usafi zijifunze kutoka kwa wananchi na sisi tujifunze
kutoka kwao.
Aidha Bw. John amewataka viongozi wahusika kutokaa maofisini na
kutembelea maeneo husika na kujiuliza kwanini gari zinakwama na kuongeza
kuwa tatizo hilo limepelekea lawama kwa baadhi kampuni za usafi
kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa wakati.
Hii
ndio hali halisi ya viroba vya uchafu vilivyolundikwa katika eneo la
Pugu Kwalala pembezoni mwa barabara na makazi ya watu ambapo wananchi
wamekuwa wakizilalamikia kwa sababu kipindi cha mvua vinaweza
kuwasababishia magonjwa ya milipuko ikiwemo Kipindupindu.
Mkazi
wa eneo la Gongo Mwisho wa lami - Pugu Kwalala Bw.Erasto Njau
akilalamikia ubovu wa magari ya taka ya Halmashauri ya Manispaa ya jiji
la Dar es Salaam na vile vile utaratibu mbovu wa ukusanyaji wa taka
ambapo hata kama gari imeharibika yangetumika magari mengine kuja kubeba
taka suala ambalo linalohusu uongozi wa Manispaa ambao ndio
unaogharamia magari yanayobeba taka kitu ambacho kinaonyesha utaratibu
wa ubebaji taka bado haujakaa sawa.
Mama Lishe Asha Omari Dundo akizungumzia
kero ya Mlundikano wa taka katika eneo lake la biashara ambalo sio
dampo rasmi la kutupia takataka na anapouliza anaambiwa magari yamekwama
dampo kutokana na ubovu wa miundo mbinu kitu ambacho ni hatari kiafya
kwa wateja wake wa chakula ambacho ndio biashara anayoifanya kwa ajili
ya kusomesha watoto na kila anapouliza hapewi jibu linaloeleweka na
ameiomba serikali kutupia macho swala hilo kwa sababu kumekuwa na kauli
tofauti malori yamekwama na malori mabovu.
Mama Lishe Asha Omari Dundo akiwaandalia wateja wake chakula cha mchana katika eneo ambalo ni hatarishi kwa walaji.
Mkuu
wa Afya Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam Bw. Membe
Protus Membe akizungumzia jitihada za Manispaa katika kupambana na
tatizo la mlundikano wa magari ya taka yaliyokwama katika eneo la
Dampo la Pugu Kinyamwezi kutokana na ubovu miundo mbinu ya barabara
unaopelekea kukwamisha zoezi la ukusanyaji taka katika maeneo mbalimbali
ya jiji la Dar na kusababisha mlundikano wa taka nyingi kwa muda wa
kipindi cha siku hizi tatu.
Hata
hiyvo amesema katika muda wa siku tatu kuanzia leo Manispaa
itahakikisha inarekebisha miundo mbinu ya kuelekea dampo ili kuweza
kupunguza msongamano uliopo wa magari ya taka yaliyokwama yaweze kurudi
mjini kuendelea na ubebaji wa taka.
Chanzo: haki-hakingowi.blogspot.com