Kufuatia
wito wa rais Jakaya Kikwete kwa marais wa mataifa ya maziwa Makuu marais
Paul Kagame, wa Rwanda, Joseph Kabila wa jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo na Yoweri Museveni wa Uganda, kuzungumza na makundi ya waasi
yanayopambana na nchi zao, wabunge wa Kongo Kwenye taarifa yao ya pamoja
iliyosomwa na mbunge Benjamin Mukulungu , wabunge hao wa Kivu Kusini na
Kaskazini wameomba kuwe na mtazamo wa jumla wa viongozi wa kanda ya
maziwa makuu na umoja wa mataifa ili kumaliza vita nchini CongWabunge wa
Kivu wamepongeza msimamo wa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wa kutaka
kuwe na mazungumzo kati ya serikali za Congo Rwanda na Uganda na makundi
ya waasi wanayopingana nayWabunge wa Kivu wametaka pendekezo la Rais
Kikwete ni lazima lipewe kipaumbele na jumuiya ya kimataifa ili kuwe na
amani ya kudumu kwenye eneo hilo.Mbunge wa upinzani Emerio Kunji kutoka
jimbo la Kasai amesema amepanga kutoa hoja rasmi bungeni ili kuweko na
azimio la bunge kuhusu msimamo ambao serikali ya Congo inatakiwa
kuchukua kwa ajili ya kutatua mzozo wa Kivu
Friday, May 31, 2013
Mrehemu Ernest Zulu azikwa Maposeni Songea
MWILI wa marehemu
aliyekuwa mwandishi wa vikao vya Bunge la Tanzania
Ernest Zulu umezikwa katika makaburi ya kichifu yaliyopo Maposeni Peramiho
wilayani Songea mkoani Ruvuma huku mazishi
hayo yakifanyika bila kuhudhuriwa na familia yake jambo ambalo liliwashangaza
baadhi ya watu waliohudhuria mazishi hayo.
Wakiongea kwa sauti za chini kwenye mazishi
hayo baadhi ya wakazi wa Peramiho walisema kuwa wameshangazwa kuona wasifu wa
marehemu ukisomwa na kuonyesha kuwa marehemu amewaacha watoto wanne na mke
mmoja lakini cha ajabu hawaonekani kwenye msiba huo.
Kwa
upande wake kaka wa marehemu chifu Emmanuel
Zulu akiwashukuru mamia ya watu walioshiriki kwenye mazishi hayo akiwemo akiwemo
Mbunge aliyetumwa na bunge la jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuja kuwakilisha mazishi hayo Abdukalim Shaha
wa jimbo la Mafia Zanzibar
alisema kuwa yeye hana cha zaidi ya
kumshukuru Mungu aliyetenda mambo hayo.
Aidha kwa upande wake Mbunge Abdukalim Shaha
akitoa salaamu za bunge amewataka viongozi wa dini zote kuendelea kujenga
mshikamano wa kuliombea taifa lisiingie kwenye machafuko maana amani ikitoweka
hakuna atakayekuwa huru kwa kufanya kazi zake.
Alisema kuwa marehemu Ernest Zulu
alitokea katika familia ya kichifu lakini kafanya mambo mazuri mengi katika
taifa kwa sababu wazazi wake walikuwa wakihimiza amani na utulivu vidumu siku
zote na siyo vinginevyo hivyo jamii inapaswa kuiga na kuendeleza moyo huo wa
uzalendo.
Alisema kuwa hali ya sasa inayojitokeza katika vikao vya bunge kwa
baadhi ya viongozi kutaka kushikana mwilini hivyo ni vyema jamiin kwa ujumla ikasaidiana
kumuomba Mungu aweze kuepusha balaa hasa kwa kuwakemea vijana waachane na
ushabiki usiyokuwa wa msingi.
Hata hivyo aliipongeza ofisi ya mkuu wa wilaya
ya Songea kwa kazi nzuri ya kufanikisha maandalizi ya mazishi hayo kwa
kuwapokea wageni na kufanikisha kuwapa huduma na kuwa hiyo wanaenda kuiweka
kwenye rekodi ya ofisi ya Mbunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Lakini pamoja na wakazi hao kuhudhuria
kwenye mazishi hayo wakiwemo viongozi wa safari ya mwisho ya Ernest Zulu lakini
wananchi hao walionyeshwa kutoridhika kwa kutokuwepo Mbunge hata mmoja wa
mkoani hapo zaidi ya wawakilishi.
VIA/ demashonews
Thursday, May 30, 2013
Kampuni ya usambazaji mbegu ya PANNAR SEED kanada ya kusini yatoa jezi 28 na mipira 5 kwa Timu za vijijini Songea
Meneja
wa kanda ya kusini Torio Mafie toka kushoto kwako akiwa ameshikilia
mpira pamoja na jezi wakati akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Songea jana
ofini kwake.
............................................
Hii ni baaada ya kukamilika kwa msimu wa mavuno kwa wakulima
wa wilaya ya SONGEA mkoani RUVUMA sasa kampuni ya usambazaji mbegu ya PANNAR
SEED kanda ya nyanda za juu kusini imetoa vifaa vya michezo wa soka kwa
wakulima ili kufufua michezo wakati wakiwa waanajiandaa kwa msimu mwingine
wa kilimo.
Kampuni ya PANNAR SEED imetoa jezi 28 na mipira
mitano vyenye thamani ya shilingi milioni 2 na laki moja ambapo MENEJA WA KANDA
YA KUSINI TORIO MAFIE amesema msaada huo waliotoa ni ishara kuwa wapo pamoja na
wakulima ili kuwapa vijana shughuli mbadala wakati wa mapumziko
ya msimu wa kilimo
Mkuu wa wilaya ya
SONGEA JOSEPH MKIRIKITI Akipokea
jezi na mipira kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya
PANNAR SEED
PANNAR SEED
Mkuu wa wilaya ya
SONGEA JOSEPH MKIRIKITI akitabasamu kwa furaha baada ya wakulima kuwezeshwa vifaa vya michezo ,
Hataa hivyo kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya SONGEA
amesema bado mahitaji ya vifaa vya michezo ni makubwa hivyo ameziomba kampuni
mbalimbali zinazojihusisha na shughuli za kiuchumi na kijamii wajitokeze
kufadhiri timu za vijiji wilayani hapa
SIKU YA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA KUMI NA SABA(17) YA WIKI YA MAZIWA SONGEA-RUVUMA YAFANA
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA SAID MWAMBUNGU amezindua maadhimisho ya 17 ya wiki ya maziwa nchini na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kunywa maziwa kwa wingi kwa lengo la kuboresha afya zao
Akizungumza na wananchi na wadau wa maziwa katika viwanja
vya manispaa ya SONGEA MWAMBUNGU alisema
kati ya lita bilioni 1.6 za maziwa zinazozalishwa hapa nchi kwa mwaka ni
wastani wa lita 11.6 tu zinazonywewa na mtu mmoja wa mkoa wa Ruvuma kiasi
ambacho ni kidogo ukilinganisha na viwango vya kimataifa vya lita 200 kwa mtu
kwa mwaka.
Maadimisho
hayo ya wiki ya maziwa ambayo yanafanyika kwa mara
ya kwanza mkoaniMkoani Ruvuma ambapo MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID
MWAMBUNGU aliwaamasisha wananchi wa mkoa wake kuongeza kasi ya unywaji
wa maziwa
sambamba na kufuga ng’ombe wa kisasa wanaotoa maziwa mengi badala ya
ng’ombe wa
asili ambao uzalishaji wao ni mdogo.
Maadhimisho haya yameambatana na maonyesho ya bidhaa
mbalimbali za maziwa pamoja utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa
unywaji maziwa, usindikaji na uzalishaji wake hata hivyo baadhi ya wadau wa maziwa kutoka vyama
vya usindikaji maziwa wamesema maziwa mengi yanayozalishwa hapa nchini
yanashindwa kuwafikia wanywaji kutokana na asilimia chache zinazosindikwa.
Wiki ya maziwa iliyozinduliwa leo mkoani hapa
itaendelea kwa siku nne zijazo ambapo hapo kesho madereva wa pikipiki maarufu
kama YEBOYEBO, wafungwa na wagonjwa hospitalini watagawiwa maziwa ya bure kama
sehemu ya uhamasishaji
Tuesday, May 28, 2013
Kinana: Akemea wanaowania urais 2015
Kinana (katikati)
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama kitamwadhibu bila
huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo mbalimbali
na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.Kinana alisema hayo jana wakati akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum, kilichofanyika kabla ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya siku saba mkoani humo.
