Saturday, June 29, 2013

KESHO NDIYO KESHO KWA TIMU YA MAJI MAJI - SONGEA

 Timu ya Maji Maji songea kesho inaingia katika kinyang'anyilo cha uchaguzi wa viongozi huyo hapo ni Humphery Millanzi mgombea nafasi ya mwekiti katika timu ya Maji Maji akimwaga sela zake leo katika mdahalo uliofanyika leo hii jioni majira ya saa kumi katika Radio Jogoo kwa kushirikiana na Demashonews.blogspot.com, Moja ya ahadi zake ni kuhakikisha timu ya Maji Maji inapanda daraja , kuhakikisha timu inakuwa na wanachama hai na wakudumu kwa kuandaa mikutanao na kunadi sela za timu pia kuisaidia timu inakuwa na vyanzo vya pesa ili timu kuondokana na omba omba vile vile timu kuwa kampuni. Ameendelea kusema kwa kipindi hiki akiwa kiongozi wa mpito ameweza kuisaidia timu hadi kushika nafasi ya pili wakati timu haina vyanzo vya mapato hivyo sasa atakuwa na tiba mbadala katika kuiwezesha timu hiyo endapo atachaguliwa.
Toka kushoto ni Shekhan Mzaina akiwa na Hilda Kapinga mgombea nafasi ya ujumbe pia ni mmiliki wa timu ya Luwiko football Academy ya watoto chini ya miaka kumi na saba ana aihidi kuifikisha timu ya Maji Maji mbali sana akiwa kama mpenzi wa mpira wa miguu , huku akitolea mfano wakati timu hiyo ilipoenda kucheza Mbeya na kufungwa bao 6 kutokana na wachezaji  kutokuwa na uwezo wa kifedha na kuwa na mazingira mabovu
 Toka kulia kwako ni Salum Masamaki, Said Mangwe wagombea nafasi ya wajumbe na Mohamedi Issa mgombea nafasi ya Mwenyekiti.
 Toka kushoto ni Mohamed Mtika mgombea nafasi ya ujumbe akiwa na Hamphery Millanzi mgombea nafasi ya mwenyekiti wakitafakali kwa kina juu ya sela za wenzao walizokuwa wakitoa katika mdahalo uliokuwa ukiendelea katika Studio za jogoo FM kwa kushirikiana na demashonews.blogspot.com
 Toka kushoto ni Mohamed Mtika mgombea nafasi ya wajumbe , Hamphery Millanzi mgombea nafasi ya mwenyekiti, John Kabisana mgombea nafasi ya wajumbe na Mohamed Issa mgombea nafasi ya mwenyekiti

Toka kushoto ni mtangazi wa Radio Jogoo kipindi cha michezo Hosam Ulaya , Shekhan Mzaina na Hilda Kapinga mgombea nafasi ya wajumbe
 Wagombea uongozi katika Timu ya Maji Maji wakiandika maswali yaliyokuwa yakiuliuzwa kwa njia ya simu na wasikilizaji kupitia Radio Jogoo
 Baada ya kutoka katika mdahalo
 Picha ya pamoja toka kulia walio simama ni Hamphery Millanzi mgombea nafasi ya mwenyekiti,Said Mangwe wagombea nafasi ya wajumbe,Mohamed Issa mgombea nafasi ya mwenyekiti, Mchele, Tamimu Adamu  mtangazaji wa Radio Jogoo,Mohamed Mtika mgombea nafasi ya wajumbe,Salum Masamaki, John Kabisana mgombea nafasi ya wajumbe na kuoka kulia kwa walio chuchumaa ni Hilda Kapinga mgombe nafasi ya wajumbe, Shekhan Mzaina  na Hosam Ulaya
Humphery Millanzi mgombea nafasi ya mwekiti akiteta jambo na Hilda Kapiga mgombea nafasi ya wajumbe.
Kesho ndiyo siku ambayo itakwenda kuandika historia mpya katika timu ya Maji Maji kwa kufanyika uchaguzi kuanzia saa  saa nne asubuhi na leo ilikuwa ni kujinadi kila mgombea kutoa sera zake mambo yote kesho