Friday, May 10, 2013

Misamaha Itolewe kwa Wahusika – Serikali

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi

Na Magreth Kinabo – Maelezo, Dodoma


SERIKALI
imewaagiza watendaji na wananchi kupitia kamati zao za afya kuhakikisha misamaha inatolewa kwa wote wanaostahili. Aidha imesema kuwa kituo ambacho hakifanyi vizuri katika ukusanyaji na udhibiti wa matumizi ya fedha zinazotokana na huduma kwa wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), viongozi husika wapewe onyo. Baada ya muda watakaopewa iwapo hakuna mabadiliko zichukuliwe hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuondolewa madaraka waliyopewa.
 
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi wakati akifungua mkutano wa mkutano mkuu wa mwaka wa waganga wakuu wa mikoa, wilaya na baadhi wa wakurungezi wa hospitali za rufaa na taasisi za wizara hiyo wakiwemo wakurugnezi wa asasi za kiraia, wadau wa maendeleo na washiriki kutoka  Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mkutano huo wa siku tatu umefanyik katika  ukumbi wa mikutano wa St. Gasper mjini Dodoma.
“Mwongozo wa Serikali kuhusu sera ya ucahangiajia wa huduma za afya nchini unajulikana. 

Lakini kuna vituo ambavyo bado vinaendelea kutoza gharama za uchangiaji wa huduma, kwa makundi ya watu ambayo sera inaelekeza huduma zitolewe bila malipo. Wizara imekuwa ikilamzimika kujibu malalamiko mengi kuhusu vituo ambavyo havitekelezi maelezo hayo, Nimeambiwa kuwa katika ukusanayaji wa fedha zinazotokana na kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF, vituo binafsi vinaongoza kupata fedha nyingi kuliko umaa pamoja na ukweli kwamba wana wagonjwa wachache wanaohudumia. Naamini tunajua sababu” alisema Dk. Mwinyi.

Hata hivyo alisema wongozo huo unapitiwa ili uendane na mahitaji ya kisasa.
“Tunajua umuhimu wa vituo vyetu kuwa fedha za kutosha kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi. hivyo sisi viongozi lazima tutumie njia zote halali za kupata fedha, pia tuweke usimamizi madhubuti wa kukusanya na kutumia fedha hizo, endapo hakutakuwa na udhibiti imara uboresahji wa huduma hautakuwepo hata kama kuna fedha nyingi,” alissitiza.

Alisema kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Usimamizi Bora wa Utendajia Kazi ndiyo nguzo Kuu katika utoaji wa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii’. Hivyo changamoto nyingi zinazojitokeza katika huduma za afya zinaweza kuondolewa na usimamizi na ufuatiliaji wa utendaji kazi wa walio chini.

Dk. Mwinyi aliongeza kuwa tatizo la upungufu wa watumishi katika vituo vya huduma za afya bado lipo. Idadi ya watumishi hao waliopo hadio kufikia Aprili mwaka 2013ni 64,449, ambayo ni asilimia 47 ya wanaohitajika katika vituo hivyo. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk. Rufaro Chatora alisema anampongeza waziri huyo kwa kujibu hojan kwa umahiri na kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo. Aliongeza kuwa changamoto za kiafya zinazoikabili nchi ya Tanzania, pia kwa nyingine duniani. Hivyo rasilimali kila siku hazitoshelezi, kinachotakiwa ni kuendelea kuboresha huduma hizo.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Regina Kikuli alisema mkutano hu unatoa fursa ya kujadiliana namna ya kuboresha huduma hizo. Awali akiwakarisha wageni hao katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rehema Nchimbi alisema mkoa wake umefanikiwa kutekeleza mpango wa chanjo.

Wakati huo huo SERIKALI
imesema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni lazima kwa kila mtu ili kupunguza matatizo ya uhaba wa fedha kwa ajili ya matibabu huduma zaa afya. Aidha ifafanua kuwa ifikapo mwaka 2015 bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itakuwa imefikia asilimia 15.

Kauli hiyo ilitolewa  na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi wakati jana jioni mjini Dodoma, alipokuwa akihitimisha mjadala wa kuhusu Makadrio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2013/2014 ya sh. 753,856,475,000, kati ya fedha hizo sh. 282,573,534,000 ni kwa ajili ya mtumizi ya kawaida na sh. 471,282,941,000. ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Alisema serikali ina mpango wa kuongeza wigo wa huduma ya mfumo huo, hivyo utakuwa si hiari. Alisema Serikali ina mpango wa kuwa na Sheria Mpya ya ‘National Social Health Insurance’, ambapo kila mtu atakuwa na bima hiyo ili kupunguza matatizo katika sekta ya afya. Dk. Alisema lengo la serikali ni kupanua mfuko huo.

Akijibu hoja ya baadhi ya wabunge kuwa bajeti ya maendeleo inaonekana kuwa ni tegemezi, Waziri huyo alisema ni kwa sababu wadau wa maendeleo wanaonesha kuchangia fedha nyingi katika eneo hio, hivyo fedha nyingi zinawekwa katika maeneo mengine.

Chanzo:www.thehabari.com