Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Ndugu. Adam H. Mayingu tuzo ya kuwa Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii Tanzania kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake. Tuzo hiyo ilitolewa kwenye maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Mifuko ya Jamii mjini Dodoma. Mh. Raisi alisema PSPF ni mfuko madhubuti na una fursa nyingi za kimaendeleo kwa wananchi wa Tanzaniai na unauwezo mkubwa na salama katika uwekezaji . Aliongezea kwa kusema sio kweli kwamba Mfuko huu uko mahututi kama ilivyozungumziwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari, bali Mfuko huu unadai wadai wake Trilioni 6 na kudai sio kufilisika tena
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akisoma kipeperushi cha nyumba za PSPF zinazokopeshwa kwa wanachama wa Mfuko huo, huku akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo ndugu Adam H. Mayingu akimuelezea kuhusu nyumba hizo na fursa zingine zilizopo PSPF kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na ujumbe kwa Watanzania kwamba mtu yeyote mwenye umri usiopungua miaka 18 anaweza kuwa mwanachama wa PSPF
Mtangazaji
wa TBC Amina Mollel akikabidhi fomu ya kujiunga na PSPF kwa Meneja
Masoko wa Mfuko huo Bi. Costantina Martin mala baada ya kuvutiwa na
kukata shauri ya kuwa mwanachama wa Mfuko wa kwa njia ya uchangiaji wa
hiari
Timu ya
PSPF iliyokuwa kwenye maonyesho ya wiki ya hifadhi ya Jamii wakiwa na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wao ndugu Adamu Mayingu katikati. Timu hiyo
inastahili pongezi kutokana na uduma bora waliyokuwa wakiitoa kwa
wananchi waliokuwa wakitembelea banda hilo la PSPF pale Nyerere squire
Dodoma.