Friday, May 10, 2013

Taswira Kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchini:Kikao Cha Wakurugenzi, Makamishna,Maafisa Bajeti na Maafisa Ununuzi wa Wizara Chaanza Mkoani Morogoro kama sehemu ya maandalizi ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2013/2014

Mkurugenzi wa Idara ya Ugavi na Ununuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mapesi Manyama aliyesimama akitoa maelekezo ya namna ya kuandaa Mpango kazi na Ununuzi kwa Maafisa Bajeti wa Jeshi la Polisi  katika kikao kazi cha kuandaa Mpango huo kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 kwa ajili ya Jeshi hilo  kikao kikao hicho kinaendelea mjini Morogoro, Wa pili kutoka kushoto aliyekaa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi.
  Maafisa Bajeti wa Idara ya Zimamoto na Uokoaji  wakiwa katika zoezi la kuandaa Mpango Kazi na Ununuzi kwa ajili ya Idara hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi  ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2013/2014 katika kikao kazi kinachoendelea katika Hoteli ya Edema  mjini Morogoro. 
 Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Magereza pichani wakiandaa Mpango kazi na Ununuzi wa Idara yao kwa ajili ya ajili ya utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2013/2014 katika kikao kazi kinachoendelea katika Hoteli ya Edema  mjini Morogoro.  
 Sehemu ya Maafisa Bajeti wa Idara ya Uhamiaji wakiwa pamoja na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Idara hiyo. Bw. Piniel Mgonja watatu kutoka kushoto wakiandaa Mpango kazi na Ununuzi  wa Idara yao ikiwa ni sehemu ya Maandalizi ya Utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2013/2014  katika kikao kazi kinachoendelea katika Hoteli ya Edema  mjini Morogoro. 
 Sehemu ya Maafisa Bajeti, Maafisa Ugavi na Ununuzi  pamoja na Kaimu Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Edwin Makene wa kwanza kutoka kushoto wakiwa katika zoezi la kuandaa  Mpango kazi na Mpango wa Ununuzi kwa ajili ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 wa wizara hiyo katika kikao kazi kinachofanyika mjini  Morogoro.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi watatu kutoka kushoto kwa waliokaa  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi, Makamishna, Maafisa Bajeti na Maafisa Ununuzi  wa Wizara hiyo wanaoshiriki katika kikao  kazi cha Kuandaa mpango kazi na mpango wa ununuzi  kwa ajili ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2013/2014, wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ugavi na Ununuzi Bw. Mapesi Manyama wa wizara hiyo, kikao hicho kimeanza jana katika hoteli ya Edema mjini Morogoro

Na
Christina R. Mwangosi
Afisa habari
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchini