Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na wanachama wa CCM kata ya Elerai mara tu baada ya kuwasili kwenye kata hiyo..
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibadilishana jambo na
mmoja wa wanachama wakongwe wa kata ya Elerai kabla ya kuanza kwa
mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa Udiwani ya kata hiyo.
Mbunge wa Vijana mkoani Arusha , Ndugu Catherine Magige akihutubia
wakazi wa kata ya Elerai na kuwataka wakazi wa kata hiyo kutambua
thamani ya kura kwa kuichagua CCM.
Naibu Waziri wa Ardhi, Mhe. Goodluck Olemadeye akihutubia wakazi wa
kata ya Elerai na kuwaambia CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa
wakati na kila kilichoahidiwa Arusha kitafanyika.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa kiti cha
udiwani kata ya Elerai, Mwl.Emmanuel Laizer,na kuwaambia wana Arusha
muda wa kufanya maendeleo ni huu na CCM haina kazi nyingine zaidi ya
kuleta maendeleo Arusha.
Mgombea
wa kiti cha Udiwani kwa tiketi ya CCM, Mwalimu Emmanuel Laizer
akihutubia wakazi wa kata ya Elerai kwenye mkutano wa kufunga kampeni.
Bibi na mjukuu wake wakifuatilia kwa makini yale yanayosemwa na
viongozi wa CCM wakati wa kufunga kampeni za udiwani kata ya Elerai.
Mbunge
wa Vijana Arusha ,Ndugu Catherine Magige akisikiliza kwa makini sera za
mgombea wa udiwani wa kata ya Elerai ,Mwl. Emmanuel Laizer.
Mboya
akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwaelezea kuwa alipotea sana
kuishabikia Chadema na amewasihi wakazi wa kata hiyo kutofanya makosa
kama kweli wanataka maendeleo.