Tahariri ya Gerson
Msigwa.
Awali ya yote napenda
kuwapongeza na kuwashukuru wasomaji wote Blog yangu.
Nawaahidi kuwa pamoja
na majukumu yanayonikabili katika ujenzi wa Taifa, hamtajutia kunitembelea
katika Blog hii na ukurasa wangu wa Facebook.
Nimeamua kwa dhati
kuwa na ukurasa wa “Tahariri ya Gerson Msigwa” Mahali hapa nitakua nikimulika
kitaaluma, kwa uchambuzi mfupi juu ya yale ninayoyaamini katika fani hii ya
uandishi wa habari. Kwa maoni yangu hapa ndipo mahali ninapoweza kutoa mchango
wangu wa mawazo kuhusu fani hii na mimi naamini kuwa itakua mahali muafaka pa
kukirithisha kizazi kinachonifuata juu ya fani hii ya uandishi wa habari. Sina maana
kuwa kila nitakachoandika hapa ni msahafu, hapana. Ni maoni yangu tu.
Hivyo basi nawaalika
wadau kushirikiana name katika safu hii, na nyie pia mnaweza kutoa maoni yenu
ili mradi tujadili mambo kwa faida ya fani ya uandishi wa habari tuliyoisomea
na tunayoitumikia.
Tahadhari; Tahariri
zangu zote hazitakua na mtazamo wowote wa Kisiasa, Kidini, Kikabila wala
Kikanda na naomba hata mtakaopendezwa kushiriki mjadala muongozwe na mtazamo
huo. Kwa niliowakwaza kwenye hili wanisamehe kwa sababu mimi ni miongoni mwa
watu wanaoamini kuwa binadamu wote ni sawa, dini, siasa, kanda na makabila
havina faida yoyote kuvishabikia.
Yatakayokuwemo kwenye
tahariri hii ni yangu binafsi na hayahusiani na taasisi yoyote wala mamlaka
yoyote, wala kikundi chochote, wala tabaka lolote nakadharika.
Kwa hiyo, Karibuni
wadau.