Monday, June 3, 2013

CLOUDS MEDIA GROUP YAJITOLEA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA KUTOKA NCHINI AFRIKA YA KUSINI KUJA NCHINI TANZANIA

    Barua inayoonyesha walioanza kuchangia msiba wa Ngwea.
Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
"Tumeamua kwa mikono miwili kushiriki katika msiba huu wa ndugu yetu Mangwea,” alisema kwa ufupi. Ngwea amepangwa kuletwa Tanzania kesho Jumamosi na kuagwa Jumapili, kabla ya kupelekwa mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yake.
---
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
 
KAMPUNI ya Clouds FM, imejitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kwa ajili ya kuutoa Afrika Kusini hadi Tanzania kwa ajili ya kuzikwa, ukiwa ni utaratibu unaoonyesha kuwa wadau wote wameamua kushirikiana katika suala hili.

Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, alithibitisha kuchukua uamuzi huo kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya nyota huyo wa Bongo Fleva.