Kinana alisema, katazo la wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au nafasi yoyote kabla ya muda halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.
"Ndugu zanguni, nawakumbusha kwamba kwa hili hatuna mzaha nalo, hivyo hakikisheni kila mmoja wenu kama kiongozi hajihusishi kwa namna yoyote kushiriki katika kutumiwa na wanachama hao wanaojipitishajiptisha", alisema Kinana na kuongeza;
"Ni lazima Chama kiwe kikali kwenye jambo hili, kwa sababu kama kitawaacha watu hawa kukiuka taratibu na kanunzi za Chama wanazidi kukifanya chama kuwa na makundi mengi ambayo yatakipeleka pabaya," alisema Kinana
Kinana alisema, kazi walioyonayo wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia.
Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
"Ni wazi kazi yatu CCM ni kuhakikisha tunatekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si mamneno kama wanavyofanya wengine. ni kazi kubwa imefanyika chini ya uongozi wa Rais Kikwete na katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki tumedhamiria kuifanya zaidi",
Alisema moja ya maeneo ambayo licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana utekelezaji wa ilani ya CCM, ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi.
"Kwa kweli CCM lazima hawa tuwapongeze maana kuna wengine kazi yao imebaki kuwashambulia huku wakijua watendaji hao hawana fursa ya kujitete mbele ya jamii. chapeni kazi nasi tupo nyuma yenu, na kila wakati tutakuwa tukitambua juhudi na kazi kubwa mnayoifanya kwa jamii," alisema Kinana.
Chanzo: Bashir Nkoromo
Mama aliyejifungua watoto watano aruhusiwa kutoka hospitali baada ya kuomba
Bi Sophia Mgaya aliyekaa kitandani akiwa amebeba mmoja wa wawatoto
watano aliowazaa kabla ya watototo hao kufa wote(Picha na maktaba)
Hawa ndio watoto aliojifungua katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na kesho wakafaliki dunia (Picha na maktaba)
..........................................................................
Na Nathan Mtega,Songea
MWALIMU Sophia
Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma aliyejifungua watoto
watano kwa wakati mmoja kwa njia ya upasuaji mnamo Mei 25 mwaka huu katika
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo
mjini Songea na watoto hao kuishi kwa muda wa masaa kumi kabla hawajafariki
dunia ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.
Akizungumza na Demashonews kwa njia ya simu Sophia Mgaya akiwa nyumbani kwake Ruhuwiko mjini
Songea alisema alilazimika kuomba kutoka wodini kwa sababu alikuwa akijisikia
uchungu anapowaona wanawake wenzake wodini humo wakiwakumbatia watoto wao baada
ya kujifungua huku wa kwake wote wakiwa wamefariki dunia baada ya kuzaliwa.
Alisema kuwa muda
wote aliokuwa hospitalini hapo baada ya watoto wake kufariki huku akiwa bado
anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa alikuwa akilia muda wote anapowaona
wanawake wenzake waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao hivyo
akaamua kuomba aruhusiwe kutoka hospitalini hapo.
‘’Niliomba
kuruhusiwa kutoka hospitali na kwenda kujiuguza kidonda nyumbani kwa sababu ya
uchungu na majonzi niiiyokuwa nikiyapata wodini hapo ninapowaona wanawake
wenzangu waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao huku wa
kwangu wakiwa wameshazikwa”alisema Bi.Mgaya
Aidha aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo pamoja na
wafanyakazi wote kwa namna walivyomuhudumia yeye pamoja na watoto wake watano
waliozaliwa na kuishi kwa muda wa masaa ya kumi ambapo alisema kuwa yote
yaliyotokea anaamini kuwa ni mapenzi ya Mungu.
Mganga Mkuu mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma
Dkt.Benedict Ngaiza akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu kuwa waliamua
kuridhia ombi la mama huyo kuondoka hospitalini hapo baada ya kujiridhisha kuwa
anaendelea vizuri kwa sababu walifanya kila walichoweza kukoa uhai wake na
watoto lakini watoto walifariki baada ya masaa kumi.
Wakizungumza baadhi
ya wananchi waliomshuhudia mama huyo na watoto wake baada ya kuzaliwa na kabla hawajafariki walisema kuwa kuna kila
sababu kwa kila mwenye uwezo wa kumsaidia mama huyo kwa namna yoyote afanye
hivyo
Bi.Marietha Ngonyani
na Lusi Haule wakazi wa mjini Songea waliwaomba wananchi mbali mbali kujitolea
kumsaidia mama huyo kwa sababu bado anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa
na pia tukio hilo
limemuathiri kisaikolojia pia hivyo anahitaji faraja.
VIA/ www.demashonews.blogspot.com
RAIS DKT. KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI ADDIS ABABA, ETHIOPIA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri
Mohamed Morsi walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addis Ababa, Ethiopia
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri
Mohamed Morsi walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addis Ababa, Ethiopia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) professor Ntumba Luaba na ujumbe wake walipokutana
na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addis Ababa, Ethiopia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller walipokutana
na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addis Ababa, Ethiopia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller walipokutana
na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addis Ababa, Ethiopia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Waziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller walipokutana
na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addis Ababa, Ethiopia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulishaWaziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller kwa Mhe Gideon Moi, Seneta wa Kaunti ya Baringo nchini kenya na ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha KANU cha nchi hiyo walipokutana
pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa
Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa,
Ethiopia.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya
Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa
Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani Mh Liberata Mulamula
walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya
Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa
taaisi ya kimataifa inayoshughulikia mapambano dhidi ya Ukimwei, Kifua
Kikuu na Malaria ya The Global Fund Dkt Mark Dybil na afisa wa taasisi hiyo Bi Shu-shu Tekle-Haimanot walipokutana
na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addis Ababa, Ethiopia
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Mkurugenzi Mtendaji
wa UNAIDS Michel Sidibe walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya
mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU)
katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel
Sidibe pamoja na Mratibu wa Masuala ya Ukimwi wa Marekani Balozi Eric
Goosby walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe
za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya
Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia
WADAU JITOKEZENI KUDHAMINI UHURU MARATHON!!
Katibu
mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania, Seleman Nyambui akiongea katika
mkutano na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa wadhamini wa Uhuru
Marathon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni mkurugenzi wa
Kampuni ya Intellectuals ambao ndiyo waandaaji wa mbio hizo, Innocent
Melleck.
MKurugenzi
wa Kampuni ya Intellectuals ambao ndiyo waandaaji wa mbio hizo,
Innocent Melleck akiongea katika mkutano na waandishi wa habari wakati
wa ufunguzi wa wadhamini wa Uhuru Marathon iliyofanyika leo jijini Dar
es Salaam. Pembeni ni Katibu mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania, Seleman
Nyambui.
Waandishi
wa Habari waliohudhuria mkutano huo wakiwajibika wakati wa ufunguzi wa
wadhamini wa Uhuru Marathon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
WAKATI
mbio zinazosubiriwa kwa hamu kubwa na watu wengi hapa nchini za Uhuru
Marathon zikitarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu, waratibu wa mbio hizo
wamezitaka kampuni, taasisi au watu binafasi wanaotaka kuzidhamini
wafanye hivyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni
ya Intellectuals walio waandaaji wa mbio hizo, Innocent Melleck alisema
wameamua kufungua milango ya udhamini, ili ziweze kufana zaidi.
Melleck
alisema, wanariadha wengi kutoka ndani na nje ya nchi wameonyesha nia
ya kushiriki mbio hizo zitakazokuwa zikifanyika kila Desemba
zikiambatana na maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanzania Bara, hivyo
wameona ni bora wafungue milango kwa wadhamini.
“Nadhani
wote mnakumbuka uzinduzi wa mbio hizi za Uhuru, uliofanyika Desemba
mwaka Jana, ukiwa unaashiria kuanza kwa mchakato wa maandalizi ya mbio
zenyewe ambazo zitaanza kufanyika Desemba mwaka huu.
“Mbio
hizi za Uhuru, kama lilivyo jina lake zimeanzishwa ili kuongeza chachu
kwa Watanzania kuwa na moyo wa kulinda amani, umoja na mshikamano wetu.
“Kwa
sasa maandalizi ya awali yanaendelea vizuri, nasi tumeona huu ni muda
muafaka kufungua milango ya udhamini kwa makampuni, mashirika na taasisi
mbalimbali ambazo zitahitaji kushirikiana nasi katika kufanikisha mbio
hizi wajitokeze na kupata taratibu za udhamini,” alisema Melleck.
