Timu
ya Maji Maji songea kesho inaingia katika kinyang'anyilo cha uchaguzi
wa viongozi huyo hapo ni Humphery Millanzi mgombea nafasi ya mwekiti
katika timu ya Maji Maji akimwaga sela zake leo katika mdahalo
uliofanyika leo hii jioni majira ya saa kumi katika Radio Jogoo kwa
kushirikiana na Demashonews.blogspot.com, Moja ya ahadi zake ni
kuhakikisha timu ya Maji Maji inapanda daraja , kuhakikisha timu inakuwa
na wanachama hai na wakudumu kwa kuandaa mikutanao na kunadi sela za
timu pia kuisaidia timu inakuwa na vyanzo vya pesa ili timu kuondokana
na omba omba vile vile timu kuwa kampuni. Ameendelea kusema kwa kipindi
hiki akiwa kiongozi wa mpito ameweza kuisaidia timu hadi kushika nafasi
ya pili wakati timu haina vyanzo vya mapato hivyo sasa atakuwa na tiba
mbadala katika kuiwezesha timu hiyo endapo atachaguliwa.
Toka
kushoto ni Shekhan Mzaina akiwa na Hilda Kapinga mgombea nafasi ya
ujumbe pia ni mmiliki wa timu ya Luwiko football Academy ya watoto chini
ya miaka kumi na saba ana aihidi kuifikisha timu ya Maji Maji mbali
sana akiwa kama mpenzi wa mpira wa miguu , huku akitolea mfano wakati
timu hiyo ilipoenda kucheza Mbeya na kufungwa bao 6 kutokana na
wachezaji kutokuwa na uwezo wa kifedha na kuwa na mazingira mabovu
Toka kulia kwako ni Salum Masamaki, Said Mangwe wagombea nafasi ya wajumbe na Mohamedi Issa mgombea nafasi ya Mwenyekiti.
Toka
kushoto ni Mohamed Mtika mgombea nafasi ya ujumbe akiwa na Hamphery
Millanzi mgombea nafasi ya mwenyekiti wakitafakali kwa kina juu ya sela
za wenzao walizokuwa wakitoa katika mdahalo uliokuwa ukiendelea katika
Studio za jogoo FM kwa kushirikiana na demashonews.blogspot.com
Toka
kushoto ni Mohamed Mtika mgombea nafasi ya wajumbe , Hamphery Millanzi
mgombea nafasi ya mwenyekiti, John Kabisana mgombea nafasi ya wajumbe na
Mohamed Issa mgombea nafasi ya mwenyekiti
Toka
kushoto ni mtangazi wa Radio Jogoo kipindi cha michezo Hosam Ulaya ,
Shekhan Mzaina na Hilda Kapinga mgombea nafasi ya wajumbe
Wagombea
uongozi katika Timu ya Maji Maji wakiandika maswali yaliyokuwa
yakiuliuzwa kwa njia ya simu na wasikilizaji kupitia Radio Jogoo
Baada ya kutoka katika mdahalo
Picha
ya pamoja toka kulia walio simama ni Hamphery Millanzi mgombea nafasi
ya mwenyekiti,Said Mangwe wagombea nafasi ya wajumbe,Mohamed Issa
mgombea nafasi ya mwenyekiti, Mchele, Tamimu Adamu mtangazaji wa Radio
Jogoo,Mohamed Mtika mgombea nafasi ya wajumbe,Salum Masamaki, John
Kabisana mgombea nafasi ya wajumbe na kuoka kulia kwa walio chuchumaa ni
Hilda Kapinga mgombe nafasi ya wajumbe, Shekhan Mzaina na Hosam Ulaya
Humphery Millanzi mgombea nafasi ya mwekiti akiteta jambo na Hilda Kapiga mgombea nafasi ya wajumbe.
Kesho
ndiyo siku ambayo itakwenda kuandika historia mpya katika timu ya Maji
Maji kwa kufanyika uchaguzi kuanzia saa saa nne asubuhi na leo ilikuwa
ni kujinadi kila mgombea kutoa sera zake mambo yote kesho