Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa mkutano wa wawekezaji wa sekta
binafsi (CEO Round
Table Dinner) uliofanyika
juzi usiku katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski.
Na
Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana amesema ubinafsishaji
haujafanikiwa vizuri kwani tangu sera hiyo ianze nchini kuna viwanda havifanyi
kazi wala kutoa ajira kama ilivyokusudiwa na hivyo serikali ya Chama cha
Mapinduzi inahitaji wawekezaji wa sekta binafsi katika kuboresha huduma katika
reli, barabara na viwanja vya ndege.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari, pamoja na wawekezaji wa sekta binafsi katika
mkutano ulifanyika juzi usiku katika hoteli ya Kilimanjaro
Kempiski.
Sera ya CCM
ipo wazi, tunawahitaji wawekezaji wa sekta binafsi na tumekuwa tukiwahitaji
tangu siku zote, lazima kwanza tutambue uwepo wao ili tuweze kuwashirikisha
katika sekta ya kusaidia jamii katika hhudma za jamii
Katibu Mkuu
wa Chama cha Mapinduzi amezungumza na wawekezaji wa sekta binafsi, mwezi mmoja
tangu katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) naye kuzungumza
na wawekezaji hao. Wakurugenzi hao hukutana na vyama mbalimbali kujua sera zao
vyama na ushirikiano wao na sekta binafsi nchini.
Credits: Habarimseto blog