Mmoja wa wananchi wanaoshiriki katika ulinzi wa Pori la Akiba la Selou akingoa jino la Tembo aliyeuawa na majangili na kisha kukurupushwa na askari wanyama pori kabla hajafanikisha mpango wake wa kuchukua meno ya tembo huyu. Wadau wa wanyamapori wanabashiri kuwa hivi sasa idadi ya tembo wanauawa kwa ujangili ni kubwa mno kiasi cha kuhatarisha uwepo wa wanyama hao katika kipindi kifupi kijacho endapo hatua za kukabiliana na ujangili hazitachukuliwa haraka na kwa nguvu kubwa.
Meno ya Tembo yaliyokutwa yakiungua kwa moto baada ya watu wanaosadikiwa kuwa majangili kukurupushwa na askari wanyama pori wakati wakijiandaa kukamilisha zoezi la kukausha meno hayo ili yasafishwe kwenda sokoni
Sehemu ya Pori la Akiba la Selou ambalo kwa sasa linakabliwa na chngamoto kubwa ya kukithiri kwa vitendo vya ujangili unaotishia kutoweka kwa wanyama hasa tembo.
Wakati Tembo wakiwa hatarini kutoweka kutokana na ujangili wanyama wengine wanaendelea kupeta akiwemo ngiri huyu ambaye ni mzee. hatari anayokabiliana nayo ni ya kuliwa na simba, chui, duma na wakati mwingine mbwa mwitu. hata hivyo wataalamu wa wanyamapori wanasema wanyama kama ngiri ni halali kuliwa kwa sababu wapo porini pamoja na umuhimu wao pia ni chakula kwa wanyama walao nyama.
Pundamilia nao mambo yao poa huko porini.