Monday, June 3, 2013

Safari yangu ya Singapore na niliyoyakuta. Wadau mpoooooo!!!!!!!!



Hapo ni ndani ya Airport Dubai.

Bado Dubai Airport

Ukiwa unasafiri kuaga vizuri Muhimu

Haya sasa jiji la Singapore hilo hapo

Nimekutana na Wadau Hamis Mkotya wa Mtanzania na kaka yangu Chidaga niliyeachana nae siku nyingi akiwa ofisi ya Ardhi Manispaa ya Songea, Ruvuma. Joto nyuzi 38

Jamaa wamepamba mji wao hadi raha. Hapo ni jengo lenye picha ya Meli, nimeambiwa hata ndege zinatua hapo juu lakini bado nafanyia kazi ukweli juu ya hili

Nikiwa Airport Singapole

Jamaa kwa vikwangua anga ni noma.

Vikwangua Anga vinaendelea


Singapore.

Singapore iliasisiwa February 06, 1819 chini ya ukoloni, ikapata serikali Juni 03, 1959 na ilipata uhuru Agosti 31, 1963.

Jina hili la Singapore ni jina lenye asili ya Malaysia ambako linatamkwa Singapura. Maana ya Singapura ni Mji wa Simba yaani the Lion City.

Wakati wote huo Singapore ilikua ni nchi moja pamoja na Malaysia hadi Agosti 09, 1965 ilipojitenga rasmi na kuanzishwa kwa Jamhuri ya Singapore.

Nchi hii ina eneo dogo la ukubwa wa kilometa za Mraba 710 ambalo ni dogo pengine sawa na wilaya moja tu ya jiji la Dar es salaam. kulingana na sensa ya mwaka jana (2012) Singapore ina watu 5,312,400.

Nchi hii imepiga hatua kubwa katika maendeleo, bandari yake inatajwa kuwa bandari ya tano duniani kwa kuwa na shughuli nyingi za usafirishaji na upokeaji wa mizigo. Nchi hii pia imejizatiti katika shughuli za viwanda hasa katika uzalishaji wa bidhaa kama vile za kielectronic, nguo na utalii wa mapambo.

Kiuchumi pato la nchi hii yaani GDP lipo juu, mwaka jana ilirekodi pato la dola 327.555 bilioni na pia pato la mtu (per capita) 61.046.

Hii ni nchi ya visiwa na inaundwa na visiwa 63. Ipo kusini mashariki mwa Bara la Asia na asilimia 75 ya wananchi wake ni wachina na wanaobaki ni wahindi na wamalasia.

Kwa watanzania kuingia Singapore huhitaji kuwa na visa, lakini ni miongoni mwa majiji ambayo gharama za maisha zipo juu kwa sasa.

Siri kubwa ya mafanikio ya SINGAPORE ni watu wake kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kufuata taratibu za nchi, kuwepo utekelezaji makini wa mipango ya serikali unaotokana na watendaji na viongozi wa umma kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao