Thursday, May 23, 2013

Tembo wa Selou hatma yake nini?

Mkuu wa Kikosi cha kuzuia ujangili kanda ya Kusini Obeid Mmari akionesha pembe zilizokamatwa kwa waandishi wa habari. Kulia kwake ni Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deus Nsimeki na nyuma ya RPC ni mwandishi wa habari Mkongwe Gideon Mwakanosya wa PST.

Hapa zimekamatwa pembe 11 na mtuhumiwa ni Issa Omary Mayono (48) Mkazi wa Namtumbo Mkoani Ruvuma.

RPC Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki akionesha pembe zilizokamatwa kwa waandishi wa habari hawapo pichani.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili kanda ya kusini Obeid Mmari kilo moja ya jino la tembo ina thamani ya dola za kimarekani 550. Na hapa zimekamatwa kilo 42.6 hivyo jumla ni dola za kimarekani 23,430. kwa hesabu za haraka kwa madafu hapo ni sawa na karibu shilingi 39,000,000 za kibongo. Lakini ukipiga hesabu kwa tembo sita waliuawa, tembo mmoja ana thamani ya dola 15,000 za Marekani, hivyo mara sita ni sawa na dola 90,000 ambazo ni sawa na shilingi 149,000,000/= za kibongo.

Haya kazi ipo hapo, Majangili ndio hao wamechachamaa, sipati picha baada ya miaka mitatu minne ijayo porini kutakuwa na tembo? au vitabaki vicheche na ngiri. 

Imbombo jilipo!!!!