MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU WA PILI KUSHOTO AKIWA PAMOJA NA
MKURUGENZI WA MKUU WA TAKUKURU DKT EDWARD HOSEA NA KATIKATI NA KAMANDA
WA TAKUKURU MKOA WA RUVUMA DAUD MASIKO KATIKA PICHA YA PAMOJA NA
WATUMISHI WA TAASISI HIYO MKOANI RUVUMA
........................................
IMEELEZWA kuwa
mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa nchini ambavyo vinazidi kuongezeka siku
hadi siku ni jukumu la kila mmoja katika jamii ikiwa ni pamoja na viongozi wa
serikali na viongozi wa taasisi za
kidini kwa sababu rushwa ipo katika mihimili yote ya serikali huku baadhi ya
vitendo vya viongozi na mfumo wa uongozi ukiruhusu kuwepo kwa mianya ya rushwa.
Akizungumza katika
mafunzo ya siku moja kwa viongozi wa madhehebu ya dini ya kiislamu na kikikristo
wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma yaliyofanyika mjini Songea mkoani Ruvuma Mkurugenzi
Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini Dkt Edward Hosea alisema
kuwa kutokuwepo kwa uwazi,uwezo wa uwajibikaji wa viongozi na watendaji wa serikakali
kuwepo kwa mianya ya rushwa.
Alisema kuwa kwa
sababu maadili ya umma yametiwa unajisi mbele ya madhabahu ya kidini na hasa
nyakati za chaguzi mbali mbali taasisi imeona umuhimu wa kuwashirikisha
viongozi wa dini mbili kubwa hapa nchini kwa kuwapatia mafunzo ya namna ya
kudhibiti na kupambana na rushwa kwa sababu rushwa ni suala mtambuka linalogusa
kila eneo na kila mwananchi.
Dkt. Hosea aliwaambia
viongozi hao wa dini kuwa kutoa na kupokea rushwa ni dhambi lakini pia ni kosa
la jinai hivyo kuna kila sababu ya kutafakari kwa pamoja namna ya kuitokemeza
rushwa kwa umnoja wa taifa na siyo
busara kuliacha jukumu hilo mikononi mwa taasisi hiyo pekee kwa sababu wahusika
wa rushwa wapo katika kila sekta na hasa sekta zinaziotoa huduma kwa wananchi.
Akizungumzia mianya
ya kukuwa kuwa vitendo rushwa nchini ni pamoja na kuwepo kwa mapungufu katika
utawala bora na uwajibikaji wa viongozi na watendaji wa sekali na sekta binafsi
ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa utawala wa kisheria kwa baadhi ya viongozi na
watendaji wa sekta zinazotoa huduma kwa umma kwa kutokuwepo kwa uwazi na uwezo thabiti
wa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Akizungumzia madhara
ya rushwa kwa jamii alisema kuwa mtu mwenye kipato cha chini ndiye muathirika
mkubwa wa rushwa kuliko mwenye kipato kikubwa kwa sababu mwenye kipato cha
chinji hulazimika kutoa rushwa kubwa huku mwenye kipato kikubwa akitoa rushwa
ndogo na vitendo hivyo huambatana udanganyifu,wizi,ubadhirifu na mmomnyoko wa
maadili na viwango vya rushwa kwa kwa watu wenye kipato cha chini kikiwa ni
asilimia 3.3 huku wenye kipato kikubwa ni asilimia 0.9.
Akijibu maswali ya
baadhi ya viongozi wa dini waliotaka kufahamu juu ya utendaji wa taasisi hiyo
katika kushughulikia rushwa kubwa ambazo zimekuwa zikilalamikiwa nia wananchi
walio wengi alisema taasisi imepewa mamlaka ya kuchunguza lakini mamlaka ya
kushitaki ya kwenye ofisi ya mwendesha mashitaka wa serikali kwa mfumo wa muundo
wa taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana
na rushwa hauipi tasisi iwezo wa kushitaki bal;I kuchunguza.
Awali akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said
Mwambungu mbali ya kumpongeza mkurugenzi
mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini kwa uamuzi wa kuendesha
mafunzo kwa viongozi dini kuhusu mapambano dhidi ya rushwa lakini aliwaomba
viongozi wa dini kusaidia katika jukumu la kudumisha amani na utulivu wa nchi kama
ulivyoasisiwa na waasisi wa taifa.