Alisema
kutakuwa na mbio ndefu za kilomita 42, mbio za kati za kilomita 21 na
zile za kujifurahisha za kilomita 5, hivyo mdhamini anaweza kuchagua
aina ya mbio anazotaka kuzidhamini.
Naye
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui
alisema, tayari kwa upande wao wamekamilisha vitu vingi ikiwemo
kupendekeza mzunguko wa mbio hizo na kuangalia mambo yote ya kiufundi.
“Tunawaomba wadhamini wajitokeze ili kwa pamoja tuweze kufanikisha mbio hizi zenye malengo mazuri kwa Taifa letu kwa ujumla.
“Mbio
hizi tutazisimamia na kuziendesha katika hadhi ya kimataifa ili
kuhakikisha kuwa zaidi ya kulinda Amani na Umoja wetu, pia tunalitangaza
taifa letu kote ulimwenguni.
“Kwa
kuwa mimi ninaangalia zaidi upande wa ufundi, nichukue nafasi hii pia
kuwasihi wanariadha wa hapa nchini kuanza maandalizi ya mbio hizi,
itakuwa si vyema nafasi za juu zikichukuliwa na wageni, wakati sisi
tunao wanariadha wazuri hapa nyumbani,” alisema.
Uhuru
Marathon ni moja kati ya mbio zinazotarajiwa kuleta mapinduzi mapya
katika riadha, ikiwa pamoja na kukumbusha umuhimu wa kutunza na kulinda
amani tuliyonayo.
Taswira Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa:Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe Ashiriki Maandamano ya kuadhimisha miaka 50 OAU/AU Jijini Dar es Salaam Nakusema :'' Umoja wa Afrika (OAU/AU) umepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mjini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 25 Mei, 1963''.
"Brass Band" ikiongoza maandamano
kutokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuelekea
Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 OAU/AU.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akimkabidhi Mkuu wa Mabalozi
na Balozi wa DRC hapa nchini, Mhe. Juma Khalfan Mpango Mwenge wa Umoja
wa Afrika (OAU/AU) kuashiria kuanza kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja
huo yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam
Picha zaidi za maandamano.
Mhe. Membe akishiriki maandamano hayo.
Mhe. Membe, Mabalozi, wananchi na wageni waalikwa wakiwa katika maandamano hayo kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika
Mhe. Membe akisikiliza Wimbo wa Taifa na AU zilizopigwa kuadhimisha miaka 50 ya umoja huo
Picha zaidi wakati wa wimbo wa Taifa
Mhe. Membe, Mabalozi, na Viongozi wengine wakiangalia burudani kutoka
vikundi mbalimbali vya utamaduni vilivyopamba maadhimisho hayo
Burudani ikiendelea.
Kikundi kingine cha burudani kilichopamba sherehe hizo.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
--
Na Ally Kondo
Umoja wa Afrika (OAU/AU) umepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mjini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 25 Mei, 1963.
Hayo yalisemwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.
Membe (Mb) katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja huo
iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam tarehe 25 Mei,
2013.
Mhe. Membe alieleza
kuwa, AU imefanikiwa kutimiza lengo la kuzikomboa nchi zote za Bara la
Afrika isipokuwa Saharawi kutoka katika tawala za kikoloni. Alisema
katika kufanikisha hilo, Tanzania imechangia kwa kiasi kikubwa kwani,
Makao Makuu ya Ukombozi ya AU yalikuwa hapa nchini.
Kuhusu Demokrasia na
Utawala Bora katika nchi za Afrika, Mhe. Waziri alisema kuwa AU imeweka
utaratibu mzuri wa kuhakikisha kuwa wanachama wake wanaheshimu utawala
wa sheria kwa kuweka sheria kali za kukomesha tabia ya kuingia
madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi. Sheria hizo ni pamoja na;
nchi inayotawaliwa kijeshi kusimamishwa uanachama wa AU, kuwekewa
vikwazo vya kiuchumi pamoja na Kiongozi wa Mapinduzi kutoruhusiwa
kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi wa kidemokrasia.
