Nimesafiri kupitia kituo cha mabasi Ubungo nikashangazwa na kuendelea
kwa zoezi la ukusanyaji wa shilingi 200 kwa kila abiria asiye na tiketi
anayeingia kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo jijini Dar es
salaam.
Ri!!siti kama ibavyoonekana pichani inasema ni ushuru wa kumsindikiza abiria lakini hakuna abiria anayesindikizwa. Mbaya zaidi hata wabeba mizigo wenye toroli na ambao wamevaa sare za kuonesha ni wafanyakazi kituo cha mabasi cha ubungo hutoza pesa nyingi za kuanzia shilingi 1000 kwa kubeba begi kutoka getini kwenda ilipo basi.
Ukiwa getini hapo na hata ndani ya kitu cha mabasi cha Ubungo hasa asubuhi muda wote huwa ni kelele za mabishano kati ya abiria na vijana wanaowataka watoe pesa.
Ukiondoa tatizo hilo bado kituo hiki cha mabasi kikubwa kuliko vyote kinahitaji kupangiliwa matumizi kwa sababu kwa sasa ni kama vile bado pana vurugu tu na ikichanganywa na tatizo la ubovu wa miundombinu yake basi mtu anajuta kupitia Ubungo.
Ni hayo tu wadau