Thursday, May 16, 2013

KUTOA NI MOYO " TUMSAIDIE KIJANA HUYU "

Mohamed Kandije (31) 
.....................................................................
Na Stevie Chindiye, Tunduru
Naomba nianze kwa kutumia msemo wa wahenga kuwa Kabla hujafa hujaumbika huyu unaye muona hapo  ni Mohamed Kandije (31) mabaye ni Mkazi wa Kijiji cha Tindinya katika Kata ya Ngapa Tarafa ya Nakapanya Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma anaomba msaada wako wa hali na mali kutoka kwa watu Binafsi na taasisi ili aweze kupata Mikono ya Bandia na kumuwezesha walau kujitetea katika mapambano ya kimaisha.


Kama anavyo onekana amekatwa mikono Mwezi wa 4 mwaka 2010 baada ya kupata ajili ya kuungua na moto alipoangukia jikoni kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Kifafa uliompata wakati huo akiwa mfanyakazi wa Kampuni ya CONSO UNITED  LTD yenye makao makuu yake katika eneo la Bandarini Mtaa wa Kurasini Shimo la Udongo Jijini Dar es Salaam.


Baada ya kupatwa na ajali hiyo ambayo pia ilimsababishia kupoteza viungo vya Uzazi ambavyo pia viliondolewa pamoja na Mikono hiyo na wataalamu wa Hospitali inayotoa huduma kwa wagonjwa wanaofanya kazi katika Mgodi wa machimbo ya Shaba nchini Zambia.


Anasema mkasa huo ulimpata wakati wakiwa katika eneo la Kasumbaalesi katika mpaka wa Nchi za Congo na Zambia wakati huo akiwa msaidizi wa Shughuli mbalimbali (UTINGO) katika Gari aina ya International mali ya kampuni hiyo ambalo lilikuwa likiendeshwa na Dereva aliyemtaja kwa jina la  Yusuph Baisi ambaye pia toka wakati huo walipoteana na hajui aliko.


Alisema kinacho muumiza zaidi ni Viongozi wa kampuni hiyo kumtelekeza na kukiuka ahadi waliyo muahidi wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mgodi huo  na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nchi Tanzania ambako alihamishiwa kwa matibabu kuwa wangemghalamia kwa kumnunulia viungo Bandia.


Alisema ndoto za kupatiwa viungo hivyo  zilianza kuyeyuka baada ya viongozi wa kampuni hiyo kumkana kuwa hawakuwa wamemujiri kufanya kazi hiyo kwa madai kuwa aliyekuwa amemtafuta ni Dereva wa gari hilo hivyo hawawezi kuwajibika kwa lolote na hata huduma waliyo itoa kwake zilikuwa ni fadhila la huruma yao tu.


Huku akibubujikwa na machozi kwa uchungu  Mohamedi aliendelea kueleza kuwa kinacho muuma zaidi ni kitendo cha Viongozi hao ambao baadae pia walianza kumkejeli kuwa akiona vipi anywe hata sumu ya panya na kujiua iliasiendelee kuteseka na maisha hayo . 


Kijana huyo ambaye kwa sasa amepata kilema hicho  cha maisha kimemtia katika maisha ya kuwa ombaomba katika mitaa ya Mji wa Tunduru, Anasema kuwa hali hiyo inamfadhaisha na imemfanya pia akimbiwe na Mkewe Mpendwa Amida Mnayahe na kumuachia Mtoto wa Kiume aliye mtaja kwa jina la Rajae Mohamed anayesoma darasa la 2 ambaye pia anashindwa kumuhudumia kwa chakula,nguo  na kumsomesha.


Kwa aliyeguswa anaombwa kumtuma mchango wake kupitia namba yake ambayo ni 0765-956-264