Friday, May 24, 2013

Mikutano ya vyama vya siasa na Maandamano vyapigwa marufuku Ruvuma

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki

Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limepiga marufuku maandamano na mikutano yote ya vyama vya siasa mkoani humo kutokana na sababu za kiusalama.

kwa agizo hili la Jeshi la Polisi maana yake hata Mkutano wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA uliopangwa kufanyika Mei 26, 2013 umepigwa marufuku.

Mkutano huo ulipangwa kutanguliwa na maandamano ya amani ya wafuasi wa CHADEMA ambayo yalipangwa kuanzia katika Chuo Kikuu Huria Mjini SONGEA hadi eneo la Matarawe ambako kungefanyika mkutano wa Kampeni ya M4C.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deus Nsimeki amewataka wananchi kutohudhuria maandamano hayo ya CHADEMA na Mkutano wao uliopangwa kufanyika huko Matarawe 26/05/2013 kwa kuwa shughuli hizo hazijaruhusiwa kufanyika.