Sunday, June 9, 2013

MKUU WA WILAYA YA SONGEA AENDELEA KUPAMBANA NA WAFANYABIASHARA WANAOPANGA PEMBEZONI MWA BARABARA

 Mkuu wa Wilaya Songea Ndg. Joseph Joseph Mkirikiti akiwapa maelekezo wafanya biashara ambao hufanya biashara zao kwa kupanga kandokando ya barabara kuu kitendo ambacho ni kinyume cha sheria za usalama barabarani.
 Baada ya kupewa maelekezo na mkuu wa wilaya mama huyu ambaye hakufahamika jina lake kwa kuwa ni mwelewa  akaamua kukusanya bidhaa zake na kuelekea maaneo waliyotengewa kufanyia biashara zao ambayo ni Majengo
 Mkuu wa wilaya akiendelea kutoa somo kwa machinga ambao walikuwa upande wa pili kuwa si sahihi kufanya biashara maeneo hayo kwani ni hatari hasa kwa waendesha vyombo vya moto pamoja na watumiaji wengine wa barabara ambao baadhi huwa hawako makini wawapo barabarani .
 Baada ya kutoa soma kwa waelewa na waungwana huwa wanatekeleza na kuondoka kama inavoonekana hapa huyu mfanya biashara akielekea sehemu waliyotengewa kufanya biashara maaeneo ya Majengo.
 Mkuu wa wilaya ya songea Ndg. Joseph Josep Mkirikiti akisalimiana na moja wa vijana wake ambaye amekuwa akikimbizana naye mara kwa mara juu ya kufanyia biashara kandokando ya barabara ikiwa ni pamoja na eneo la Dilux, Soko kuu na kituo kikuu cha Mabasi mjini Songea.
Kijana huyo ambaye hakufahamika jina mara moja alimueleza mkuu wa wilaya kuwa hii sehemu huwa wanapenda kufanya biashara kwani ni sehemu ambayo ni ya mchanganyiko wa watu wengi ambao huwa wanapita katika maeneo hayo pia kwa wasafiri ambao huwa ndio wateja wao wakubwa.
Baada ya  mkuu wa wilaya kusalimiana na rafiki yake ambaye mara kwa mara wamekuwa maeneo tofauti tofauti yasiyo ruhusiwa kufanyia biashara na kijana huyo kumweleza tatizo lake aliamua kumpa fedha zimsaidie kujikimu baada ya kumoona kija huyu ni mchakalikaji wa kutafuta maisha.
Somo linapokolea haina haja ya kutumia nguvu kama inavyoonekana katika picha hiyo hapo juu , Kijana huyo akikusanya biashara yake kwa amani tayari kuelekea katika sehemu husika amabyo wametengewa na serikali kwa ajili ya kufanyia biashara zao.
Hata hivo Mkuu wa wilaya ameendela kusema kuwa eneo wanalofanyia biashara zao  sio eneo salama kwani eneo hilo ni finyu nalinaweza kusababisha ajali kwa watumiaji wa barabara.
Kwa sababu baadhi yao wamekuwa wakipanga biadhaa zao bara barani na kusababisha kuziba njia kama inavyoonekana katika picha hapo juu.
 Aidha Joseph Mkirikiti ametoa ushauri kwa wafanya biashara wadogowadogo maarufu kwa jina la machinga kuwa na umoja kwa kuunda vikundi vyenye uongozi ili kurahisisha mawasiliano yao na mamlaka zilizopo ikiwa ni pamoja na ofisi ya manispaa ya Songea .
Pia amewashauri wafanya biashara hao wadogowadogo kufikiria kupanua wigo wa kufanyia biashara zao badala ya kunga'anga'nia kufanyia biashara hizo katikati ya mji kwani eneo hilo ni finyu.

Habari na Picha kwa Hisani ya www.demashonews.blogspot.com