Kutokana na msimamo
huo, AU imefanikiwa kupunguza matukio ya mapinduzi katika nchi za Afrika
tangu ilipoanzishwa. “Afrika imeshuhudia matukio ya mapinduzi matano
katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ukilinganisha na matukio 34
yaliyotokea kabla ya kipindi hicho”. Mhe. Membe alisikika akisema.
Katika kukabiliana na
migogoro inayozuka mara kwa mara katika nchi za Afrika, alisema kuwa, AU
imebadilisha kipengele ambacho kilikuwa kinakataza nchi za Afrika
kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine. Hivyo, kutokana na
mabadiliko hayo nchi za Afrika sasa zinaweza kuingia katika nchi
nyingine kulinda amani.
Kwa upande wa
maendeleo ya kiuchumi, Mhe. Waziri alisema kuwa hatua kubwa imefikiwa,
hususan kupitia Jumuiya za Kiuchumi za Kikanda, kama vile SADC, EAC na
ECOWAS. Hata hivyo alibainisha kuwa, ukosefu wa miundombinu imara kama
barabra na reli, kuunganisha Bara zima la Afrika ni kikwazo katika
kufikia malengo ya kiuchumi kwa nchi nyingi za Afrika.
Sherehe za kuadhimisha
miaka 50 ya Umoja wa Afrika (OAU/AU) zilipambwa na shughuli mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuwasha mwenge wa AU, maandamano na burudani kutoka
vikundi mbalimbali vya utamaduni. Aidha, sherehe hizo zilihudhuriwa na
Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimatafa hapa nchini, wanafunzi
na wananchi.
Monday, May 27, 2013
BREAKING NEWS: WATU NANE WAFALIKI DUNIA NA WENGINE KUMI NA MOJA MAJELUHI KATIKA AJALI YA GARI - NAMTUMBO
Hili ndilo lori lililopata ajali katika kijiji cha Hanga
..............................................
Watu
nane wamefariki dunia baada ya gari
walilokuwa wanasafiria kutoka kijiji cha mputa wilaya ya Namtumbo kwenda Songea
kuacha njia na kupinduka katika kijiji
cha Hanga eneo la Bombambili wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma .
Roli hilo lilikuwa limebeba magunia ya ufuta, mpunga wakiwemo na abiria
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit
Nsimeki amesema ajali hiyo imetokea jana Tarehe
26.05.2013 majira ya saa nne na nusu( 4:30 usiku katika kijiji cha Hanga eneo la
bombambili mkoa wa Ruvuma, chanzo cha
ajili hiyo ni mwendokasi na dereva kuendesha gari akiwa amelewa,
Ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za usajili T.677 ADL aina ya Isuzu lori , mali ya mfanyabiashara wa
mazao maarufu kwa jina la Mtazamo. likiendeshwa na dereva aitwae CHRISTIN
NYONI mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa LIHULI
SONGEA,
Baada ya ajali
hiyo kutokea dereva wa gari hilo amekimbia na kutelekeza gari porini
hadi sasa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya jitihada za kumtafuta
ili sheria ifuate mkondo wake.
Kamanda
wa Polisi amesema gari hilo liliacha njia baada ya kugonga daraja na
kupinduka na kusababisha vifo vya watu nane(8) na majeruhi kumi na moja (11) ambao
wote
wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.
Kutokana
na ajali hiyo mbaya kamanda wa polisi
wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki
ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya mizigo kutopakia mazao pamoja na abiria
na atakayekiuka atachukiliwa hatua kali za kisheria.
Pia ametoa wito kwa wamiliki/wasimamizi wa
magari kuwa wanatakiwa kuhakikisha magari ya mizigo,mazao hayapakii abiria na
atakaye kiuka agizo hili hatafikishwa mahakamani mala moja
ambapo
Sunday, May 26, 2013
Huu ni Msimu wa viazi vitamu Songea. Rambo moja buku mbili tuuuuuuuu!!!!!!!
Kandokando mwa barabara kuu ya Songea kwenda Njombe Vijiji vya Mtyangimbole, Hanga, Mlilayoyo hadi Madaba, Viazi vitamu kibao, buku zako mbili unabeba rambo nzima ya viazi. Songea maisha tambalale!!!!!
Vitamu hivyo balaaaaaaaa!!!!
Akina dada hujipatia ajira wakati huu ya kuuza viazi kandokando mwa Barabara
Leta buku mbili nikuachie
Subscribe to:
Posts (Atom)